Jamal Akbar
JF-Expert Member
- Oct 9, 2014
- 413
- 473
Wengi wa wanaosapoti UKAWA wana hoja kwamba MAGUFULI hafai kuwa Raisi kwasababu eti yu katika MFUMO (SYSTEM) ambayo ndio tatizo. Watu hawa wamefika mbele zaidi na kutoa mifano ya Nahodha mzuri (MAGUFULI) ambaye wanadai hawezi kuivusha meli mbovu iliyotoboka kutokana na dhoruba. Nitajadili hoja hii kwa kujikita zaidi katika mfano huu huu wa MELI na NAHODHA (Meli na Nahodha zikisimama "symbolize" kwa nafasi ya Nchi na Raisi)
Kwa kawaida kabla ya NAHODHA kuanza safari HUKAGUA MELI yake kuhakikisha iko salama ikiwa ni moja kati ya jitihada za kuhakikisha anamaliza safari salama. Ukaguzi huu hauishii tu kwa NAHODHA kukagua MELI, Uimara na utayari wa Nahodha kukisimamia chombo pia ni suala la msingi na muhimu (ikumbukwe ukaguzi haufanywi kwa kukurupuka tu SAFARI ikikaribia kwani unaweza kufika katikati ya SAFARI na kugundua hukuandaa kila kitu hivyo kuangamiza KILA KILICHOMO KWENYE MELI kwa kifupi ni kwamba Maandalizi Kurupushi ya maigizo ni HATARI sana kwa SAFARI hii).
Ni dhahiri kuwa MAGUFULI alifanya UKAGUZI SAHIHI WA MELI HII kabla ya kuanza kwa safari na amelidhihirisha hilo katika Wizara zote alizoziongoza na ndio maana hahitaji kuingia kwenye masoko na na barabarani leo hii kutafuta matatizo kwani ni wazi ukikurupuka unaweza pata SPARE ZA KICHINA zisizoweza kustahimili MAWIMBI NA DHORUBA YA SAFARI HASA PALE UNAPOKUWA NA NAHODHA ASIYE NA UTAYARI WA KIUTENDAJI NA KIAFYA. Umuhimu wa NAHODHA imara upo waziwazi kwani hata tukirudi kwenye Maandiko matakatifu wakati Bwana Yesu alipokuwa akisafiri na wanafunzi wake aliamshwa kutoka usingizini ili kutuliza Dhoruba (naomba nieleweke simfananishi kwa namna yeyote ile Mgombea yeyote Yule na Bwana Yesu BALI naonyesha umuhimu wa Nahodha hodari katika safari)
Ieleweke kwamba kama MELI ina matobo hata kutia Nanga haitoweza kwani ITAZAMA. Kichekesho kinakuja unapowauliza UKAWA ni jinsi gani Watatuvusha katika Dhoruba hii wengi hujibu "haijalishi nahodha gani anaingia kuongoza alimradi wasafirishaji hawa wametoka kwanza", haya ni majibu yanayostahili kuitwa ya KILOFA. Hatuwezi kufanya gambling katika uongozi wa Nchi la sivyo yatatukumba kama yaliyoikumba Titanic. Hatutaki kupata NAHODHA yeyote tu aingie KUONGOZA MELI hii, Tunataka aliyejipanga kuongoza nchi apate nafasi hiyo. Hatutaki NAHODHA aliyehamia kampuni nyingine kutafuta nafasi ileile aliyonyimwa katika kampuni ya awali baada ya kunyimwa kazi kisa alizamisha Boti na Mitumbwi hapo kabla kisha leo hii tumpe unahodha wa MELI KUBWA.
Ikumbukwe pia Mfumo unaundwa na Wanasiasa (Politicians) + Watendaji (Bureaucrats). Politicians hupatikana kwa kura lakini Bureaucrats hupatikana kwa Merits. Bureaucrats wanatakiwa kuwa non-political lakini kwa mfumo wa Nchi yetu ulivyo sasa wako subordinate to Politicians ambapo WAZIRI MKUU ndiye MKUU WAO. CHADEMA wanasema wanataka kupambana na MFUMO lakini wameshindwa kuuvunja MFUMO MBOVU WALIO NAO HIVI SASA. Nikirejea moja kati ya thread zilizowekwa humu ndani kuelezea mfumo wa CHADEMA unaohoji Jinsi CHADEMA wanavyopeana uongozi na kuachiana vyeo ni dhahiri mfumo wao ni mbovu zaidi. Nanukuu "Aliyeanzisha chama ni Edwin Mtei na ndiyo mwasisi wa Chadema na ndio Mwenyekiti wa kwanza wa Chama hicho, Mwenyekiti aliyefuata ni marehemu Bob Makani ambae alimuoa dada wa Mtei, na Mwenyekiti wa sasa Kamuoa mtoto wa Mtei ambae ni mwasisi na mwenyekiti wa kwanza wa chadema". Hapo Bado hawajashika MELI wana mfumo mbovu hivi, vipi wakipata UNAHODHA.
Kiulinganishi Mmoja wa waomba nafasi ya UNAHODHA aliwahi kuwa mkuu wa MFUMO na MATOBO ALIYOYALETA kwa nchi hii yanafahamika. UKAWA WALILIONA HILI KUANZIA MUDA MREFU NA WALIMSHAMBULIA HADI AKAACHIA NGAZI, LEO HII WAMEMPA UONGOZI WAKITAKA AONGOZE JITIHADA ZAO ZA KUPEWA TENDA AMBAPO NAHODHA WAO ATAKUWA YULEYULE WALIYEMPINGA SIKU ZOTE. (This is Non-sense na ni hapa ndipo tunatakiwa Tunapoanza kuhoji na kupata mashaka kwamba huyu NAHODHA anayetafuta nafasi kwa nguvu zote hataleta mtandao wake kama ambavyo amekwishaanza kwa kumvuta SUMA-YEYE?
Watanzania hatuko tayari kumkabidhi fisi bucha, hatuwezi kutoa tenda ya UNAHODHA wa meli kwa NAHODHA MCHOVU, anayepita mitaani kujua matatizo wakati safari imekwishawadia, hatuko tayari kuzama. Ninaamini TINGATINGA la kazi lipo Kura Yangu nitampa NAHODHA SAHIHI MTENDAJI WA KUAMINIKA Dr. JOHN POMBE MAGUFULI "Every era has its chair, THIS IS MAGUFULI's ERA #HapaKaziTu