UKAWA wamchokoza Rais Magufuli

UKAWA wamchokoza Rais Magufuli

Kwa hiyo na bungeni sasa tutegemee maamuzi ya kukurupuka kama ya serikali. Rais Magufuli, Mambo ya Ndani Mwigulu na Spika wa Bunge Tulia...duh, Watanzania tutakoma!
Hatutakubali kijinga , tutapambana mpaka tone la mwisho .
 
Ukiona kuna malalamiko ujue kazi inafanyika, Tumwache Rais atimize wajibu wake !!
 
Ni utawala wa kimabavu ili kuhakikisha Wabunge wa upinzani wanatishwa kwa kila namna mpaka wasalimu amri kwamba Bunge ni tawi la CCM linaloendeshwa na remote control toka Ikulu.
Wasichojua ni kuwa, kutumia dola ku-deal na wapinzani ni sawa na kumpiga teke chura.
 
It is absolutely true.

Haiingii akilini kwa huyo mdada ambaye anasemekana ana PhD ya sheria, halafu ashindwe kuielewa principle ya natural justice inayosema Man can not be a judge on his own case.
Utafiti kidogo unaonesha kwamba wengi wa Maprofesa Tanzania walikuwa ni vihiyo shule za awali tena wengine vihiyo wa kutupwa. Ni asilimia ndogo sana ambao walionesha uwezo toka primary hadi sekondari na hawa wengi wao hawataki kujihusisha na siasa. Lakini walio wengi ni wale ambao walikuja kujiunga na masomo ya chuo kikuu kwa njia zisizoeleweka kwa sababu tu wazazi wao walikuwa na uwezo.

Kama matokeo ya darasa la saba, form four na form six ya maprofesa wetu wengi yangeanikwa, ungekuta waliofaulu vizuri bila kubebwa ni asilimia chini ya 30%. Wengi ama walipelekwa nje na wakarudi na uprofesa au walisoma kwa kuunga unga na baadaye kuibuka na uprofesa. Mfano mzuri ni huyu mtoto wa Mkuu aliyeko UDOM ambaye inawezekana ndani ya miaka minne au mitano akautwaa udokta/uprofesa kiulaini!
 
Kwa hiyo na bungeni sasa tutegemee maamuzi ya kukurupuka kama ya serikali. Rais Magufuli, Mambo ya Ndani Mwigulu na Spika wa Bunge Tulia...duh, Watanzania tutakoma!

Hiyo inaitwa one man show..
 
Watanzania ni watu wenye kiwango kikubwa cha unafiki, kuna watu walisema ikulu inaendeshwa na remote kutoka msoga, masikini! wameyakana maneno yao tena, mara JPM anamuabisha JK, hatumii busara, anataka kujipatia sifa ili mwenzake aonekane hakufanya kitu.
Wimbo umegeuka sasa....demokrasia! Rais dikteta anatimua watu hovyo....ala! kesho wamesahau, mbona hajamtimua Kitwanga? hapa hawako tayar kuhoji, je mamlaka husika zimemkamata na kosa?.... Kalewa, katiwa pingu,....kaonewaa!!!.... kwani yeye peke yake ndio anakunywa pombe? Rais ni dikteta hafati sheria......bungeni sheria zimekiukwa mtu katiwa korokoroni, hakuna demokrasia wabunge wanafukuzwa hovyo tu, hapa hawataki kujua sheria ilikiukwa au la!
Rais ashauriwe anyamaze na afanye kazi, hii mikutano ya vyama iruhusiwe tu tena wapewe na ulinzi kama katiba inavyotaka, atambue sisi ni wanafiki, likiisha hili utasikia Rais ananyamaza tu hasemi chochote.
Umasikini wetu sio bahati mbaya, kwa tabia za watanzania ingekuwa ajabu kama tusingekuwa masikini, tulistahili kuwa hivyo.
 
magufuli mkabila sana aisee ameona ampeleke msukuma aanatoka mkoani kwake geita daa
 
UKAWA wamchokoza Rais Magufuli


Rais John Magufuli

WABUNGE walio katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) jana walimtuhumu Rais John Magufuli kuwa analiendesha Bunge kutokea Ikulu kwa kumtumia Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson.

Wakizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya habari ya Bunge, wabunge hao walisema wanachokiona bungeni ni Rais Magufuli akiwa kama Spika wa Bunge huku viongozi wengine wa Bunge wakiwa ni matawi yake.

Wa kwanza kutoa tuhuma hizo katika mkutano huo uliohudhuriwa na wabunge wengi wa Ukawa alikuwa Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara ambaye alisema Bunge la 11 haliko huru kwa sababu maamuzi yake yanatolewa na Rais Magufuli kutoka Ikulu kupitia Naibu Spika, Dk. Ackson.

