Umejaribu kuja na propaganda ambayo haina msaada mkubwa sana kwa sasa kwa chama chako. Ukijaribu kuangalia kwenye vyama vyote kuanzia ccm, nccr, cuf nk vyote kwa pamoja vimezidiwa na cdm kwa kufanya kazi ya kisiasa kwa kutembelea wapiga kura wengi. Kwa hiyo cdm inavuna matunda ya kazi yake ya kisiasa kwa kuwapa elimu ya uraia wapiga kura wengi kuliko chama chochote. Kwa kukusaidia ili jitihada zako ziwe ni za kukisaidia zaidi chama chako ulipaswa useme hivi, nguvu kubwa iliyofanywa na cdm kuwafikia wapiga kura hatimaye imezaa matunda, vyama vingine vinangoja nini kufanya kama cdm?