UKAWA mnafanya nini Dodoma mpaka dakika hii?

UKAWA mnafanya nini Dodoma mpaka dakika hii?

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
26,021
Reaction score
25,423
Inaonekana wazi kwamba CCM wameliteka bunge la katiba na kuna kila dalili kwamba wanataka kututungia katiba ya CCM. Lengo la tume ya Warioba lilikuwa ni kukusanya maoni ya wananchi na hatimaye kutunga katiba ya wananchi. CCM, kupitia kwa mwenyekiti wa chama chao, wameyakataa maoni yote ya wananchi yaliyomo kwenye rasimu ya katiba.

Kwa kuwa lengo lilikuwa ni kutunga katiba ya wananchi na kwa kuwa sasa lengo hilo limebadilishwa na CCM kwa makusudi, hakuna haja ya wabunge wazalendo wanaotetea katiba ya wananchi (UKAWA) kuendelea kuwepo Dodoma na kukubali kutungishwa katiba ya CCM. Fungasheni virago mrejee nyumbani. Waachieni wabunge wa CCM na vibaraka wao watunge katiba ya CCM na wakiileta kwa wananchi tuikatae sawia.

Nampongeza sana Prof Lipumba kwa kukataa kutumikishwa na CCM kwa manufaa ya chama chao ghairi ya manufaa ya wananchi. Nawaomba wabunge wazalendo muondoke Dodoma mara moja muwaache wabunge wa CCM peke yao waendelee kutunga katiba ya CCM. Msikubali kutumiwa kama mihuri kupitisha katiba ya CCM!!!!!
 
Kesho lazima wafungashe virago maana magamba tayari wamesharejea maagano yao na shetani tangu walipo kataa ubalozi wa israeli
 
Kesho lazima wafungashe virago maana magamba tayari wamesharejea maagano yao na shetani tangu walipo kataa ubalozi wa israeli

mkuu, kwani si walisema leo ndio kinaeleweka, wamesogeza mpaka kesho tena? inaonekama CCM walishasoma alama za nyakati, sasa wanajaribu kurefusha matanga. katiba mpya ya wananchi itatungwa pindi CCM waking'oka madarakani mwaka 2015. hata huko kenya katiba mpya itapatikana baada ya kanu kung'atuliwa mamlakani-
 
Upo sawa mkuu

Natamani niwatumie mabasi makubwa waondoke wote wa pamoja wakiimba nyimbo za kizalendo tuwapokee hapo ubungo kabla ya kutwanyika tupige mkutano wa nguvu jwangwani pale kama kaiwada kupaza sauti za kizalendo juu ya wakoloni ccm kuwa hamna chenye mwanzo kisichokuwa na mwisho
 
Utabwatuka wewe lakini upende usipende ccm lazima iwe na influence kubwa kwenye kuandika katiba kwa kuwa ndicho kilinachoaminiwa na wananchi wengi.
 
hakuna kitu anachoniudhi kikwete kama kuingilia huu mchakato wa katiba. maoni tutoe sisi, uamuzi atoe yeye. sasa siangekaa tu hapo magogoni na wasaidizi wake na kuandika hicho anachokitaka kwenye katiba? kulikuwa na haja gani kutumia mabilioni ya kodi zetu na mpaka sasa bado yanalipwa bunge lililojaa watu wake?
Mudi sio mrefu nitaanza kumuoni MPUUZI!
 
Wapo wanafanya fujo na kukaa kwenye vikao vya usiku kupanga mipango halamu.
 
hakuna kitu anachoniudhi kikwete kama kuingilia huu mchakato wa katiba. maoni tutoa sis, uamuzi atoe yeye. sasa siangekaa tu hapo magogoni na wasaidizi wake na kuandika hicho anachokitaka kwenye katiba? kulikuwa na haja gani kutumia mabilioni ya kodi zetu na mpaka sasa bado yanalipwa bunge lililojaa watu wake?
Mudi sio mrefu nitaanza kumuoni MPUUZI!
Wewe ndiyo kitasa kweli tangu lini bavicha akawa na akili hata ya kwenye kisoda ndiyo maana unaandika pumba tu.
 
