UKAWA kushinda Umeya Dar ni muujiza uliomshinda S. Sitta

Mwikimbi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,762
828
Samweli Sitta yule spika wa bunge maalumu la katiba la mwaka jana ni mtenda muujiza asiyekubali kushindwa.

Hata baada ya Jakaya kikwete kutangaza hadharani theluthi mbili kupitishsa rasimu ya chenge, na hata Mwigulu kumtaka sita kuahirisha bunge lile kwa kutokuwa na uhakika na akidi ya theluthi mbili, bado kwa kujiamini sita alitenda muujiza kwa kupitisha rasimu ile kwa kura mbili ambazo hadi leo hazijulikani zilitoka wapi.

Wasaidizi wa mtenda muujiza huyo ni pamoja na Hamad rashid, naibu spika Tulia acson, na dr Francis Michael ambao ukimwacha Hamad rashid walizawadiwa kuwa board members wa Bandari baada ya kumsaidia mtenda muujiza kupitisha rasimu ya katiba kwa muujiza.

Mtenda muujiza hakukomea hapo bali ktk uchaguzi mkuu wa october 2015 alitenda tena muujiza mwingine kuhakikisha kuwa Magreth Sitta anapeta kwenye kura za maoni kupitia ccm ili kugombea kiti cha ubunge cha urambo. this time alihitaji kutenda muujiza ili aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa EWURA, Haruna Masebu asitie mguu kwenye hicho kinyanganyiro. katika kutenda huo muujiza sita alikuwa amebaki na silaha moja nayo ni uwaziri wake wa uchukuzi uliompa fursa ya kuteua tena wajumbe wa bodi ya bandari kunakosadikika kuwa ni shamba la bibi!

Hivyo Sitta akatenda muujiza kwa kumteua Haruna masebu kuwa mjumbe wa hiyo bodi, Kwahiyo Bwana akatenda muujiza tena, Masebu akawa mjumbe wa bodi ya TPA na hibyo akajitoa kwenye kinyanganyiro na Magreth sitta kapeta, Aksante muujiza.

Muujiza mwingine ni ule wa kutaka mwananwe awe meya wa manispaa ya kindondoni ambapo diwani Benjamini Sita(CCM-yenye madiwani 18) alikuwa akichuana na Diwani Jacob Boniface(ukawa-madiwani 38), muujiza UKAWA huo ulianza kwa vikao visivyoisha sebuleni kwa Sitta mwenyewe.

Tena kwa bahasha zilizonona lakini kwa bahati mbaya muujiza huu ukaishia kwa sitta kugeuka kuwa mfadhili wa ukawa, kwani pesa alizokuwa akiwahonga madiwani ni hizo hizo zilioztumika kugharamia vikao vya caucus ya UKAWA na baadaye kununua zile kalamu zenye kamera zilizomliza mwanae benjamini!

SITTA ENDELEA KUTENDA MIUJIZA.
 
Kumbe sita ni mchumia tumbo
 
sijui uchaguzi wa Meya wa Tanga CUF walishindwa vipi kuleta wabunge wa Pemba kuongeza idadi ya kura, Ila naamini kuna madiwani wa ukawa walisaliti na kuipigia ccm
 
Ndugu yangu kilichofanyika Tanga ni zaidi ya unavyoweza kufikiria.Ni kwamba,Uchaguzi ulifanyika,kura zikapigwa CCM wakapata kura 17 CUF kura 21.Wakati wa kusoma matokeo,mkurugenzi akayasoma kama yalivyo watu wa CUF wakaanza kushangilia,mkurugenzi akawatuliza ili atangaze mshindi rasmi mara pwaaaaa!mshindi ni wa CCM.Mkurugenzi akakimbia kutoka ukumbini na maaskari walikuwa wameshaandaliwa watu wa CUF waliojaribu kuleta vulugu wakatiwa ndani na mkurugenzi akapotea hadi sasa sidhani kama amesharudi ofisini.Yaani ilikuwa unyama unyamani.
 
so sad, lakini naamini hicho kitu kisingeweza kutokea Mbeya, iringa mjini au Arusha na watu kukaa kimya tu kama walivyokaa wanaukawa wa Tanga
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom