Vizuri ndg, yafaa pia umshauri Mkulu aheshimu na kufuata katiba. Vyama kuendesha siasa halitakiwi kuwa jambo la hisani au kuonewa huruma. Wakubali kukosolewa kwani nchi ni yetu wote watz. Pale ambapo wengine hawaridhiki na baadhi ya maamuzi, kufungua mjadala ndio busara, na sio kulazimisha cha Mkubwa. Polisi wana kazi kubwa sana ya kulinda usalama wa raia, sasa hivi wanatumika zaidi kulazimisha matakwa ya kisiasa. Sasa nao wameanza kuweka na kutekeleza maamuzi yao kwenye siasa.
Maendeleo sio wananchi kuwa wa NDIOO, bali ni kukua kwa uwezo kwa mwananchi kupata mahitaji yake. Kwa mipango mizuri (na sio kukurupuka na mapya kila siku) INAWEZEKANA bila ya kukaba wananchi wengine.