Yaani kama mchezo wa lede...marefa wa hili game washaanza ku enjoy Kwa kunywa mivinyo. UKAWA wakiondoka tu, wanafungua champaign na kuhitimisha kalamu Yao ya kuchezesha shele mchaka mchaka wa Katiba ya kufikirika. Ngoma usiyoijua vizuri Ni bora kutoicheza toka mwanzo, Ni lazima utakosea tu step. Katiba mpya itapatikana siku wale jamaa wanao ratibu security ya nchi hii watakapoamua sasa na iwe hivyo. Maana Hata kama tuna malengo ya kupata Rais mpya toka upinzani Ni wao watakaoamua. Nimejifunza sana kutokana na mambo yanavyoenda katika mfumo wa nchi na kugundua hakuna lengo lolote linalofanikiwa kama usalama wa nchi unakuwa hatarini. Tujifunze tu katika tamthilia za ki-Korea kama IRIS.
UKAWA mkiona vema kurudi mpumguze gharama za POSHO nchi inagharamika kuwalipa itakuwa vema kiuchumi, lakini kumbukeni mlishaingia mkenge na kujinasua Ni ngumu sana. Japo, kutoka kwenu itakuwa Ni ujumbe ama uwe hasi ama chanya Kwa wachezeshaji.
 
Wewe ndiyo kitasa kweli tangu lini bavicha akawa na akili hata ya kwenye kisoda ndiyo maana unaandika pumba tu.
nilikwua sijui, kumbe akili za uvccm ni sawa kabisa na akili za bavicha, nyie wote kuanzia leo nawaita misukule msiojitambua. wale wanacontroliwa na remote kutoka kwa hayatula mtei wa tengeru na nyie kutoka kwa sultan Kikwete wa magogoni.

Katiba ni yetu sisi wananchi, mwambieni huyo sultan akae pembeni kabisa, abaki mwananchi na mtoa maoni tu kama mimi kapuku wa kwa abunuas.
 
Utabwatuka wewe lakini upende usipende ccm lazima iwe na influence kubwa kwenye kuandika katiba kwa kuwa ndicho kilinachoaminiwa na wananchi wengi.

Mkuu, hili bange la leo umevuta au umekula? Ina maana kwamba kwa kuwa CCM wana inluence kwa hiyo tutumie katiba yao kuendesha nchi? Ama kweli hizi posho za Lumumba zimekulevya kupindukia!!!
 
Mkuu wapigie simu warudi ili tupumzike nafujo make ni kero kweli wanafujo kama matoto.

Ni kweli kabisa mkuu, ni bora ukawa waondoke ili maCCM yabaki kuendelea na fujo zao za kitoto. MaCCM wanataka kutulazimisha tukaubali katiba yao iendeshe nchi. Hili haliwezakani duniani wala mbinguni.
 
26th March 2014

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta akiwa katika tafakuri nzito wakati mjumbe wa Bunge hilo, Prof. Ibrahim Lipumba alipokuwa akitoa maelezo ya kukataa kuteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Uongozi ya Bunge hilo, mjini Dodoma jana. Picha/Khalfan Said

Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wametishia kujiondoa kwenye Bunge hilo leo, wakilalamikia muundo wa Kamati za Bunge hilo kuwa na wenyeviti wengi wanaotoka CCM na upendeleo wa Mwenyekiti kwa chama hicho.

Mtafaruku huo miongoni mwa wabunge unatokana na uchaguzi pamoja na uteuzi wa wenyeviti wa Kamati 12 za Bunge hilo, uliosababisha manung'uniko kutoka kwa wajumbe baada ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta, kutangaza majina ya washindi wa uchaguzi wa Wenyeviti na Makamu wenyeviti uliofanyika juzi.

Baada ya uchaguzi pamoja na uteuzi wa Mwenyekiti, wajumbe 16 kati ya 19 wanaounda Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalum la Katiba ni wanachama wa CCM, huku watatu waliobaki mmoja akiwakilisha watu wa makundi ya watu wenye mahitaji Maalum na wawili pekee wakiwakilisha vyama vya upinzani.

Sitta alitangaza majina ya wenyeviti wa Kamati za Bunge ambao walichaguliwa kwenye uchaguzi ulofanyika juzi mjini hapa kuwa ni Andrew Chenge, Pandu Ameri Kificho Ummy Mwalimu, Hamad Rashid, Shamsi Vuai Nahodha, Dk. Francis Michael, Christopher Ole Sendeka, Steven Wasira, Brigedia Mstaafu Hassan Ngwilizi, Job Ndugai, Kidawa Hamis Salehe, Anna Abdallah, Anne Kilango Malechela na Paulo Kimiti.

