Tindo
Platinum Member
- Sep 28, 2011
- 71,361
- 127,739
Nanukuu gazeti la HABARILEO
"UKIMYA wa wanasiasa walioongoza harakati za kupambana na ufisadi katika majukwaa ya kisiasa, wakati huu Serikali ikichukua hatua za wazi na haraka kukabiliana na ubadhirifu wa mali za umma, umeibua maswali kuhusu uzalendo kwa nchi yao.
Miongoni mwa wanasiasa waliohusishwa na maswali hayo ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu, Frederick Sumaye, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe na mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Mhadhiri Mwandamizi wa Masuala ya Siasa na Utawala wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Benson Bana, alisema kama kweli ni wazalendo, ni vyema wale wote waliokuwa wakipinga ufisadi wajitokeze hadharani, kupongeza hatua zinazoendelea kuchukuliwa".
Nami naongezea "magwiji wa kuzungumzia ufisadi - Lissu, Mnyika, Mdee nk" mko wapi kumuunga mkono Rais hata kwa kumpa majina ya mafisadi, au ndo mmefungwa
Midomo!
Mimi nilitaraji Magufuli ndio awapongeze wapinzani waliokuwa wakisema ukweli siku zote bila serekali kuchukua hatua. Wapinzani wamepiga kelele mpaka sasa makoo yamewakauka wanasubiri yale yote waliyokuwa wakiyasema yatekelezwe kisha wapongeze, maana wanajua ukianza kusifia sasa kuna hatari ya mgema akisifiwa....