UKAWA wanakesi nzito ya kujibu kwa wananchi hasa linapokuja suala la Uhuru wa kujieleza na ktk wigo mpana wa demokrasia nchini!
Yaweza kuwa ilikuwa bahati mbaya au mpango rasmi wa serikali ya awamu ya 4 kuruhusu Uhuru wa kujieleza, Ila kwa bahati mbaya wanasiasa na wananchi walitumia vibaya mno nafasi hiyo na wengine kuonesha dharau ya hali ya juu kwa utawala wa awamu iliyopita!
Mara kadhaa viongozi wa UKAWA walimdhihaki Mkuu wa nchi tena hata ndani ya bunge, rejea- walipomuita raisi Kikwete dhaifu, simply kwa kuwa na soft approach!
Wanaharakati, wanasiasa na baadhi ya watu binafsi na viongozi wa kidini waliweza hata kulumbana na Mkuu wa nchi, kufikia hata hatua ya kutishia usalama wakati mwingine kwa kutoa matamko makali ambayo hayakuwa salama sana (mfano, rejea vitisho vya maandamano ya nchi nzima yasiyo na kikomo, pia rejea kauli ya Kikwete alipokuwa anaanzisha mjadala wa katiba mpya, kuwa ".....kuna watu walisema patakuwa hapatoshi... Mimi nataka patoshe.....!")
Ni kweli upinzani imara huleta serikali imara!
Ni kweli ukiminya demokrasia basi nchi hudumaa, na pia kuna hatari ya kuzalishwa udikteta!
Lakini demokrasia lazima iwe na mipaka! Wale tuliokuwa tuna-enjoy Uhuru wa kujieleza tulijisahau ktk haki tulizokuwa tunazipata na kusahau wajibu wetu katika kuzilinda nafasi hizo muhimu tulizokuwa tunapata!
Waliopewa dhamana ya kupaza sauti wakatumia nafasi kufanya kampeni na sasa wameishia kuwa wanasiasa! Watu walikuwa wakitoa taarifa muhimu za nchi na kuzichapisha katika media (internet au magazeti) tena hata bila ya kuwa na uhakika au kujali sensitivity ya taarifa wanazotoa!
Kweli ni haki kujieleza au kuuelezea umma yanayojitokeza nchini, hata yakiwa sensitive vipi, lakini je ni kweli huwa hatujali kabisa madhara yatokanayo na taarifa zinazoweza kuathiri mustakabali wa taasisi, nchi au jamii zetu! Nadhani jibu hapana! Pale usalama wa taasisi au ustawi wake unapoweza kutishiwa huwa tunapaswa kuzuia utoaji wa taarifa hizo, rejea kesi ya Zitto na Kitila walipoondolewa chadema hawakufanya uhaini wowote, Bali taarifa walizokuwa wanaziandaa zilikuwa zinatishia ustawi wa chama! Walikuwa sahihi kudeal na watu wanaotishia ustawi wa taasisi yao!
Kabla ya kulaumu serikali ya sasa, je UKAWA na vyama rafiki, mlikuwa au mna mchango gani/mikakati ipi inayowezesha au kuimarisha haki hii ya msingi ya mwanadamu (haki ya Uhuru wa kujieleza) iendelee kuwa exercised lakini bila ya kuathiri ustawi wa taifa/jamii zetu?