Ukawa kuandamana nchi nzima

Ukawa kuandamana nchi nzima

Kilaza

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2013
Posts
3,324
Reaction score
1,378
ukawaa.jpg


Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Freeman Mbowe akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Wanaomfuatia ni wenyeviti wenza wa umoja huo James Mbatia (katikati) na Profesa Ibrahimu Lipumba. Picha na Edwin Mjwahuzi


Na Fidelis Butahe na Hawa Mathias, Mwananchi

Kwa ufupi
Watangaza maandamano nchi nzima, ni iwapo Rais Kikwete hatasitisha Bunge la KatibaWamtaka CAG kukagua hesabu za Bunge hilo


Dar es Salaam.
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umemtaka Rais Jakaya Kikwete kusitisha Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea mjini Dodoma na iwapo hatafanya hivyo utaongoza maandamano nchi nzima.


Umoja huo pia umeeleza kuwa kuendelea kwa Bunge hilo ni sawa na kuvuruga mchakato wa kupata Katiba Mpya, kuiweka nchi rehani, kufuja fedha za walipakodi, kuwahadaa Watanzania kwa kupitisha Katiba isiyotokana na maoni yao, huku kanuni zikibadilishwa na kuingizwa mambo ya Tanganyika katika Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Kadhalika, umemtaka Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalumu wa matumizi ya fedha za Bunge hilo kwa maelezo kuwa zinatumika bila maelezo sahihi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, mwenyekiti mwenza wa umoja huo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) akiwa na wenyeviti wenzake, Freeman Mbowe (Chadema) na Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), alisema hawatataja muda lakini wanataka jambo hilo lifanyike haraka iwezekanavyo.

“Iwapo Rais Kikwete hatatumia mamlaka yake kusitisha Bunge na kukubali liendelee kinyume na matakwa ya wananchi, Ukawa tutawaongoza Watanzania kupaza sauti kupinga najisi inayotiwa kwenye maoni yao, kupitia maandamano na mikutano ya hadhara nchi nzima,” alisema Mbatia.

Akizungumzia iwapo Rais anayo mamlaka ya kusitisha vikao vya Bunge hilo, Wakili na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Jesse James alisema anaweza kufanya hivyo kwa kutumia dhamana ya uongozi aliyonayo, lakini kisheria hawezi kutokana na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kutokuwa na ibara inayompa mamlaka hayo.

“Rais ni Amiri Jeshi Mkuu, Mkuu wa nchi na Serikali. Majukumu hayo ndiyo yanayomfanya awe na uwezo wa kusitisha shughuli za Bunge hilo, hasa akiona theluthi mbili ya wajumbe kutoka kila upande kwa ajili ya kufanya uamuzi haitapatikana.”

Aprili 16, mwaka huu wajumbe wanaotokana na vyama vya siasa vinavyounda Ukawa na baadhi kutoka Kundi la 201, walisusia vikao vya Bunge hilo wakitaka msingi wa mapendekezo ya Rasimu ya Katiba usibadilishwe, wakipinga uamuzi wa CCM kutaka kuingiza mfumo wa serikali mbili badala ya tatu zilizopendekezwa katika rasimu.

Mbatia alisema Ukawa imechukua uamuzi wa kuandamana kutokana na wajumbe wa CCM pamoja na wengine 166 walioteuliwa kupitia kundi la wajumbe 201, kuendelea na vikao vya Bunge hilo na kuingiza mambo yao katika Rasimu ya Katiba, huku wakilipwa fedha za walipakodi.

“Mambo wanayoyajadili na kuyachomeka kinyemela kwenye rasimu kama ardhi, elimu, maji, kilimo, uvuvi, mifugo na serikali za mitaa ni masuala yanayopaswa kuandikwa kwa kina ndani ya Katiba ya Tanganyika siyo Katiba ya Jamhuri ya Muungano,” alisema Mbatia na kuongeza:

“Zanzibar walijadili wenyewe mambo yao ya ndani na kutengeneza Katiba yao, hivyo hatuoni mantiki ya wajumbe kutoka Zanzibar kujadili na kuamua mambo ya Tanganyika. Bunge la Katiba halina sifa za kujadili mambo yasiyo ya muungano. Hii inaonyesha CCM wamelewa madaraka.”

