UKAWA wamdhalilisha Paul Makonda

UKAWA wamdhalilisha Paul Makonda

Hiii simulizi mzuri Sana maana unajua kutunga vitu vitamu tunga nyingine tena
 
Makonda anakiherehere sana. na amezoe kutumiwa tu. Hajui kupima kina cha maji kama ni saizi yake
Ukisema ana kiherehere ni kama umampa kasifa fulani. Makonda ni mjinga. Na sisi kwenye ukoo wetu tumeazimia yeyote atayekuwa mwanaCCM katika ukoo wetu hatutamtambua hadi atakapojiondoa katika chama hicho, maana anaweza kuleta mkosi katika ukoo. Makonda katika karata ni gharasa ama lile li joker!
 
CCM mwaka ujao watakuwa kama yule mama wa malawi, alisema uchaguzi ni batili wakati hana authority! shame chama cha mafisadi (CCM).
 
Mjumbe wa bunge maalum la katiba ambaye pia ni katibu wa chipukizi taifa wa chama cha mapinduzi Paul Makonda kupata wakati mgumu akijaribu kufuta nyayo za UKAWA baada ya kuzomewa na wananchi na kuondoka katika mkutano wakimuacha jukwaani akishindwa kuhutubia mkutano huo alipopanda kujibu swali kuhusu katiba mpya.


Nukuu ya Nyerere ilitumika kumdhoofisha na kushindwa kuhutubia mkutano hadi ukavunjika huku wananchi wa mjini Geita wakiwaomba Ukawa waendelee kuwaelimisha wananchi kuheshimu maoni ya jaji Warioba na kuacha kuwahadaa wananchi kama ambavyo chama cha mapinduzi kimewahadaa katika mkutano huo.


Tukio hilo lilitokea jana katika mkutano wa hadhara wa chama cha Mapinduzi uliofanyika katika viwanja vya soko kuu wilayani Geita ikiwa ni mwendelezo wa chama hicho kushawishi wananchi kuhusu muundo wa serikali mbili katika katiba mpya kama ccm inavyopendekeza.


Baada ya mwenyekiti wa ccm mkoa wa Geita Joseph Musukuma kumaliza kuhutubia wananchi,aliomba wananchi kumi waulize maswali ili ayapatie majibu,ambapo kijana mmoja ambaye hakujitambulisha jina lake,aliuliza swali lililoonekana kuwakera viongozi wa chama hicho na kumfukuza aondoke mbele ya jukwaa .


Kabla ya kuuliza swali kijana huyo alisema……..
"Mheshimiwa mwenyekiti wa mkoa,Jaji Warioba na timu yake ya mabadiliko ya katiba walizunguka nchi nzima wanakusanya maoni yetu na ndiyo yaliyo andikwa kwenye rasmu,hata hivyo, baba wa taifa Julius Nyerere aliwahi kusema kwamba,kama kuna watu wanao dhani katiba mpya haitungwi na wananchi basi watu hao ni wapumbavu".
Kabla hajamaliza kuuliza swali hilo,Katibu mwenezi wa ccm mkoa wa Geita Said Kalidushi alimnyang'anya kipaza sauti kijana huyo na kumfukuza aondoke huku watu wakizomea kama ishara ya kupinga kinachofanywa na kiongozi huyo.


Baada ya mwenyekiti kugundua kuwa wananchi hawakufurahishwa na kitendo hicho,alipopanda jukwaani kujibu maswali alilazimika kumuita tena kijana huyo aendelee kuuliza swali hilo huku akiomba swali lijibiwe na Pul Makonda.


"Baba wa taifa Julius Nyerere aliwahi kusema kuwa ,wale wanaodhani katiba mpya haitungwi na wananchi ,basi watu hao ni wapumbavu,na nyie ccm mnapinga maoni ya wananchi tuliyotoa kwa Tume ya Warioba,…swali langu ni je,na nyie ccm ni wapumbavu kama alivyosema baba wa taifa? maana nyie mnakataa maoni yetu na mnasema katiba haitungwi na wananchi ila inatungwa na bunge la katiba"?
Baada ya swali hilo, umati wa mkutano huo ulilipuka kwa kuzomea na kumshangilia kijana huyo kuashiria kuwa wamekubaliana na alichouliza kijana huyo.


