UKAWA na CCM pamoja

king ndeshi

Senior Member
Oct 31, 2010
135
7
Ndugu watanzania,

amani iwe kwenu,awali ya yote napenda kuwashukuru kwa uvumilivu wenu kwa kipindi chote hichi cha uchaguzi,sababu kuvumilia kwenu ndo msingi wa amani hii inayotamalaki sasa. Kuna msemo unasemaga "amani haiji kwa ncha ya upanga''

ndugu zangu tumeshampata kiongozi wetu wa nchi hata kama sio yule tulie mchagua, bado tunaowajibu wa kumpa ushirikiano ili kwa pamoja tujenge taifa letu. Ni kweli yapo mapungufu kadha wa kadha lakini hayabadilishi hali ya kisiasa tuliyo nayo sasa,mpaka yatakaporekebishwa ndipo tutabadilisha mazingira ya kisiasa.

Kila mtu wa upande wa pili pengine anamengi yakusema kuhusiana na uchaguzi,hata mimi kama kijana niliechagua mabadiliko ninayo mengi nina na uchungu pia na kwakweli nimesha lalamika sana,lakini nitakuwa kama mtu ayetaka kwenda lindi kutoka dar kwa mguu wakati kuna magari kama nitatumia kila fursa inayotokea kulalamika.

Ndugu wananchi sio kwasababu hajashinda tuliemtaka basi hatutapiga hatua hata kidogo,siamini hivyo. Inawezekana tusipate elimu bure mpaka chuo kikuu lakini tukapata elimu bure mpaka form four!

Inawezekana tusipate katiba mpya lakini katiba iliyopo ikarekebishwa tukapata tume huru ya uchaguzi
inawezekana january makamba asichaguliwe naibu waziri wa mawasiliano, lakini tukapata waziri atakae pigana mpaka vifurushi vya data na internet vikapungua bei.

Sio hayo tu,sidhani kama raisi pombe akijenga daraja litakuwa la wanachama wa ccm peke yao, kimsingi tutapita wote.

Sidhani kama raisi pombe akijenga hospitali, watatibiwa watu wa ccm peke yao,tutatibiwa wote.
Na nazani kama ikitokea tumeisoma namba, hatutaisoma wanaukawa peke yetu,tutaisoma wote,tena tutaisomea kwa mbali.

Nnachotaka kusema tusimpe raisi stress hata akashindwa kufanya aliyopanga kuyafanya...SABABU Kosa la kumsonga sana kwa maneno na vijembe vya hapa na pale ndo mwanzo wa sisi kuisoma namba.
Tumuombee kiongozi wetu,tumpe moyo na tushirikiane kujenga nchi wote ukawa na ccm,kama tunavyoshirikiana kuisoma namba.

By the way nimefurahi kumuona dada lucy magereli,amabye kura zake hazikotosha jimbo la kigamboni ambamo ninariside. kwenye list ya wabunge watakao kwenda bungeni kwa tiketi ya chadema bendera ya ukawa viti maalumu.

Mungu ibariki tanzania,mungu mbariki raisi magufuli.

wote tuseme amina..
 
Kuna wengine wanasema rais wao siyo aliyopo bali ni fulani, sasa sijui huyo fulani anaye muamini anaongoza wapi.
 
Nenda kawaambie wanawake huo upuuzi ameokwambia wapinzani wanaleta vita kawaambieni wazee
 
To me it will take along time to accept magu as a president. Nafikiri anaweza kukurupuka kutoa amri kama alivyowahi amrisha watu wa Kigambonono kuogelea.
 
Magu-fool amepachikwa na mafia Wa jeshi na polisisyemu, fulustopu. H?ta yeye analijua hilo, huyu kiumbe si kiongozi hebu ona mambo ya aibu anayofanya, nilidhani baada ha mapushapu atajorudi kumbe kichwani hamna kitu. Anaiaibisha institution ha presidency. Hivi rais Wa kweli anaweza kutoka ofisini kwake na kwenda kuvizia watoro wizarani? Hiyo ni kazi ha ufanywa na rais? Toka lini rais akawa kiranja? Oke, naye badala ha kuwa ofisini kufanya kazi zake alienda kuranda, eti kuvizia watoro, sa sa naye si alitoroka ofisi yake?

Hivi nani alimwambia kuwa kuwepo kazini masaa yote ndio kufanya kazi? Huu ni mzigo tu pu, uraisi Wa kisingiziwa tu ili kiwete na kipipa lodo lofa waendelee kupeta.
 
ukawa wajipange kuzisimamia halmashauri na manispaa wanazoziongoza ili zionyeshe utofauti na zile zinazoongozwa na chama tawala. pia waanze mkakati wa kupenya vijijini...
 
Back
Top Bottom