“Bunge linaongozwa na Magufuli (Rais John) kutoka Ikulu moja kwa moja kupitia Dk. Tulia, Rais ndiye Spika wengine ni matawi tu, mfano tukiangalia mwongozo wa posho za wabunge wa upinzani uliotolewa juzi, umetolewa uamuzi mara mbili, haiwezekani kitu kimoja kikatolewa maelezo mawili tofauti ni wazi kuwa anafuata maagizo kutoka juu,” alisema Waitara.

Alisema hivi sasa kuna mhimili mmoja wa dola ambao ni Serikali Kuu kwa sababu maamuzi yote yanatolewa na chombo hicho huku akilitaja Bunge kuwa tawi la Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema Naibu Spika, Dk. Tulia hakupaswa kutoa uamuzi wa wabunge wa Ukawa kutolipwa posho kwa sababu ni mtuhumiwa wa jambo hilo.

“Kutomwita mheshimiwa tunamaanisha na tungekuwa na jina baya zaidi tungemwita, nina wasiwasi na PhD yake ya sheria, sijawahi kuona mtu anayelalamikiwa anatoa hukumu sijawahi kuona, yeye ni mtuhumiwa anatoaje uamuzi. Bora Spika Job Ndugai arudi,” alisema Waitara.

Katika mwendelezo wa tuhuma zake hizo, alisema Naibu Spika, Dk. Tulia aliteuliwa kimkakati na Rais Magufuli na amekuwa akiongoza matukio mbalimbali yanayogharimu wananchi.

“Naibu Spika ni Mbunge wa ‘Voda Faster’, aligombea uspika CCM wakamkataa, baada ya kuona amekataliwa Rais akaamua kumpa ubunge ili aje kugombea nafasi ya Naibu Spika ambayo nayo ameilazimisha hata CCM walikuwa hawamtaki,” alituhumu Waitara.

Waitara alienda mbali zaidi kwa kumtuhumu Dk. Tulia kuwa miongoni mwa watu waliovuruga mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya kwa kushiriki kukata maoni ya wananchi na kubakiza yaliyotolewa na CCM.


Katika mlolongo huo wa tuhuma, Waitara aliendelea kutuhumu kuwa Dk. Tulia alishiriki kuwanyima haki ya kulinda matokeo ya kura kwa kuwataka wananchi kukaa umbali wa mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Aliendelea kusema kuwa pia alishiriki kurudisha Sh bilioni 12 Ikulu bila kumshirikisha Spika Ndugai.

Kwa upande wa Mbunge wa Vunjo, James Mbatia, alisema Serikali haiheshimu maamuzi wabunge na kwa mara kadhaa Rais Magufuli amekuwa akitoa uamuzi bila kuwashirikisha.

“Bunge linakaa na kujadili bajeti na kupitisha lakini Serikali haiheshimu na haitekelezi, kuna haja gani ya kuwa na mhimili wa Bunge? Dk. Magufuli (Rais John) amekuwa akifanya maamuzi yake mwenyewe ya kuchukua fedha na kuzigawa katika taasisi mbalimbali bila kupitishwa na Bunge jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

“Kinachotushangaza ni fedha zinazobaki katika taasisi mbalimbali kupelekwa Ikulu wakati zinapaswa kurudi Hazina, anapelekewa yeye ndiye Hazina? Rais hapaswi kuzipangia fedha kazi kabla ya kupitishwa na Bunge, hakuna haja ya kuwa na huu mhimili kama unaingiliwa kiasi hiki,” alisema Mbatia.

Mbatia alisema msimamo wa Ukawa ni kufutwa kwa posho na endapo Serikali itapitisha hoja ya kukatwa kwa kodi mafao ya wabunge inapaswa iwakate viongozi wa ngazi zote waliotajwa katika sheria hiyo.

“Sheria mafao ya wabunge inahusu viongozi wote wa kisiasa, pia inaenda sambamba na pensheni ya Rais, Makamu wa Rais, mawaziri, Spika, Naibu Spika, wakuu wa mikoa na wilaya, iweje wachague wabunge tu kuwakata kodi kama ni hivyo wawakate viongozi wote waliotajwa ndiyo watakuwa wametenda haki,” alisema Mbatia.

SOURCE: Mwanahalisi
Kusema ukweli ndio uchokozi?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hebu twambie hiyo kazi inayofanyika, zaidi ya udikteta na sera za ukurupukaji ambazo hazina tija kwa Taifa.
Hata hiyo tofauti ya kiuongozi ya muda mfupi inayojionesha ni kazi.
Kinacholeta utofauti ni majina, we unaita udikteta, mi naiona ni kazi.
Ni mapema kufanya summative evaluation
 
Back
Top Bottom