Vijana wengi waliokuwa wakiunga mkono ukawa wengi wamesema kuwa kweli CCM ni chama dola na kitapata ushindi wa Tsunami baada ya kugundua kuwa mafuriko ya mgombea wa UKAWA yalikuwa yakiandaliwa. Wengine wamesema kuwa UKAWA ni Muunganiko wa vyama vinne lakini CCM ni kimoja ila watu kwenye mikutano ya CCM bado ni wengi sana karibu kila kona.
Kwa kweli tuache ubishi CCM mbele kwa mbele.
Tume imesitisha na kuwasimamisha wote waliokuwa wanaandaa karatasi za majumuisho ya matokeo ya upigaji kura. Inavyoonekana ni katika mikakati ya bao la mkono. Tume kwa sasa wengi hawaelewani kutokana na baadhi ya wakubwa kufanya mambo waliyoelekezwa na MaCCM tofauti na ilivyokuwa mwanzo na bila kufuata utaratibu wa Tume. Hawa wasimamizi wa Tume waliokuwa wanatakiwa wakasimamie upigaji kura wamesimamishwa na kuzuiwa kwenda kwenye vituo vya kupigia kura licha ya kupewa mafunzo ya siku mbili juu ya usimamizi wa kura. Sababu ya kusimamishwa kwao ni kutokana na wengi wao kuuliza inakuwaje unapoingiza matokeo ya waliopiga kura, kwenye system inatoa idadi tofauti??? Hamwoni kuwa mtatuletea matatizo tutakapokuwa vituoni??
Hawa wafanyakazi wa Tume wanadai malipo yao ya mishahara ya miezi mitatu mpaka sasa hawajalipwa na wamesimamishwa mpaka January 2016 bila kujua watalipwaje pesa zao. Kumbuka tume ilivyopewa mabilioni lakini wameshindwa kuwalipa hata hawa wafanyakazi wao. Wanafanya kazi katika mazingira magumu huku viongozi wao wakijilipa maposho kibao na wengine kuhama kwenye nyumba zao na kuishi mahotelini eti kwa kazi maalum. Mfano:- Waliopiga kura ni 100, Kinachotakiwa ukiingiza namba isomeke 100. Tofauti yake inasomeka 150,160, 200 na kuendelea.
Hivyo System inakuwa tofauti na namba ya uliyempigia kura. Yani inakuwa tofauti na makaratasi anayojaza mawakala. Karatasi inasema vingine na kwenye computer inasema vingine. Mfano kwenye ubao wa matangazo inaonyesha waliompigia Lowassa ni 50, Magufuli 45. Kwenye system ya Tume itaonyesha Lowassa 50, Magufuli 150. Wakaweka kuwa kila msimamizi wa Tume kwenye kituo cha kupigia kura atakuwa "Administrator"na anao uwezo wa kubadilisha kama kuna makosa kama hayo. Kitu ambacho hakiwezekani na haijawahi kutokea.
Huwezi kuruhusu kila moja kuwa na uwezo wa kuingilia system. Hii system ya Tume haitawezekana kwa sababu nijuavyo nchi yangu hatuna huduma za Internet nchi nzima watarudia kuhesabu kura kama kawaida. Ndio kisa cha kuagiza kuwa watu wasikae umbali wa mita 200. Kwa sababu wataona matokeo na kuwasiliana na wenzao kabla Tume hawajafanya yao.-Ndio maana yameingizwa magari 777 kwa kitu cha siku moja. Wapinzani wamefanya kampeni zao kwa amani bila matusi wala kumwaga damu. Jiulize fujo zitatoka wapi kama sio maCCM na Polisi wao ndio watakaoanzisha.
Kikwete hajiulize tangu alivyoingia madarakani 2005 watu walikaa mita 200 na mwaka 2010 ilikuwa hivyo hivyo. Jiulize iweje leo anaficha nini?? Anaficha siri ya Ritchmond, Escrow, Mikataba na wachina na wale wafanyabiashara wa Kihemen. Sheria inasema kuwa kaa mita 200 kusubiri matokeo. Na ni uamuzi wako kusubiri matokeo au kuondoka. Jiulize kwani wakati wa kuangalia matokeo vituoni utakuja peke yako na hata kama utakuja peke yako si mtakutana na wengine hata zaidi ya 100 wanaotaka pia kujua matokeo/kuona matokeo.-Mtashangilia wapi baada ya matokeo, uchaguzi unafanyika siku moja na watu kupata matokeo baada ya muda wa kumaliza kupiga kura.
NINACHOWASHAURI WAPINZANI MSIKUBALI MATOKEO, KATAENI ILI KURA IRUDIWE KUHESABIWA UPYA KUTOKA KWENYE KARATASI HALISI ZA VITUO ILIPOPIGIWA KURA.
Uchaguzi huu utakuwa siyo huru na haki na wengi watakufa yani watauwawa na Polisi CCM kwa kulinda utawala wao. Wananchi hawatakubali haki yao kuporwa.
MUNGU IBARIKI TANZANIA