UKAWA wakubaliana kuwanyima mafuta wakuu wa Wilaya

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ameagiza wenyeviti wa halmashauri 18 nchini zinazoongozwa na UKAWA kuacha utaratibu wa kutoa fedha za halmashauri kuwasaidia mafuta ya magari wakuu wa wilaya au kuzitumia kwa ajili ya masuala ya kisiasa ya vyama vyao.

Akizungumza na mameya na wenyeviti wa halmashauri zinazoongozwa na Ukawa katika mkutano uliofanyika juzi mjini Arusha, Mbowe alisema viongozi hao wanapaswa kuhakikisha fedha zote zinazokusanywa na halmashauri hizo zinatumika kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Alisema katika kikao hicho cha mameya na wenyeviti wa halmashauri, wametambua kuwa kuna matumizi mabaya ndani ya Serikali, mbali na wafanyakazi hewa ambao wapinzani wamekuwa wakilalamika tangu mwaka 2005.

Mbowe alisema bado kuna halmashauri ambazo zimekuwa zikitumia fedha kufadhili ofisi za wakuu wa wilaya na chama tawala, jambo ambalo sasa kwa halmashauri za UKAWA halitakuwapo.

“Maeneo ambayo wakuu wa wilaya wamezoea kuomba fedha za mafuta na CCM wamekuwa wakiomba fedha kwa ajili ya kazi zao tunawaambia wasithubutu tena kwenda kwenye halmashauri zinazoongozwa na UKAWA, kwani hatutawapa fedha na tunawaumbua,” alisema.

Mbowe alisema katika halmashauri za UKAWA hawataki kusikia kuna fedha zimetolewa kwa wakuu wa wilaya au chama chochote cha siasa.
Alisema katika kikao hicho wamekubaliana kuanzisha mipango mikakati ambayo itawezesha kubuniwa vyanzo vipya vya mapato ambavyo ni rafiki kwa wananchi, kupatikana kwa ajira na kuboresha huduma muhimu za Watanzania.

Akizungumza baada ya maelekezo hayo, Mwenyekiti wa Madiwani CHADEMA nchini ambaye pia ni Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro alisema watatekeleza na hawatakubali kuingiliwa na wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa na makatibu tawala.

Calist alisema katika halmashauri za UKAWA uamuzi wa mwisho wa uendeshaji wa halmashauri utafanywa na madiwani na siyo mtu kutoka nje ya halmashauri hizo.

“Tutasimama na kutetea mamlaka ya kisheria ya Serikali za mitaa hapa nchini,” alisema.

Katibu wa Madiwani wa UKAWA nchi nzima ambaye ni Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob alisema watahakikisha wanasimamia utendaji mzuri wa halmashauri zote wanazoziongoza ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.
Muanze na halmashauri ya Hai kwa mkiti wenu kwanini ilipata hati chafu?
 
Wakuu wa wilaya hawapo kikati a,ni matumizi mabovu,na kama ni makada basi chama cha mkuu wa wilaya kitoe fedha,pia kwakuwa kazi yao ni ya siasa na sasa siasa ni STOP fedha za nini kwao.
 
Mimi ninavyojua, Mkurugenzi wa Halmashauri iwe Wilaya, Mji, Mkoa au Jiji ndiye mwenye fungu la fedha na si mwenyekiti, au huo utaratibu siku hizi umebadilishwa?

Mipango ya matumizi ya hizo fedha inaidhinishwa na baraza la madiwani.
 
Hicho kikao kilifanyika hotelini kwa nani? Kwa nn kifanyike arusha wakati makao makuu yako dar?
 
