UKAWA walishukia gazeti la Mtanzania, wasema wapo gado

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Viongozi wa Vyama Vikuu vya Upinzani vinavyounda (UKAWA) Vimekanusha Uvumi unaoenezwa na Vyombo vya Habari kuwa Miongoni mwa Chama cha siasa kinachounda umoja huo ambacho ni NCCR Mageuzi kwamba kimetoa hoja ya kujitoa kwenye umoja Huo, na kusema huo ni upotoshaji Wa Vyombo vya Habari ambavyo vinatumiwa na Chama cha Mapinduzi CCM.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.

Kauli hiyo ya (UKAWA) inakuja ikiwa ,Gazeti la moja linalotoka kila siku Gazeti la Mtanzania toreo la leo Tarehe 29-mwezi wa nne mwaka huu bila ya kutaja chanzo cha uhakika kimeripoti Habari kwamba Vyama hivyo vikuu vya Upinzania vimeshindwa kufikia muhafaka kwenye ugawaji wa Majimbo na kudai kwamba Chama cha NCCR mageuzi kimepeleka hoja ya kujitoa kwenye Umoja huo.

Wakikanusha taarifa hizo leo ,wakati wakizungumza na Mtadao huu kwa Nyakati Tofauti viongozi wa Ukawa unaoundwa na Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD wameonyesha kusikitishwa na Taarifa wanaodai ni ya kuzushi na zenye uwongo na kushangaa kuripotiwa kwenye Gazeti ambalo wanasema limejaa wahariri mahiri nchini.

Wa kwaza kukanusha Taarifa hiyo ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dokta Wilboard Slaa ambapo amesema taarifa hizo zinalengo la kuwavunja nguvu Watanzania kulekea kipindi hiki anachodai wanakwenda kushika Dola.
"Nashangaa sana hicho kigazeti kuandika Taarifa ya uzushi kama hiyo,wakati ukweli ni kwamba kwa sasa tumefikia asilimia 84 ya makubaliano ambayo tunakwenda vizuri sana na tena tupo kamili kuhakikisha tunautoa utawala huu mbuvu wa CCM,leo anakuja mtu kwa kutumiwa huko anakuja na taarifa za uongo kama hizo"Amesema Dokta Slaa.

Dokta Slaa ameongeza kuwa hata Hoja ambayo wanasema kwa Chama mwenza wa Ukawa ambao ni NCCR Mageuzi kutoridhika na Ugawaji wa Majimbo ya Ubunge kwenye Uchaguzi wa hapo baadae na kusema kwamba wala kwenye Kikao kilichofanyika jana Jijini hapa ambacho pia leo kinaendelea, wala hakijavunjika na wala chama cha NCCR hawajasema wataka kujitoa.

"Kwanza kikao cha Jana tulichokutana na Viongozi wenzetu wa Ukawa hakijavunjika kama wanavyodai kwani hiyo hoja ya Ugawaji wa Majimbo hatujazungumzia kwenye kiako hicho,kwani siku nzima tulizungumzia namna ya kupata vyanzo vya pesa ili tuweze kufanya Kampeni nchi nzima sasa huyo mwandishi wa Habari katoa wapi Taarifa hizo"ameendelea kusema Dokta Slaa.

Mwandishi wa Mtandao huu alipumuuliza ni Majimbo gani ambayo wanashindwa kufikiana,Dokta Slaa amesema hawezi kujibu swali hilo kwani hayo ni mambo ya ndani ya Umoja huo na akawataka Watanzania kuwa na subira wakati viongozi hao wakiweka mambo sawa na kudai UKAWA watatoa wagombea Bora ambao anazidi dai watahakikisha wanaitoa CCM Madarakani.

Kwa upande wake Mbunge wa Kigoma Kusin David Kafulila ambaye pia ni Mjumbe wa kamati kuu ya NCCR-Mageuzi naye amekanusha taaria hizo kwamba Chama hicho kimepeleka hoja za kujitoa kwenye UKAWA.

"Kiukweli mimi nashangaa taarifa za upotoshaji kwenye Gazeti kama hilo,wakati ukweli ni kwamba UKAWA tumefikia asilimia 84 ya makubaliano na wenzetu,eti leo tujitoe,maana sisi tutakuwa watu wa ajabu sana ukweli ni kwamba hatujawai peleka hoja hizo na vilevile,tupo kwenye asilimia za mwisho"amesema Kafulila.

