UKAWA wamwandama Rais Magufuli

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
RAIS John Magufuli anaandamwa, sasa anatakiwa kuwachukulia hatua wakurugenzi, watendaji na makatibu tawala wa mikoa waliosababisha kuwepo kwa watumishi hewa, anaandika Aisha Amran.

Wabunge na viongozi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wamekuwa wakimtaka Rais Magufuli kuchukua hatua dhidi ya wale wanaofuja fedha za umma.

Safari hii Ruth Mollel, Waziri Kivuli na Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni-Ofisi ya Rais (Utumishi) amesema, endapo Rais Magufuli atashindwa kuwachukulia hatua watumishi hao, atakuwa hajatimiza wajibu wake.

Amesema, sababu inayochangia kuwepo kwa watumishi hewa ni udhaifu wa Tume ya Utumishi wa Umma kutohakiki mfumo wa rasilimali watu pia kukoseka kwa vitendea kazi ili watekeleze jukumu la kuhakiki watumishi wa umma na kisha kutoa taarifa kwa mamlaka husika.

Amesema “watumishi hewa ni tatizo la kutengenezwa kwa makusudi kwani mabilioni yanayopotea kila mwaka kutokana na malipo ya watumishi hewa yanakwenda kwenye mifuko binafsi ya viongozi na watendaji.”

Amesema, licha ya kelele na jitihada zote na taarifa rasmi za kila mwaka za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesaba za Serikali (CAG) kuonesha ukubwa na upana wa tatizo, hakuna kiongozi wala mtendaji wa idara ya serikali au taasisi ambaye amewajibishwa.

“Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri za Serikali za Mitaa ndio waajiri wa watumishi katika halmashauri zao. Kwa sababu hiyo, Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri wanahusika moja kwa moja na uwepo wa watumishi hewa katika mikoa na katika halmashauri za serikali za mitaa.

“Hawa ndio ambao wamepewa jukumu na Rais Magufuli la kuwabaini watumishi hewa katika maeneo yao na kutoa taarifa,” amesema Mollel na kuongeza;

“Tunasubiri kuona hatua zitakazochukulia na Rais Magufuli dhidi ya wakuu wa mikoa na wakurugenzi wa halmashauri ambao kwa makusudi au kwa uzembe wao wamesababisha kuwepo kwa watumishi hewa katika mikoa na halmashauri zao.”
 
Anayetumbua najipu ni JPM anayepanga serikali ni JPM, sasa kiherehere cha nini? kama huna kazi za kufanya si ukae kimya, tumwache Raisi atimize majukumu yake na si kupangiwa.
 
Sasa hili nalo ni la kumtuma Magu wakati ndio wimbo wake au wanataka baadae waseme kama tusingemuambia asingefanya, huyu raia alishajiapiza kukimbia mbio na saa nyingine anapitiliza.
 
Awamu hii mtaandika thread mpaka vidole vipinde, lakini hizo akilinj zenu ndogo watanzania wameshazishtukia , yaani watanzania tunamuelewa Magufuli kuliko maelezo

Badilisheni mbinu, kama prof kitila alivyowashaur la sivyo mtabaki historia

# Hapa KAzi Tu
 
Safi sana mumeipenda wenyewe chaguo lenu wenyewe kampeni zenu wenyewe magufuli ili ashinde sasa aaaanawatumbua eeeeh..! _anawatumbua ccm mbele kwa mbele hapo naona waliompigia kampeni MH sasa lazima itakuwa wanajuta kwa nini walimfagilia mana panga limewarudi hahahahahahahahah wanaisoma wenyewe

Vibaka wa ccm na watumbuliwe tu mana hamna namna
 
Awamu hii mtaandika thread mpaka vidole vipinde, lakini hizo akilinj zenu ndogo watanzania wameshazishtukia , yaani watanzania tunamuelewa Magufuli kuliko maelezo

Badilisheni mbinu, kama prof kitila alivyowashaur la sivyo mtabaki historia

# Hapa KAzi Tu
Tatizo sio magu tatizo ccm ni kiwanda cha wezi
Na upinzani kumuhimiza rais ni kawaida tu sababu hayo anayoimizwa siyo ya ukoo wala family ni kwa manufaa ya watanzania iwe mimi au wewe na yule
 
Tatizo sio magu tatizo ccm ni kiwanda cha wezi
Na upinzani kumuhimiza rais ni kawaida tu sababu hayo anayoimizwa siyo ya ukoo wala family ni kwa manufaa ya watanzania iwe mimi au wewe na yule
Kumbuka hii ni serikali ya Magufuli
 
Swala la watumishi hewa kai raise magufuli mwenyewe, na ataimaliza yeye na wasaidizi wake, msijifanye mnamfundisha kazi kumbe hamna la kuisemea serikali kwa wananchi, saa zingine watu wanawaona kama vikojozi flan...kama hauna jipya kaa kimya
 
ccm damu
 
Kai ndio nani raise ni nani? Wacha kutumika na maigizo man
 
Back
Top Bottom