Alisema ili Bunge hilo lipate uhalali wa kuendelea yanatakiwa kufanyika maridhiano ya pande zote zinazovutana na kusisitiza kuwa kinachoendelea sasa kinatokana na kukosekana kwa uongozi wa kisiasa.

“Wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisema kuwa suala la muundo wa serikali lilitakiwa kupigiwa kura, Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samwel Sitta anaendelea kuongoza Bunge kama mchakato ni mali yake binafsi. Baadhi ya viongozi wa chama hicho wanataka mchakato usitishwe, wengine wanataka uendelee,” alisema.

Mbatia alisema Ukawa inashangazwa na Rais Kikwete kwa kitendo chake cha kufanya ziara ya kutembelea ranchi binafsi ya kufugia wanyama ya aliyekuwa Rais wa Marekani, George Bush wakati nchi ikiwa katika sintofahamu ya mchakato wa kupata Katiba Mpya huku watu wa kada mbalimbali wakitaka mchakato usitishwe.

Profesa Lipumba alisema: “Wapo wanaosema kuwa Ukawa tumegawanyika. Hilo siyo kweli kwa sababu waliotusaliti na kuhudhuria vikao vya Bunge hata asilimia tano hawafiki. Zaidi ya asilimia 95 hatujakwenda bungeni,” alisema.

Alisema kuwa Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba alitenga masuala ya ardhi, maliasili na Serikali za Mitaa ili yaingizwe katika Katiba ya Tanganyika, hivyo kuyajadili mambo hayo katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano si sahihi. Mbowe alisema: “Viongozi wanaiacha nchi ijiendeshe yenyewe. Ni kama ndege ambayo rubani yupo lakini ameweka ‘auto pilot’, yaani wameiruhusu ndege ijiendeshe yenyewe.”


CAG achunguze

Kuhusu suala la ukaguzi wa hesabu, Mbatia alisema katika vikao vya Bunge la Bajeti, baadhi ya wabunge walihoji zinakopatikana fedha za kuendesha Bunge la Katiba na kusema kutokana na hali hiyo, ni vyema CAG akachunguza kwa undani suala hilo.

Hoja kutaka Bunge hilo lisitishwe inaungwa mkono na makundi mbalimbali pamoja na baadhi ya wabunge wa CCM, akiwamo Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba (Iramba-Magharibi) aliyesema likiendelea bila uhakika wa kupata akidi ya uamuzi itakuwa ni kupoteza zaidi ya Sh20 bilioni za walipa kodi na wananchi hawataelewa.

Hata hivyo, uongozi wa Bunge umesisitiza kuwa vikao hivyo ambavyo awali vilifanyika kwa siku 67, vitaendelea kwa siku 60 za kazi zilizoongezwa na Rais Jakaya Kikwete, bila kuhusisha siku za Jumamosi na Jumapili ambazo zinaongeza muda wa wajumbe kukaa Dodoma kuwa 84.

CHANZO: Mwananchi




TAARIFA KWA UMMA


KUHUSU


MCHAKATO WA KATIBA MPYA NA YANAYOENDELEA BUNGE MAALUM LA KATIBA


Ndugu wanahabari


Sote tunaelewa kuwa kwa matakwa ya CCM, Bunge Maalum la Katiba (BMK) limeendelea kufanya vikao vyake mjini Dodoma kuanzia Agosti 5 mwaka huu, kinyume kabisa na matarajio ya Watanzania, ambao kupitia fursa mbalimbali wamepaza sauti zao wakisisitiza maridhiano na mwafaka wa kitaifa kutangulizwa mbele badala ya maslahi ya watawala.

Tukiwa viongozi wa kisiasa ambao ni sehemu ya uongozi ndani ya jamii, wenye wajibu wa kuwa na maono chanya na muhimu kwa taifa letu, tumeendelea kufuatilia kwa karibu namna mchakato wa Katiba Mpya unavyoendelea kunajisiwa kupitia vikao hivyo vya BMK linaloendelea mjini Dodoma, likitumia rasilimali za taifa, zikiwemo kodi za Watanzania wanyonge, kujadili vitu visivyotokana na wananchi.


Mtu yeyote makini ataweza kubaini kuwa kwa namna mchakato wa Katiba Mpya unavyopelekwa au unavyokwenda kwa sasa ni matokeo ya kukosekana kwa uongozi wa kisiasa kwa Chama kinachoongoza Serikali, CCM.