Mjumbe wa bunge maalum la katiba ambaye pia ni katibu wa chipukizi taifa wa chama cha mapinduzi Paul Makonda alipopanda jukwaani kujibu swali, ghafla wananchi walianza kuzomea na kuondoka katika mkutano huo huku Makonda akipigwa na butwaa na kushindwa kuendelee kuhutubia na kulazimika kushuka jukwaa bila kutoa majibu ya swali hilo.


Tukio hilo lilitafsiriwa kama ni ishara kwamba watu wengi waliokuwepo katika mkutano huo pamoja na kwamba uliitishwa na ccm lakini wanapenda muundo wa serikali tatu katika katiba mpya ijayo.


Mkutano huo wa ccm ulilenga kufuta nyayo za mikutano iliyofanywa na viongozi wa umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) iliyofanyika mwezi jana katika mkoa wa Geita ikiongozwa na Dr. Wilbroad Slaa
 
Bado wataipata hawa magambaz, watumie rasilimali za hii nchi vibaya bado watuibie na maoni yetu?
 
Huyo msukuma bure kabisa. kakimbilia mganza na kumwamurisha mkuu wa wilaya ya Chato kumukamata mtendaji na diwani wa CDM Mganza. amakweli ukiwa ccm ni tabu
 
Hakuna shaka kuwa Ridhiwani kikwete mtoto wa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania ni miongoni mwa matajiri wakubwa nchini,Ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha DSM fani ya sheria,ajamaliza hata miaka 5 tangu amalize chuoni pale.Hamejilimbikizia mali isiyopimika kupitia kodi ya wananchi(watanzania) kwa mgongo wa baba yake mzazi mh Jakaya Mrisho Kikwete.Utajiri alionao haupimiki kutokana na ukubwa wake,utajiri anoumiliki kamwe hata kama unapata faida ya milioni moja kwa siku moja usingekuwa una utajiri huo.Mojawapo ya utajiri mkubwa alionao ni pamoja na magari makubwa ya kusafirisha mafuta nchi mbali za kusini mwa africa.Pia ni mmlikiki wa benk ya AMANA BANK,ni mmiliki wa vituo vya mafuta vya LAKE TANZANIA LTD.nchi nzima.Hizo ni baadhi tu lakini.tambua kuwa wewe umejinufaisha kupitia kodi ya watanzania ila kumbuka kuna anayetafuta hata tshs 500 ya mlo wa usiku hana,kuna anayetembea ------ nje,kuna anayetafuta shs 300 ya kununulia panadol hana kabisa,vilio vya hawa watu vitakufata popote ulipo ndani na nje ya nchi.Hivi sio vilio vya kawaida,watu wanaishi katika hali ngumu kimaisha huku wewe unafaidi kodi zao unaishi maisha ya hali ya juu kupindukia.serikali inapeleka majeshi kupigana ili kuwafulumua waasi ili magari yake ya kusafirisha bidhaa hadi kongo yaende kwa usalama,watanzania kumbuka chochote unachonunua unachangia maendeleo ya familia za baadhi ya viongozi nchini,

kilio cha watanzania kitakufata popote ulipo.
 
Tatizo la Makonda ni mbishi,
alitakiwa aombe fungu awanunue vijana pale Geita waje kwa wingi kwenye
mkutano wake huku wakihamaisha kama wanavyofanya wakubwa zake!! Sasa
aibu hiyo eti kujipima na DR. Slaa!!

nifahamisheni huyu makonda ndio nani? navyojua geita wanamsikiliza musukuma tu, sasa yeye katokea wapi?
 
Wamgemlokotoa na mawe kabisa

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Mara zote huwa nasema ccm ni janga la kitaifa watu wanakuwa wagumu kuelewa,sasa nafikiri mmeyaona yanayoendelea hapo geita,ccm hawana jipya wamechoka,miaka hamsini hakuna la maana walilofanya zaidi ya ufisadi maeneo mbali mbali,peoplesssssss powerrrrr,toeni kura kwa vyama vya upinzani vilivyoungana yaani ukawa
 
Back
Top Bottom