Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,684
- 2,157
Sio serikali wala UKAWA mtakaoibuka kededea kwenye hii minyukano ya kisiasa ya kila siku.
Kila mara viongozi waandamizi wa serikali wanaposimama huja na kauli tata juu ya upinzani na kwa watanzania kwa ujumla kana kwamba uwepo wa upinzani ndio sababu ya umaskini na matatizo yasiyoisha ya watanzania.
Katika kujibu hoja, wapinzani nao wakiibuka wanakuja kifua mbele kupinga na kueleza msimamo wao wa kupinga kauli tata za serikali.
Katika hali ya kusikitisha misimamo ya wapinzani na kauli hizo tata za serikali za mara kwa mara vyote kwa pamoja havina tija ya moja kwa moja kwa watanzania zaidi ni kama vinachochoe hali mbaya kwa watanzania.
Nionavyo mimi serikali Katika wiki kadhaa za mwanzo wa uhai na upya wake ni kama walikuwa wanakuja vizuri. Nasema hivi kwa sababu serikali ilianza kushughulika na matatizo ya watanzania kwa vitendo moja kwa moja. Lakini kadiri siku zinavyoenda naona kama wamehama nakuelekeza nguvu zao kushughulika na wanasiasa wa upinzani.
Mara kwa mara serikali imekuwa ikisisitiza nidhamu na nidhamu yenyewe wanayoitaka kwa mtazamo wangu ni ile ya "akikohoa hata kwa bahati mbaya itika Naaamu". Na hao wanaoambiwa waitike hawako tayari na hawatakaa wakubali kuitika eti kisa yeye ni mkubwa kwani hata wakiitika au wasipoitika hakuna baya watakalokuwa wametenda.
Kwanini serikali isiindelee kama ilivyokuwa imeanza!? Kwani muhimbili tayari vitanda vimetosha!? Bandarini je, makontena yanalipa ushuru na hayatoroshwi!? Wanafunzi je, wote wameshapata madawati, vitabu, maabara, chemicals na walimu wakutosha!? Hivi, hizi zahanati na vituo vya Afya, hospitali na maduka ya dawa ya msd vina dawa na vifaa tiba vya kutosha!?
Kipi kitawamaliza wapinzani, ni kukimbizana nao kila siku barabarani, kwenye mikutano na mahakamani au kutatua matatizo ya moja kwa moja ya watanzania!?
Hivi haya matatizo ya elimu, Afya, miundombinu, na stahiki za wafanyakazi vikishughulikiwa ipasavyo na serikali, hawa wanaoitisha maandamano wataitisha kwa sababu gani!? Na hata wakiitisha nani ataenda wakati anaona matatizo yake yanafanyiwa kazi!?
Huku kutunishiana misuli kukiendelea hivi, si serikali wala upinzani watakaoibuka na ushindi zaidi zaidi ni watanzania wote tutakaoendelea kuumia!
Wekeend njema!