Jamani habari za weekend...............
Mimi siipendi ccm kuliko mugabe asivyopenda nchi za magharibi...........
Lakini tasaidiane kujibu hoja hizi nilizokumbana nazo,
kwamba vyama vinavyounda ukawa vinapata ruzuku kubwa kwa pamoja si chini ya 1bil kila mwezi, lakini sasa matumizi yake vipi? Yanaendana kweli na watu wenye dhamira ya kweli ya kuchukua madaraka?
-- mfano cdm wamepanga karibu ofisi zote kuanzia shina hadi taifa, kwa nini hawajengi ofisi za chama?
-- vyama hivi vinapiga kelele kuhusu elimu mbovu inayotolewa kwa sasa, kama wana dhamira ya kweli kuhusu elimu kwa nini hawajengi walau shule chache na waziendeshe kwa ufanisi kudhihirisha wanachopigania?
-- barabara bora zimeongezeka lakini bado hazitoshi, kwa nini wasingetumia sehemu ya ruzuku kujenga barabara mfano kule kwa kange bunda-kisorya hadi nansio ukerewe, kule kwa mama makinda na filikunjombe njombe-makete, kule kwa nchimbi na mama jenista songea-boda ya msumbiji na tz?
Nisaidieni kujibu
Sijaelewa, ni chama gani kinajenga barabara, na tsh billion moja inajenga barabara gani ya maana? Lorry moja la kifusi tani 15 siyo chini ya laki2.5 had tatu na ukikisambaza hata mita20 kwa unene wa sentimita15 haimalizi. Hicho ni kifusi, bado base course ambayo lorry moja ni lak9 kule Lugoba, uje lami na mitaro!
Nijuavyo mimi mkusanya kodi ataitumia kodi kutoa huduma. Siyo CCM au Upinzani watapaswa kutumia ruzuku kuboresha miundombinu bali ni uendeshaji, ni kama overhead cost tu! Naweza kukubaliana na mtoa uzi kwa nini vyama havina ofisiza maana. Walitenga million500 (nusu billion) wanapata jengo zuri tu iwe kama ofs kuu yao