UKAWA:Umeya Dar,ni jaribio muhimu kwenu.

magode

JF-Expert Member
Oct 2, 2014
2,204
3,337
Wanabodi,
Amani iwe nanyi.

Km tujuavyo sote,kwa mara ya kwanza ktk historia ya nchi yetu,jiji la dar litaongozwa na ukawa kwa miaka 5 ijayo. Nataka kuwakumbusha tu umuhimu wa dhamana hii mliyopewa na wananchi wa jiji hili.

Wananchi hasa sisi tunaotaka yale mabadiliko ya kweli,ukiacha haya yanayohubiriwa na watu wale wale. Tungependa kuona uongozi tofauti kabisa na uliopita. Tunataka jiji litoe mwelekeo wa upinzani nchini kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2020.

Mkiboronga hapa,hakutakuwa tena na matarajio ya kuchukua dola kwa miaka hii ya karibuni. Piganeni kuhakikisha jiji linakuwa la mfano kwa kila kitu.

Kuna mambo mawili tu yatatokea baada ya miaka 5. Ukawa kuchukua nchi au kurudi kwenye mfumo wa chama kimoja. Sitegemei chama kingine kuaminika km ukawa itapotezwa.

Nawasilisha.
 
Ukawa sio chama na miaka mitano ni mingi sana kwa adui kupanga hujuma, ni vyema vyama vingegawana majukumu mapema.
Viungane tu pale wanapohitajika kufanya maamuzi ya pamoja.
 
Ukawa sio chama na miaka mitano ni mingi sana kwa adui kupanga hujuma, ni vyema vyama vingegawana majukumu mapema.
Viungane tu pale wanapohitajika kufanya maamuzi ya pamoja.
Kuanza kujibagua ni mwanzo wa kufarakana. Wakibaki wamoja ktk mazingira ya muungano wao,ni mafanikio. Hapa tunataka waonyeshe tofauti kati yao na ccm. Hii ni fursa muhimu mno!!
 
tuache kujisifia ushindi na kuelezea sifa za chama tunataka kuona kazi siyo marumbano tena tumewapa halmashauri hizo zote ole wenu tusikie migogoro na marumbano tena
 
Kuanza kujibagua ni mwanzo wa kufarakana. Wakibaki wamoja ktk mazingira ya muungano wao,ni mafanikio. Hapa tunataka waonyeshe tofauti kati yao na ccm. Hii ni fursa muhimu mno!!
Kinachotakiwa ni ufanisi katika utendaji, kwa bahati mbaya kisheria kuna mambo hayawezi kufanyika pamoja.
Kila chama kina katiba yake na matakwa ya hizo katiba ndio yataleta utata baadae, mfano uchaguzi wa viongozi wa chama.
Nafikiri unakumbuka sakata la ZZK kabla ya uchaguzi CHADEMA, sasa kutakuwa na vyama vitatu ambavyo kimojawapo kikipata kiongozi mwenye maono tofauti itakua shida.
 
Sina shaka sana na mameya ila mabaraza ndio ya kumulikwa vizuri na viongozi waandamizi wa UKAWA.
 
Back
Top Bottom