UKAWA kufungua kesi mahakamani leo

UKAWA kufungua kesi mahakamani leo

Riziki Magembe

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2014
Posts
886
Reaction score
206
Taarifa toka katika gazeti moja la leo la mtanzania 29/4/2014 limeripoti kuwa UKAWA wanajiandaa kumfungulia kesi mwanasheria mkuu wa serikali juu ya wa mjadala wa rasimu bungeni.

Mashtaka yake yatakuwa ni kutosimamia sheria inayowataka wajumbe wa bunge maalum kujadili rasimu iliyowasilishwa bungeni kwa mujibu wa sheria kinyume chake wajumbe wamejikita kujadili mambo ambayo hayamo katika rasimu iliyoletwa bungeni.

Sheria ya mchakato wa katiba namba 25(2) inasema wajumbe wataboresha rasimu na sikubadilisha ama kufuta yaliyomo ndani ya rasimu.

Mantiki ya kuboresha mfano wake ni kuwa nyumba ina madirisha 3 umeambiwa uyaboreshe maana yake sio kuongeza madirisha yawe 4 ama kupunguza yawe 2 ila mantiki yake kuyaboresha maana yake ni kama yalikuwa ya mbao unaweka ya viyoo lakini yale yale 3,kama yalikua hayana nondo za ulinzi unayawekea nondo lakini yatabakia yale yale 3 na sio kuongeza yawe 4 au kupunguza yawe 2,huko si kuboresha.
 
Wakuu katika kuonyesha dhamira ya dhati kuelekea upatikanaji wa katiba ya Wananchi,Mapema leo Mawakili wa Umoja wa katiba ya Wananchi wakiongozi na Wakili msomi Twaha Taslima watafungua kesi ya kikatiba katika mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam kutaka Tafsiri ya kisheria kuhusiana na Bunge maalum la katiba kujadili mambo yaliyo nje ya rasimu ya katiba.

-My take,Huu ni mwanzo mzuri hasa kuzingatia mbinu za CCM kupindua msingi wa rasimu ambyo msingi wake ni maonh ya wananchi.
 
DUh ,sasa kazi ,mashee nao wanampeleka Lukuvi mahakamani na mapadri nao wanampeleka Lukuvi mahakamani kwa kufanya siasa ndani ya kanisa lao badala ibada ,eti wanadai kwanini amegeuza nyumba ya ibada kufanyia mkutano wa serikali yake na chama hivi amekosa uwanja huko jangwani ? kazi kweeeli kwel !
 
ukawa baada ya kunyimwa posho wanahangaika sana
 
Kwa hiyo maandamano yameahirishwa au wanafanya vyote kwa Pamoja?? hivi Mtikila naye ni UKAWA??
 
wakuu mwaka huu ccm lazima waweseke tu
 
Hii ni akili ndogo, unafiki au zezeta?, binadamu aliye huru kimawazo hawezi kutoa mchango kama huu!
 
Now we are talking the same language UKAWA.People were asking what will UKAWA do to fight for the best constitution after walking out of the Parliament,Some dumb supporters of CCM thought they already won the battle after UKAWA decision,What they didn't know is that UKAWA had a PLAN B & C to fight for this katiba,Filing a constitutional case at the high court was that PLAN B.
 
Hii ni akili ndogo, unafiki au zezeta?, binadamu aliye huru kimawazo hawezi kutoa mchango kama huu!

Mbona umepaniki hivyo mkuu?Mapambano ya kuipigania Tanganyika ndiyo yameanza rasmi hivyo.Mind you,UKAWA wana back-up ya makundi mengi ya Watanzania nyuma yao wakiwemo Wasomi na Wataalam hivyo hii kesi lazima iwaendee kinyume na mnavyotaka.
 
Wakuu katika kuonyesha dhamira ya dhati kuelekea upatikanaji wa katiba ya Wananchi,Mapema leo Mawakili wa Umoja wa katiba ya Wananchi wakiongozi na Wakili msomi Twaha Taslima watafungua kesi ya kikatiba katika mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam kutaka Tafsiri ya kisheria kuhusiana na Bunge maalum la katiba kujadili mambo yaliyo nje ya rasimu ya katiba.

-My take,Huu ni mwanzo mzuri hasa kuzingatia mbinu za CCM kupindua msingi wa rasimu ambyo msingi wake ni maonh ya wananchi.
I'm afraid hoja hii haijakaa vizuri na nirahisi sana kujibiwa kisiasa. BMK linauwezo wa kuongeza ama kupunguza yaliyoko kwenye Rasimu kwa maslahi mapana ya nchi na wananchi wa Tanzania...
 
Sasa mahakama ndo itapiga kura bungeni?.
Upotezaji wa mda na hela bure.
Hata kama watashinda bado wabunge wengi wakagoma kupitisha kipengele cha muundo wa muungano,mahakama haiwezi kuwalazimisha.
 
Sasa mahakama ndo itapiga kura bungeni?.
Upotezaji wa mda na hela bure.
Hata kama watashinda bado wabunge wengi wakagoma kupitisha kipengele cha muundo wa muungano,mahakama haiwezi kuwalazimisha.
-Ha ha ha ha Unajitekenya nakucheka mwenyewe,
 
Back
Top Bottom