Kuna ombwe kubwa la uongozi wa kisiasa katika jambo hili. Ni kama vile mchakato unajiendea tu wenyewe bila mwongozo wowote kutoka kwa watu walioko madarakani ambao wananchi walitarajia wangetumia mamlaka yao ya dhamana ya uongozi ili taifa lipite salama katika wakati huu mgumu na tupate Katiba Mpya na bora.


Vipo viashiria vingi tu vinavyoweka wazi hali hiyo ya ombwe la uongozi wa kisiasa katika mchakato huu wa kisiasa, ikiwa ni pamoja na kauli kinzani za viongozi wa Serikali na CCM yenyewe.

Wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza kama vile kunahitajika mazungumzo zaidi na kwamba suala la muundo wa serikali lilipaswa kupigiwa kura kabla, Mwenyekiti wa BMK anaendelea kuongoza bunge kama vile mchakato ni mali binafsi ya CCM na walioko madarakani.

Wakati baadhi ya viongozi wa Serikali ya CCM wakitoa kauli za kuhitaji kuwa makini na taratibu za kuendesha mchakato huu chama chao kinatoa kauli za kuzidi kuharamisha na kutia najisi mchakato mzima. Mchakato unakwama, nchi inayumba, Watanzania wako katika sintofahamu kwa sababu tu tumekosa uongozi wa kisiasa katika jambo hili.


Kiashiria kingine cha pengo hilo la uongozi wa kisiasa ambacho kwa kweli kwetu sisi kimetusikitisha zaidi kitendo cha Rais Jakaya Kikwete kuendelea na ‘hamsini zake’ kama vile nchi haina tatizo lolote.


Yaani wakati nchi na wananchi wako katika sintofahamu ya hatma ya Katiba Mpya itakayoweka misingi ya wao kujitawala na kuongozwa watakavyo, makundi mbalimbali yakipaza sauti zao, mataifa mengine yakituangalia kwa makini na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wakifuatilia mchakato, Rais Kikwete anapata muda wa kutembelea ranch ya Rais Mstaafu wa Marekani George Bush!


Wakati Rais Kikwete akiendelea kutalii dunia, wenzake wako mjini Dodoma wakichukua posho kwa kazi ambayo wananchi hawajui wanaifanya kwa maslahi ya nani!


Kwa ujumla mambo yote yanayoendelea sasa katika mchakato huu ni matokeo ya ombwe hilo kama tulivyosema.


Inaonesha kuwa CCM wamelewa madaraka na viongozi wanaona dhamana ya uongozi iko juu ya wananchi hivyo hawajali umuhimu na nafasi ya mamlaka ya wananchi katika kuamua mstakabali wa taifa lao kwa ajili ya kizazi cha sasa na kuweka msingi wa vizazi vingi vijavyo.

Hivyo leo tungependa kuzungumza tena kuhusu Rasimu ya Katiba na mchakato wenyewe hapa ulipokwama;

Tunapenda kusema wazi kuwa tumeshangazwa sana na kitendo cha CCM na Serikali yake kulazimisha kuendelea kwa Bunge Maalum la Katiba Mpya, tena kwa mtindo ule ule wa kunajisi na kupuuza maoni ya wananchi yaliyomo kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya kama yalivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.


Wamefanya hivyo pasi na kujali kilio cha wananchi kinachopazwa kutoka kila kona ya nchi, ambapo Watanzania mmoja mmoja na katika makundi mbalimbali wametaka maoni yao yazingatiwe kwa kujadiliwa, kuboreshwa na kisha kupitishwa na Bunge Maalum la Katiba kabla wao hawajayapigia kura ya maoni kwa ajili ya kuipitisha au kuikataa Rasimu ya Katiba Mpya.


Wajumbe wanaotokana na CCM pamoja na makada wengine wapatao 166 wa chama hicho ambao waliteuliwa kuingia kwenye bunge hilo kusimamia maslahi ya CCM kupitia kundi la wajumbe 201, wameamua bila haya mbele ya umma si tu kupuuza rasimu iliyotokana na maoni ya wananchi bali sasa wameamua kuingiza mambo yao waliyodhamiria tangu mwanzo kwa kadri ya maamuzi na maelekezo ya vikao vya chama hicho vikiongozwa na Mwenyekiti wao Jakaya Kikwete.