Kumbukeni kwenye halmashauri kuna fungu kwa ajili ya oc. Fungu hili ni kweli linapitishwa na madiwani lakini namna linavyotumika ajuaye ni ded na technical staffs wake na hapo ndo viongozi kama dc anapoingia na hasa pale anapokuwa akifanya kazi za halmashauri passee. Ni kweli pia kwamba dc ana budget yake lakini kwa vyovyote vile na kwa baadhi ya shughuli lazima dc ataingizwa.
Unaongelea mazoea, hilo fungu linapitishwa na nani na nani anapaswa kusimamia matumizi yake?
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ameagiza wenyeviti wa halmashauri 18 nchini zinazoongozwa na UKAWA kuacha utaratibu wa kutoa fedha za halmashauri kuwasaidia mafuta ya magari wakuu wa wilaya au kuzitumia kwa ajili ya masuala ya kisiasa ya vyama vyao.

Akizungumza na mameya na wenyeviti wa halmashauri zinazoongozwa na Ukawa katika mkutano uliofanyika juzi mjini Arusha, Mbowe alisema viongozi hao wanapaswa kuhakikisha fedha zote zinazokusanywa na halmashauri hizo zinatumika kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Alisema katika kikao hicho cha mameya na wenyeviti wa halmashauri, wametambua kuwa kuna matumizi mabaya ndani ya Serikali, mbali na wafanyakazi hewa ambao wapinzani wamekuwa wakilalamika tangu mwaka 2005.

Mbowe alisema bado kuna halmashauri ambazo zimekuwa zikitumia fedha kufadhili ofisi za wakuu wa wilaya na chama tawala, jambo ambalo sasa kwa halmashauri za UKAWA halitakuwapo.

“Maeneo ambayo wakuu wa wilaya wamezoea kuomba fedha za mafuta na CCM wamekuwa wakiomba fedha kwa ajili ya kazi zao tunawaambia wasithubutu tena kwenda kwenye halmashauri zinazoongozwa na UKAWA, kwani hatutawapa fedha na tunawaumbua,” alisema.

Mbowe alisema katika halmashauri za UKAWA hawataki kusikia kuna fedha zimetolewa kwa wakuu wa wilaya au chama chochote cha siasa.
Alisema katika kikao hicho wamekubaliana kuanzisha mipango mikakati ambayo itawezesha kubuniwa vyanzo vipya vya mapato ambavyo ni rafiki kwa wananchi, kupatikana kwa ajira na kuboresha huduma muhimu za Watanzania.

Akizungumza baada ya maelekezo hayo, Mwenyekiti wa Madiwani CHADEMA nchini ambaye pia ni Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro alisema watatekeleza na hawatakubali kuingiliwa na wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa na makatibu tawala.

Calist alisema katika halmashauri za UKAWA uamuzi wa mwisho wa uendeshaji wa halmashauri utafanywa na madiwani na siyo mtu kutoka nje ya halmashauri hizo.

“Tutasimama na kutetea mamlaka ya kisheria ya Serikali za mitaa hapa nchini,” alisema.

Katibu wa Madiwani wa UKAWA nchi nzima ambaye ni Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob alisema watahakikisha wanasimamia utendaji mzuri wa halmashauri zote wanazoziongoza ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.
Nafikili uchaguzi umeisha. Sasa ni wakati wa kushilikiana kuijenga Tanzania bila ya kujali vyama vyetu. Maana sote dhamila yetu ni kuiona Tanzania ikipiga hatua kubwa kimaendeleo.
 
Madiwani ni sawa na wabunge sio waajiriwa wala watendaji wa serikali.Meya ni sawa na spika wa bunge yeye ni spika wa baraza la madiwani si mtendaji wala mwajiriwa wa halmashauri.Naona hicho kikao chao koko wameongelea utendaji AS IF mameya na madiwani ni watendaji na waajiriwa wa Halmashauri.Kwa hiyo yakija malipo watagoma kuidhinisha na kulipa!!!! Hivi wanajua mipaka yao?
labda sijakuelewa vizuri,kwa hiyo kwa maneno yako mwamuzi wa matumizi ya fedha za halmashauri/mji au jiji ni mkurugenzi ?naomba uniweke sawa.
 
Back
Top Bottom