Jamani lazima tusema ukweli kwa maslahi ya nchi. Tusikae tunashabikia upumbavu eti chopa sijui kumi. Jamani jamani hivi tunawajali wananchi au atuwajali? . Tazama mshindani wetu amekwenda mwendo wa barabara na angalia idadi ya wananchi aliowafikia. Sisi tunajitapa na chopa. Upuuuzi gani huu. Wapo wanachama wetu kule mahospitalini hawana madawa wala hela ya kujitibu, inaonyesha hatuwajali sisi tunajali maslahi binafsi tu. Halafu tunajitapa tutatetea wanyonge. Wananchi wamezinduka msidhani hawana akili. Narudia kusema wananchi wameerevuka sana tofauti na tunavyofikiri. Tutaionja joto ya jiwe kwenye sanduku la kura