Aidha, ili kukamilisha idadi ya wajumbe 19 wa kamati ya Uongozi ya Bunge, Sitta aliwateua Fakaria Hamis Shomari, Mary Chatanda, Prof. Ibrahim Lipumba, Amon Mpanji na Abuu Juma.

Kati ya wajumbe hao, wanaowakilisha vyama vya upinzani walikuwa ni Hamad Rashid na Prof. Ibrahim Lipumba wote kutoka CUF, licha ya kuwa chama hicho kilishamfukuza uanachama Hamad Rashid.

Baada ya kuahirishwa kwa kikao hicho cha Bunge, Wajumbe wa Ukawa walikutana katika ukumbi wa Pius Msekwa, na kuteua kamati yao ya Uongozi yenye wajumbe 20 kwa ajili ya kujadili suala hilo kwa kina.

Kamati hiyo ilihamia katika moja ya ukumbi ndani ya Jengo la Utawala la Bunge na kufanya kikao kilichochukua takriban saa tano, huku baadhi yao wakiitwa kwenye Kamati ya Kanuni ya Bunge hilo kwa lengo la kutafuta maridhiano juu ya suala hilo.

Wajumbe waliokwenda kwenye Kamati ya Kanuni za Bunge hilo ni James Mbatia na John Mnyika.

Akizungumza na NIPASHE kabla ya kuingia kwenye kikao hicho cha Kamti ya Kanuni, Mbatia alisema kuwa Ukawa inatarajia kutoa uamuzi wa nini kifanyike juu ya suala hilo baada ya kuunganisha mawazo atakayoyapata kwenye Kamati ya Kanuni pamoja na maoni ya kikao cha Ukawa kilichokuwa kikiendelea kwenye Jengo la Utawala.

"Nimewaacha wenzangu wakiendelea na kikao, mimi nakwenda kwenye Kamati ya Kanuni, yale nitakayoyapata huko tutaunganisha na mawazo ya wengu na ndipo tutatoa tamko letu," alisema Mbatia

Hata hivyo taarifa kutoka kwenye chanzo chetu ndani ya kikao cha Kamati ya Ukawa, zilieleza kuwa Kamati hiyo imeamua wajumbe wake kujitoa kushiriki kwenye Bunge Maalum na kuondoka mjini Dodoma endapo hakutafanyika mabadiliko ya kanuni kwa ajili ya kuwezesha wapinzani kupata uwakilishi kwenye Kamati ya Uongozi wa Bunge.

"Subirini kwa sasa siwezi kuzungumza chochote, lakini kaeni tayari kesho (leo) kuna kitu kikubwa kitatokea kwa wajumbe wanaounda Ukawa kufanya maamuzi magumu baada ya kumaliza kikao cha Kamati ya Kanuni kumalizika na kutueleza walichoazimia," kilisema chanzo hicho.

Katibu wa Ukawa, Julius Mtatiro, alipoulizwa kuhusiana na maamuzi ya kikao hicho aliwataka waandishi wa habari kuvuta subira ili viongozi wa Ukawa watoe taarifa kwa wajumbe wake na baadaye kutoa taarifa ya uamuzi wa wajumbe kwa waandishi wa habari.

Kwa upande wake Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Prof. Lipumba aliliambia NIPASHE kuwa baada ya majadiliano ya muda mrefu wamekubaliana kusubiri maamuzi ya Kamati ya Uongozi ya Bunge na ajenda zitakazoletwa leo bungeni ili watoe uamuzi wao.

Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni kikao cha Ukawa na kile cha Kamati ya Kanuni za Bunge vilikuwa vikiendelea kwenye kumbi tofauti bungeni mjini Dodoma.

