UKAWA ni wazembe wa kutupwa

UKAWA ni wazembe wa kutupwa

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,169
Reaction score
48,451
Hapa siwazungumzia wana UKAWA ambao ni watu wa kawaida mitaani wasio na nyadhifa kwenye vyama vinavyounda UKAWA. Hapa nawalenga viongozi wa vyama hivyo kuanzia wenyeviti wao hadi maofisa wa Makao Makuu kwenye vyama hivyo.

Kuna suala linaendelea la kuwa na Rais bila ya kuwa na Baraza la Mawaziri, hivi msimamo wa UKAWA ni nini hasa. Wao wanaona kuwa ni sawa au si sawa? Kwa maana nyingine kama wao ndiyo wangekuwa wamepewa serikali mpaka leo wangekuwa pia hawajatangaza baraza lao la mawaziri?

Hili jambo la Bandari UKAWA wana taarifa gani kuhusu sakata zima? Kwa maana watu wafahamu kuwa Bandari ya Dar es salaam ina uwezo wa kutunza kwa wakati mmoja Makontena zaid ya milioni 4. kwa maana nyingine hayo zaidi ya 2000 yanayotajwa na Waziri Mkuu Majaliwa ni tone tu katika makontena yanayopitia Dar es salaam. Maana yangu ni kwamba inawezekana kuna watu wameachwa kutokana na maslahi ya kisiasa waliyonayo Waziri Mkuu na wenzake ndani ya CCM.

Ada elekezi kwa shule binafsi UKAWA wao msimamo wao ni upi? Maana wenye shule zao wameahidi kutozifungua msimu wa kufungua ukifika. Je UKAWA wanandhani hatua za Serikali ni sahihi au si sahihi na wao msimamo wao ni upi? Wanaona hiyo njia wanayotumia Serikali ndiyo itakuwa inajenga uwezo wa shule za Umma na kuboresha elimu au ndiyo Elimu inashushwa kiwango chake?

Halafu kuna hili la CCM kufanyia vikao vyake kwenye ofisi kuu ya Umma Tanzania, Ikulu. Kama sheria inazuia siasa kwenye majengo ya umma kama mashule na kadhalika inakuwaje chama cha siasa kitumie Ikulu ambayo ni ofisi kuu ya Umma kufanyia vikao vyake? Je UKAWA na wao wangeshika madaraka wangetumia Ikulu kufanyia vikao vyao vya kisiasa.

UKAWA ni wazembe sana, kila inapotokea nafasi ya kujijenga kisiasa wao huwa wako Bize na harakati zisizo na mashiko!
 
Mkuu hili unalijua leo? unatakiwa ukapimwe akili kama alivyowahi kushauri mchungaji Msigwa! UKAWA hawajali maslahi mapana ya wananchi....LENGO la UKAWA ni Kutwaa MADARAKA hata kama Kiongozi wao ni JIWE ....
 
Hapa siwazungumzia wana UKAWA ambao ni watu wa kawaida mitaani wasio na nyadhifa kwenye vyama vinavyounda UKAWA. Hapa nawalenga viongozi wa vyama hivyo kuanzia wenyeviti wao hadi maofisa wa Makao Makuu kwenye vyama hivyo.

Kuna suala linaendelea la kuwa na Rais bila ya kuwa na Baraza la Mawaziri, hivi msimamo wa UKAWA ni nini hasa. Wao wanaona kuwa ni sawa au si sawa? Kwa maana nyingine kama wao ndiyo wangekuwa wamepewa serikali mpaka leo wangekuwa pia hawajatangaza baraza lao la mawaziri?

Hili jambo la Bandari UKAWA wana taarifa gani kuhusu sakata zima? Kwa maana watu wafahamu kuwa Bandari ya Dar es salaam ina uwezo wa kutunza kwa wakati mmoja Makontena zaid ya milioni 4. kwa maana nyingine hayo zaidi ya 2000 yanayotajwa na Waziri Mkuu Majaliwa ni tone tu katika makontena yanayopitia Dar es salaam. Maana yangu ni kwamba inawezekana kuna watu wameachwa kutokana na maslahi ya kisiasa waliyonayo Waziri Mkuu na wenzake ndani ya CCM.

Ada elekezi kwa shule binafsi UKAWA wao msimamo wao ni upi? Maana wenye shule zao wameahidi kutozifungua msimu wa kufungua ukifika. Je UKAWA wanandhani hatua za Serikali ni sahihi au si sahihi na wao msimamo wao ni upi? Wanaona hiyo njia wanayotumia Serikali ndiyo itakuwa inajenga uwezo wa shule za Umma na kuboresha elimu au ndiyo Elimu inashushwa kiwango chake?

