nimekaa na kutafakari sana eti mnaitaka Nchi...tena mmeenda mbali kwenda kuomba support kwenye mataifa makubwa.........In return mnataka kuwapa nini........Mkishapata hii nchi Muanze kugawana kila mtu afidie kile alichopoteza katika harakati za kuichukua Tanzania tulivu....
Mnataka kutuletea ya Libya...Mje mtufanye tuishi kwa Mashaka....Upo ushahidi wa Makubaliano Mliyoweka na Mataifa yanayotolea macho Rasilimali za Watanzania...To hell I was In support of u but after noticing this nikawafikiria ndugu zangu kue kijijini wanaotegemea Rasilimali za TZ kwenye maisha yao ya kila siku I SAID NO THANK YOU UKAWA.....
sikuelewa mantiki yenu ya kutka Serikali 3....kumbe ilikuwa ni kuuondoa umoja wa WATZ ili mfanikishe hili...kwa Urahissi.
Soon nitaapload Mzigo hapa tuone Mkakati wenu wakuiuza hii nchi.
Nachelea kusema, "hakuna umaskini mkubwa kwa binadamu kama umasikini wa fikra." Hivi ni taifa gani hapa duniani linaloishi lenyewe bila mahusiano na mataifa mengine. Je ni chama gani cha kisiasa hapa duniani kisichokuwa na mahusiano na chama kingine ndani na nje ya nchi?
Jamani zama za kuwadanganya watanzania zishapitwa na wakati. Ujinga ni mtaji mkubwa sana kwenu CCM. Hilo kwa sasa lina nafasi ndogo sana katika uwanja wa siasa.
Je, unataka nchi hii iuzwe mara ya pili? Madini yetu leo yanamfaidisha nani? Mazao ya misitu na wanyama pori wanamfaidisha nani? Hili nalo kwa leo linaitaji darubini ya ajabu kulijua?
Je, wezi na wahujumu uchumi wapo kwenye vyama vya upinzani au chama tawala? Hujui hata muundo wa serikali unayoitete!
Katiba pendekezwa ambayo ndiyo dira na mwongozo kati watawala na watawaliwa mmeifinyanga kwa manufaa ya nani? Kiongozi gani asiyewajibishwa atakapo hujumu nchi yake? Huo nao wauona uongozi bora?
Haya yote kwa kiasi kikubwa kwa watanzania tunayajua na tunayaona. Ukimya wetu si ujinga. Utulivu wetu siyo hashirio la usalama na kwamba yote ni AMANI tu. Ukimya huu unajambo zito.
Hakuna binadamu yeyote aliyetokea katika sayari hii aliyevumilia yote kwa nyakati zote. Maji yenye utulivu yana kina kirefu. Litakapo tokea jambo lolote kama ishara ya kuchoka udhalimu huu, mzimo wake utakuwa mzito.
Ukiona Baba wa familia anafurahia kula na kujisaidia kwa jirani yake ujue huyo Mzazi haitakii mema familia yake. Ukiona mzee wa familia anajisifia kitambi alicho nacho kwa sababu eti anakula kwa jirani, ujue kifuatacho katika familia yake ni janga zito. Je, na hili linaitaji ufahamu wa pekee kujua tunapowatazama watawala wetu leo Tanzania?
Mwisho nikupe ushauri: Tanzania ya leo imebadilika sana. Jenga hoja kabla na kusema chochote. Bla bla za kimfumo na kiitikadi kichama hazina mashiko leo. Hadithi za kufikirika za "tuta..." zishazoelema. "You can't teach an old dog new tricks." Chama tawala mmechoka na kuchokwa. Hakuna jipya tena.