UKAWA mnafanya kosa la kiprotokali

UKAWA mnafanya kosa la kiprotokali

meningitis

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2010
Posts
8,464
Reaction score
4,828
Najitambulisha kama mkatoliki kindakindaki...na sio mara ya kwanza kufanya hivi.niliwahi kufanya hivi hapo awali na nilimtuhumu Askofu Pengo kwa tamko lake kuhusiana na mashambulizi dhidi ya mapadre wetu.inawezekana kipindi kile sikumuelewa Kadinali Pengo...nilikurupuka kumtuhumu kama alivyokurupuka Gwajima.

Nilimtuhumu kwa kupingana na msimamo wa wengi dhidi ya nani muhusika wa mashambulizi yale.nilimtuhumu kwa kutoelekeza wakatoliki tufanye nini dhidi ya ufirauni waliofanyiwa mapadre na waumini wa Kanisa katoliki,nilikasirika na kumuona ni msaliti na anasimama na serikali inayotuudhi!

Mambo yalivyoendelea nilijikuta naanza kuelewa zaidi kauli za kadinali Pengo na kuziona ni sahihi na zinazingatia ukweli au uchunguzi wa mambo.

Ndio maana kwa kauli hii ya juzi sikutaka kukurupuka.

Nimeanzisha thread zipatazo mbili kuhusu sakata na kauli ya hivi karibuni ya kadinali Pengo lengo ni kujua uhalisia na ukweli wa kile alichokisema Askofu Pengo..zote zimeishia kapuni.

madhumuni ya uzi huu ni kuwatahadharisha Ukawa juu ya kukurupuka!

Nawasihi na kuwatahadharisha Ukawa juu ya kumdharau Pengo kisa porojo na matusi ya Gwajima.

Nawatahadharisha Ukawa kutojifungamanisha na Gwajima mtu ambaye amewakosea adabu wakatoliki ...hakuna mkatoliki anayefurahishwa na matusi dhidi ya Kadinali Pengo na haitatokea kamwe hata kama angeshikwa ugoni!

Ukawa jihadharini sana!hapa ndipo mtakapopoteza!

Nawasilisha kwa uchungu!
 
Hapo upo sawa hata mi mkatoliki sijafurahishwa na kitendo cha pengo kutukanwa n ukawa wajue wakatoliki ni wingi na wanasikiliza viongozi wao wa dini so wakifanya ujinga kwa hilo kweli watapoteza
 
Dr Slaa na Lipumba wameshauriwa vibaya!
Gwajima hakustahili sabahi kutoka kwao.
 
Mnakuza mambo na kumuwekea maneno mdomoni mwa Mtu...
Wote tulimsikia Gwajima, akieleza kumuheshimu Ngalikumtwa.
Sasa huo ugomvi wa Catholic na Gwajima unatokea wapi??
Ngalikumtwa ni nani?

Mkuu hii thread yako imejaa hisia tu na hujaonyesha mashiko yoyote zaidi ya kutaka kutia hofu ambayo kimsingi haipo...
 
Mnakuza mambo na kumuwekea maneno mdomoni mwa Mtu...
Wote tulimsikia Gwajima, akieleza kumuheshimu Ngalikumtwa.
Sasa huo ugomvi wa Catholic na Gwajima unatokea wapi??
Ngalikumtwa ni nani?

Mkuu hii thread yako imejaa hisia tu na hujaonyesha mashiko yoyote zaidi ya kutaka kutia hofu ambayo kimsingi haipo...

Mkuu usitufanye sisi ni watoto na hatujasikia kilichosemwa na Gwajima.

Ukawa wangejituliza vyumbani na kuacha jambo hili lipite kimya kimya.kumtembelea Gwajima ina maana mnakubaliana na yote aliyosema Gwajima kitu ambacho si sahihi.

Tusiwe wanafiki.
 
kwenda kumtembelea mgonjwa sio kosa ,mimi sio mkatoliki alikuwa anapeleka ujumbe ila maneno aliyotumia hayakuwa na stahasana
 
Gwajima kweli ni shujaa, mpiganaji, msemakweli bila kuogopa, bora ukamuacha kuliko kumchokoza binafsi nampenda na ni mfano wa kuigwa swala la kutumia maneno ambayo hata muhusika hayamuumi. It's shame kabisa.
 
Na bado maana UKAWA hawawezi soma alama za nyakati....kumbe JF kuna vijana wana akili lakini wanavurugwa na mapenzi ya vyama vyao
 
Gwajima kweli ni shujaa, mpiganaji, msemakweli bila kuogopa, bora ukamuacha kuliko kumchokoza binafsi nampenda na ni mfano wa kuigwa swala la kutumia maneno ambayo hata muhusika hayamuumi. It's shame kabisa.

Wewe ndio mbumbumbu kbs CCM wapo kimya kwenye hili maana wanajua madhara yake......
 
Back
Top Bottom