Mbunge Kafulila amebanisha kuwa kwa sasa umoja huo unaweka mipango ambayo anasema ni mizuri ya kuhakikisha kushinda kwa kishindo kwenye uchaguzi Mkuu hapo baadae na kuwataka Watanzania kupuuza Taarifa ambazo anaziita ni za kizushi.

Naye Kiongozi Mmoja wa Juu wa Chama cha Wananchi CUF aliyezungumza na Mtandao kwa sharti la kutotaja jina lake kwenye mtandao huu ambapo amfichua siri ambayo anasema kwa sasa Chama cha Mapinduzi CCM kimepeleka Fungu la pesa kwa waandishi wa Habari pamoja na Wahariri kuandika Habari za upotoshaji juu ya UKAWA ili kuwapa hofu wananchi na hata alipoiona Taarifa hiyo kwenye Gazeti la Mtanzania amedai kuwa hakuweza shangaa.

Chanzo: Fullhabari
 
niliona hilo gazeti ila nilijua ni UONGO MTUPU NA PIA NI JANJA YA CCM HASA BAADA YA KUZIDIWA KETE. KWANI KINANA AMESHAMALIZA KUIMARISHA CCM UKAWA WANAPITA ALIPOPITA KUIBOMOA CCM. KINANA AKIPITA TENA ATAZOMEWA HIVYO NILIJUA NI JANJA TU YA CCM
 
Hii habari imefanya naenda lunch nikiwa na amani moyoni, maana niliposoma ule upuuzi wa wahariri wa magazeti ya Bashe kidogo tu nimpigie Dr Wangu simu kuwa mapigo ya moyo yanadunda kama ngoma za kizaramo......Tnx God kwa hili tamko.
 
Maskini wee. Mhariri Kibanda amekuwaje tena? Mtu aliyepata tuzo ya kutetea haki za binadamu anatumika na mafisadi wa CCM. Ama kweli tumikia "kafirii" upate maradi wako.
 


Naye Kiongozi Mmoja wa Juu wa Chama cha Wananchi CUF aliyezungumza na Mtandao kwa sharti la kutotaja jina lake kwenye mtandao huu ambapo amfichua siri ambayo anasema kwa sasa Chama cha Mapinduzi CCM kimepeleka
Fungu la pesa kwa waandishi wa Habari pamoja na Wahariri kuandika Habari za upotoshaji juu ya UKAWA ili kuwapa hofu wananchi na hata alipoiona Taarifa hiyo kwenye Gazeti la Mtanzania amedai kuwa hakuweza shangaa.

Chanzo: Fullhabari
Wataliwa sana pesa, watu wakishaamua wameshaamua, ni vigumu mno kuwapindua kwa njia hiyo, CCM tuliipenda mno....
 
Nimepenyezwa habari kwamba waandishi wa gazeti hilo waliokwenda ku-cucover ule mkutano wa UKAWA ni wafuasi wa ZZK.
 
wahariri wa hili gazeti niliwaona maboya walipoweka kwenye ukurasa wa mbele kuwa ''walinzi wa chadema wakamatwa na silaha za kivita'' yaani jumapili kumefanyika sherehe za sikukuku ya muungano jtatu unaweka habari za kipropaganda wakati kulikua na habari kubwa.....niliwadharau bashe pamoja na team yake
 
Nimefurahi sana kupata kanusho hili mapema!! Inatakiwa kujiimarisha zaidi upande wa habari ili kuondoa sintofahamu zitakazoletwa na haya majizi ya ccm kwani zipo nyingi zinakuja!!

ASANTENI SANA UKAWA!!
 
Yaani mie wala sikupata presha wala shaka.. Niliijua toka mwanzo habari zile ni za uongo.. Swali ninalojiuliza tu hapa ni kwa mhariri na mwandishi wa habari zile kuleta na kuruhusu kuchapwa kwa habari ambazo walikuwa wanajua kwa asilimia 100 ni za uongo, wanajisikiaje mioyoni mwao kwa kusaliti maadili ya kazi zao (ambazo ni muhimu sana) kwa ajili ya visenti..? Wanajisikiaje wananchi wanapalalamika ukanjanja wa waandishi wa habari..?
 
Back
Top Bottom