UKAWA wawasilisha hoja kwa Spika kumng'oa Naibu Spika Dr. Tulia

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,751
239,410
Wabunge wa upinzani wamewasilisha kwa spika wa bunge hoja ya kumng'oa naibu spika , Dr Tulia Ackson kwa kutokuwa na imani naye .
Mbunge wa simanjiro James Ole Millya ndiye aliyebeba jukumu hilo huku akisindikizwa na mbunge wa kibamba , John Mnyika na mbunge wa Konde (CUF) , Said Khatibu Haji , alipowasilisha hoja hiyo kwa Katibu wa bunge Dr Thomas Kashililah.

Chanzo - Mwananchi .

Tetesi zinadokeza kwa zaidi ya nusu ya wabunge wa CCM wanaunga mkono jambo hilo kwa madai ya kuchoshwa na tabia ya naibu spika huyo ya kupindisha kanuni , huku wengine wanadai kwamba hata mchakato wa uteuzi wake hawakuridhishwa nao .

Kama hilo litafanikiwa basi inasemekana kwamba huyu mama ataingia kwenye vitabu vya dunia kwa kuwa naibu spika aliyehudumu kwa muda mfupi zaidi tangu dunia iumbwe .
 
Tatizo ni chama kwanza na c taifa kwanza, cdhani kama wataungwa mkono na chama tawala.
 
Kwa ile michango ya wabunge kumsifia naibu spika, sioni hoja hiyo ikipita. Wameweka matumbo yao mbele kiasi kwamba vichwa havifanyi kazi.

Mbunge anaongea kumsifia naibu spika hadi msikilizaji unaona aibu!
 
Sizani kama itafanikiwa, laba kama ipo ya wananch......maana anaweza kupingwa na watu zaidi ya 40m
 
Huyu dada anayo kazi.Minong'ono ilianza tangu safari ya kuufikia unaibu spika ilipoanza.Ngoja tukae mbele ya luninga zetu maana bunge letu haliishiwi tamthilia.
 
UKAWA bhana! badala mngepambana kupata wabunge wengi mkajidai mnataka uraisi kwa kufikiri Ni rahisi,

Sasa mmegeuka kinyonga kila rangi mpo!
 
Tatizo wabunge wa CCM ni wanafiki sana,ngoja tuone kabla ya kutoa hukumu
 
Bado ni usiku wala hakujakucha poleni sana hii serikali ya magufuli siyo ya kutikiswa.
Kwa hiyo kupeleka hoja ni kuitikisa Serikali?Kuna uhusiano kati ya ktukokuwa na imani na Bunge na kutikisika kwa Serikali?Mwenzako wa kudadavua amakuja na uzi wa Kingunge sikjakuona kule vipi?
 
Kutokana na wabunge kutojielewa itakuwa ni vigumu upinzani kufanikiwa kwenye hiyo hoja ya kupiga kura kutokuwa na imani na naibu Spika Tulia. Wale wabunge wa CCM waliotoka nje siku ile watakuwa wameshaonywa tayari.
 
Haya ni madhara ya kuteua wadhifa nyeti kama wa naibu spika. Anatetea sana intrest ya chama kuliko Taifa.
 
Wabunge wa upinzani wamewasilisha kwa spika wa bunge hoja ya kumng'oa naibu spika , Dr Tulia Ackson kwa kutokuwa na imani naye .
Mbunge wa simanjiro James Ole Millya ndiye aliyebeba jukumu hilo huku akisindikizwa na mbunge wa kibamba , John Mnyika na mbunge wa Konde (CUF) , Said Khatibu Haji , alipowasilisha hoja hiyo kwa Katibu wa bunge Dr Thomas Kashililah.

Hoja yao imeshindwa kabla ya kuwakilisha.Angalia genge lililowakilisha hiyo hoja wote UKAWA!!!! Hakuna hata mbunge mmoja wa CCM!!!
 
Kama hili linawezekana mbona mgombea wa nafasi ya Naibu Spika wa UKAWA alishindwa? Wajipange upya, hizi sarakasi zitawaponza.
 
Back
Top Bottom