CHANZO: NIPASHE
 
Yaani kama mchezo wa lede...marefa wa hili game washaanza ku enjoy Kwa kunywa mivinyo. UKAWA wakiondoka tu, wanafungua champaign na kuhitimisha kalamu Yao ya kuchezesha shele mchaka mchaka wa Katiba ya kufikirika. Ngoma usiyoijua vizuri Ni bora kutoicheza toka mwanzo, Ni lazima utakosea tu step. Katiba mpya itapatikana siku wale jamaa wanao ratibu security ya nchi hii watakapoamua sasa na iwe hivyo. Maana Hata kama tuna malengo ya kupata Rais mpya toka upinzani Ni wao watakaoamua. Nimejifunza sana kutokana na mambo yanavyoenda katika mfumo wa nchi na kugundua hakuna lengo lolote linalofanikiwa kama usalama wa nchi unakuwa hatarini. Tujifunze tu katika tamthilia za ki-Korea kama IRIS.
UKAWA mkiona vema kurudi mpumguze gharama za POSHO nchi inagharamika kuwalipa itakuwa vema kiuchumi, lakini kumbukeni mlishaingia mkenge na kujinasua Ni ngumu sana. Japo, kutoka kwenu itakuwa Ni ujumbe ama uwe hasi ama chanya Kwa wachezeshaji.

Kabla jogoo hajawika, ule utabiri wangu wa kuwaasa ukawa waondoke Dodoma umetimia. Hakukuwa na haja ya kuendelea kuwasaliti wananchi kwa kutupilia mbali maoni yao. Waacheni hao wanafiki waliozoea vya kunyonga waendelee kuteketeza fedha za umma bila huruma huku wananchi wakiishi kwa kula majani na kukosa huduma za hospitali, maji, shule, barabara, nk.

Nawapongeza sana UKAWA kwa kujiondoa bungeni na kuwaachia wabunge wa CCM waendelee na utunzi wa katiba ya CCM. Wana-UKAWA mlitumwa kwenda bungeni kusimamia katiba ya wananchi, sio kutumiwa kama mihuri ya kupitisha katiba ya CCM. Ni bora kuwaacha CCM (INTARAHAMWE) wenyewe bungeni wakatunge katiba yao kisha wailete kwa wananchi waipige chini. Hawa wanahizaya wa CCM hawana huruma na mabilioni ya pesa za wananchi zionazoteketea katika utunzi wa katiba. Walaaniwe INTARAHAMWE wote kwa kutaka kuitumbukiza nchi kwenye damu kisa tu waendelee kuning'inia madarakani!
 
Upo sawa mkuu

Natamani niwatumie mabasi makubwa waondoke wote wa pamoja wakiimba nyimbo za kizalendo tuwapokee hapo ubungo kabla ya kutwanyika tupige mkutano wa nguvu jwangwani pale kama kaiwada kupaza sauti za kizalendo juu ya wakoloni ccm kuwa hamna chenye mwanzo kisichokuwa na mwisho

Kinachonisikitisha na kunishangaza zaidi ni pale CCM wanapotaka kuwaaminisha watanzania kwamba uwepo wa serikali 3 (serikali ya Tanganyika, Zanzibar na MUUNGANO) eti ni kuvunja muungano. Muungano utavunjikaje wakati katika hizo serikali 3 imo serikali ya Muungano? Hivi hawa INTAHAHAMWE hawana haya? Mtaji wa hawa watu ni ujinga watanzania. Ndio. Eti watanzania wanaaminishwa uongo huo nao wanaukubali!

Hivi jamani mtu ukiwa na nyumba yako ambayo haikidhi mahitaji, ukiamua kuifanyia renovation au ukaibomoa na kujenga nyumba mpya kubwa, imara na bora zaidi, tatizo liko wapi? Ni nini hofu ya CCM katika uwepo wa serikali 3 hadi waanze kuwatisha raia kwamba ikiwa serikali 3 zitaruhusiwa jeshi litachukua nchi? Kama ndivyo basi, sisi raia tunaoteseka chini ya utawala wa CCM tunakaribisha jeshi lije litawale badala ya kuendelea kuishi ndani ya utumwa wa serikali ya CCM.

Watu hawahawa waliwaaminisha watu kwamba vyama vingi vikiruhusiwa, nchi itaingia vitani kama ilivyowahi kutokea huko Rwanda. Walifikai hatua ya kutembea nchi nzima wakionyesha mikanda ya vita ya Rwanda na intarahamwe ili kuwatisha wananchi kuhusu ujo wa vyama vingi. Hatimaye vyama viliruhusiwa na hatujawahi kuona nchi ikiingia vitani. Ama CCM wamezoea kuishi kwa UWONGO, ukweli hawauwezi!
 
Back
Top Bottom