Gangongine
JF-Expert Member
- Dec 31, 2015
- 3,854
- 1,776
Nakumbuka vema kilichotuunganisha mpaka tuigize kususia Bunge la Katiba ni kuwatetea Wananchi ili Maoni yao yazingatiwe kwenye Katiba Inayopendekezwa. Aidha, wakati wa Uchaguzi tuliwadanganya tena Wananchi kwamba wakituchagua tutapigania Katiba ya Wananchi na kweli tukapata Kura milioni 6. Hata hivyo baada ya Uchaguzi tumesahau kabisa Ajenda hii na wala hatuizungumzii tena kwa kisingizio cha kushindwa Uchaguzi Mkuu 2015. Tumesahau tulianza Ajenda hii kabla ya Uchaguzi Mkuu na tulipaswa kuipigania hata baada ya kushindwa Uchaguzi. Wananchi wenye akili wamatuelewa vizuri kwamba kumbe Ajenda ya Katiba Mpya ilikuwa ujanja wetu wa kushinda Uchaguzi na hatukuwa tunamaanisha toka mioyoni mwetu!!
Ajabu Mgombea wetu alisema kipaumbele kwenye Ilani ya Ukawa ni ELIMU, ELIMU, ELIMU (ELIMUx3) lakini sidhani kama Ilani yetu ilitamka hivyo???? Hapo ndipo usanii wetu ulipobainika mbele ya wenye akili tukapoteza Uchaguzi Mkuu. Kama kweli tuna nia hiyo basi tuoneshe sasa vinginevyo tumewasaliti wananchi na hatuwezi kuaminika tena! MABADILIKOOOOOOOO!