Halafu kuna hili la CCM kufanyia vikao vyake kwenye ofisi kuu ya Umma Tanzania, Ikulu. Kama sheria inazuia siasa kwenye majengo ya umma kama mashule na kadhalika inakuwaje chama cha siasa kitumie Ikulu ambayo ni ofisi kuu ya Umma kufanyia vikao vyake? Je UKAWA na wao wangeshika madaraka wangetumia Ikulu kufanyia vikao vyao vya kisiasa.

UKAWA ni wazembe sana, kila inapotokea nafasi ya kujijenga kisiasa wao huwa wako Bize na harakati zisizo na mashiko!

Sijui umekula maharage ya wapi wewe! Ovyo kabisa. Kwani ofisi zao hao ukiwa huzioni? peleka ulofa wako huko.
 
Ungehitimisha basi na wewe kwa kutoa maelekezo ni nini kingefanyika badala ya kulaumu.
 
UKAWA ilishakufa tangu 25 octoba walivyoshindwa kwa aibu.

haipo tena.
 
kwani ukawa bado wapo? lengo la ukawa ilikuwa kushika dola, wameangukia pua. hivi sasa kila chama na hamsini zake mpaka bunge litakapokutana. hayo maswali uliza chama binafsi na si ukawa.
 
Mtoa mada umenena hata mimi nashangaa,iweje viongozi wakuu hasa mwenyekiti Mbowe hatoa matamko kwa haya yanayoendelea nchini?Ukawa wamemwacha Magufuli anatamba kwenye vyombo vyote vya habari.Huu ni udhaifu.
 
Nalaani vikali magufuli kugeuza ikulu ni kijiwe cha kupigia majungu. Nyerere mwenyewe hajawahi fanya upuuzi kama huo. Hivi magufuli ni nani hasa, hadi afanye ikulu pango la kukutania wanyang'anyi?
 
Kama hujui haya yote mazuri yanayofanywa na Magufuli yanatokana na kazi nzuri ya UKAWA,dosari zinazojitokeza UKAWA wanaziona,kwa kuwa si wa kukurupuka watatoa jibu sahihi nini ambacho Magufuli ana takiwa akifanye ili mambo yaendelee kwenda vizuri.
 
ukawa sio wa kuwabeza kaka naamini kbs kuna kitu wanacho na muda ukifika wataongea mengi ambayo kimsingi wenye jicho la tatu tutawaelewa tu
 
Nalaani vikali magufuli kugeuza ikulu ni kijiwe cha kupigia majungu. Nyerere mwenyewe hajawahi fanya upuuzi kama huo. Hivi magufuli ni nani hasa, hadi afanye ikulu pango la kukutania wanyang'anyi?

Well said.
 
Mtoa mada umenena hata mimi nashangaa,iweje viongozi wakuu hasa mwenyekiti Mbowe hatoa matamko kwa haya yanayoendelea nchini?Ukawa wamemwacha Magufuli anatamba kwenye vyombo vyote vya habari.Huu ni udhaifu.

magu anatumia ilan ya chadema wameshasema
 
Mbona hujiulizi kwanini atangazi Baraza la Mawaziri mpaka sasa?

Siasa mchezo wa kuviziana... Tulia usikie wanakuja na lipi.

Akili za kubemendwa sio wakati wake huu
 
ndemesi hoja yangu hapa ni kwamba jee muda unawasubiri wao tu UKAWA. Mwalimu aliwahi kusema "Linalowezekana leo lisingoje kesho" na pia alisisitiza "it ca be done, play your part" yaani "Inawezekana timiza wajibu wako"
 
Last edited by a moderator:
Mtoa mada umenena hata mimi nashangaa,iweje viongozi wakuu hasa mwenyekiti Mbowe hatoa matamko kwa haya yanayoendelea nchini?Ukawa wamemwacha Magufuli anatamba kwenye vyombo vyote vya habari.Huu ni udhaifu.

Sio kila muda unatakiwa kuongea utachosha watu,wakati wa Msiba wa Mawzo ulikuwa hauwaoni kwenye media,wakati kiongozi wao kauwawa kiongozi gani wa ccm katoa pole,waache ccm wagombane wenyewe wewe unataka waongee nini
 
Ndugu yangu uongo na porojo ni kazi kubwa sana, hivyo wavumilieni tu viongozi wenu katika kipindi hichi kigumu wamejifungia kutunga hadithi, porojo na uongo mpya wakuja nao mtaani kwa sasa hawana la kusema
 
Back
Top Bottom