Goodluck Mshana
JF-Expert Member
- Aug 7, 2011
- 1,272
- 1,128
Yatosha kusema ni wakati sasa wa UKAWA kufanya maamuzi sahihi kwa mtu sahihi ndani ya muda sahihi. Mtakubaliana na mimi kwamba mgombea wa CCM, Dr. Magufuli atatoa upinzani mkali ambao haukufikiriwa wala kuwazwa. Wengi tulidhani kikombe cha utukufu kingemdondokea kati ya Jaji Ramadhani, Membe au Lowassa.
Mambo hayakuwa kama yalivyokuwa. Mapenzi ya mwenyekiti nayo yaliyeyushwa na wazee wa cc. Hivyo kuacha vilio vya kwa 'team' husika. Sasa tunaye Pombe. Siyo mchafu kiasi cha kumtumia kuweza kuipoka nchi toka CCM. Nasema si kazi rahisi na UKAWA wasipo changa vyema karata basi mjipange kuwa wapinzani kwa miaka 10 mingine. Huu ndiyo ukweli. Lazima tubadilike kwenye hili.
Ushauri wangu ni UKAWA kumchagua mtu ambaye ni neutral. Mtu ambaye yeye binafsi anauzika kwa wananchi. Mtu ambaye hatokani na chama chochote ndani ya UKAWA ili kupunguza pressure na ukwasi wa viongozi ambao hadi sasa kuna sintofahamu inayopelekea vikao kuwa vingi!
Napendekeza muanze mazungumzo na Dr. Mengi awe mgombea kwa tiketi ya UKAWA. Au kama Mengi inakuwa tabu fanyeni mazungumzo na Jaji Warioba. Watu hawa watatoa changamoto kubwa kwa Magufuli na kulainisha nyonga na vitasa vya magogoni.
Ninaamini kwa hawa wawili Ikulu itakuwa nyepesi kupaingia. UKAWA fanyeni hivyo kwa maslahi mapana ya Taifa na kuweza kuwapunguzia Watanzania maumivu ya another 10 years. Nakubali pasi na shaka kwamba Magufuli anayo record nzuri ya utaendaji kazi. Kitu ambacho kinawasukuma Watanzania wengi kuamini atawatendea haki na kuamsha matumaini mapya. Lakini watanzania hawa wan adabu ya kwamba John yupo kwenye mfumo corrupt, mfumo wa dhuluma, mfumo wa wavivu kufikri na kiutendaji, mfumo kujuana (nepotism), mfumo wa walafi wanaokula bila kunawa, nakadhalika nakadhalika. Magufuli hawezi tenda vyema maana mirija ya fahamu na damu imeingiwa na mafuta (cholesterol) hivyo atatenda kama ilivyo kwa anayemuachia nchi.
UKAWA changa karata vyema. Tumejiandikisha vya kutosha kwenye daftari la kudumu na Watanzania wanawangoja muwatendee haki.