Bila kujali wala kuguswa na miito ya Watanzania mbalimbali wanaotaka jambo hili liongozwe na maridhiano kwa ajili ya mwafaka wa kitaifa badala ya kuweka matamanio ya watawala mbele, CCM na mawakala wao katika mchakato huu wameendelea pia kufuja na kutumia vibaya fedha za wananchi kupitia Bunge Maalum la Katiba kwa kujadili na kuingiza vitu visivyokuwemo au visiyotakiwa kuwa sehemu ya rasimu hii iliyopo sasa.


Hali hiyo imefanyika kwa namna kadhaa ikiwa ni pamoja na kutofuata sheria inayosimamia mchakato mzima, kubadili kanuni za uendeshaji wa BMK hasa katika taratibu za kujadili na kupitisha ibara na kubwa zaidi kuingiza masuala ya Tanganyika kwenye Rasimu ya Katiba ya Muungano.


Kimsingi masuala wanayoyajadili na kuyachomeka kinyemela kwenye Rasimu ya Pili ya Warioba, mathalan masuala ya Ardhi, Elimu, Maji, Kilimo, Uvuvi, Mifugo, Serikali za Mitaa nk ni masuala yanayopaswa kuandikwa kwa kina ndani ya Katiba ya Tanganyika na siyo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Ni vyema kukumbuka kuwa Zanzibar walijadili wenyewe mambo Yao ya Ndani na kutengeneza Katiba yao na hatuoni mantiki ya kuruhusu Wajumbe toka Zanzibar kujadili na kuamua mambo ya Tanganyika. BMK haina Sifa ya kujadili yasiyo ya Muungano.


Hivyo tofauti na wanavyotaka kujionesha katika jamii, CCM kupitia BMK wameamua kupindua kabisa rasimu nzima na kuweka maazimio ya vikao vyao kuwa ndiyo Katiba ya Tanzania. Jambo hili haliwezi kukubalika.


Kutokana na uchakachuaji huo wa Katiba Mpya unaoendelea kufanywa na CCM kupitia BMK, UKAWA tumefikia maamuzi yafuatayo;


· Tunamtaka Rais Jakaya Kikwete asitishe shughuli za BMK mara moja lisiendelee kuvuruga
na kuharibu mchakato wa Katiba Mpya na kuiweka nchi katika sintofahamu juu ya jambo hili
nyeti;

· Tunamtaka Rais Kikwete asitishe BMK ili lisiendelee kufuja fedha za Watanzania maskini
wanaopigania Katiba Mpya iwapatie matumaini ya kuongozwa na kujitawala wanavyotaka.


· Tunamtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalum
kwenye matumizi ya fedha za BMK ambayo kuanzia Bunge la Bajeti lililopita tumebainisha
wazi kuwa yana uvundo mkubwa wa ufisadi na hayana maelezo sahihi.


· Iwapo Rais Kikwete atashindwa kutumia mamlaka yake kusitisha BMK na hivyo likaendelea
kinyume cha matakwa na maslahi ya wananchi kama lilivyofanya awali na linavyofanya sasa,
UKAWA tutawaongoza Watanzania kupaza sauti zaidi kupinga najisi inayotiwa kwenye maoni
yao, kupitia maandamano na mikutano ya hadhara nchi nzima.



Asanteni kwa kutusikiliza.


Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
Mwenyekiti CUF


Freeman Aikaeli Mbowe
Mwenyekiti CHADEMA


James Francis Mbatia
Mwenyekiti NCCR Mageuzi


Wilbrod Peter Slaa
Kny Makatibu Wakuu, UKAWA.




NB Ikumbukwe JINI likitoka kwenye CHUPA huwa halirudi ndani ya CHUPA serikali 3 ni lazima sio ombi tena.
 
Tunawatakia kila la heri kitu cha maana ni ujumbe maalum katika mikutano si kutukana au kumwaga kashfa.Ningependa mikutano hiyo ilenge kuwajenga na kuwafunza waTanzania uchafu unaofanywa na bunge la posho huko mjini Dodoma.
 
Ndicho wan akitaka CCM hiki sio ? Na yaani is dodoma kwa yule mkuu wa Mkoa wa hovyo asiyejua sheria .....
 
UKAWA KUFANYA MAANDAMANO NCHI
NZIMA KUANZIA WIKI IJAYO YASIYOKUWA
NA RATIBA WALA KIKOMO.
Mhe James Mbati akisoma Tamko la UKAWA
kwa niaba ya Mchumi wa Kimataifa Prof I
brahim Lipumba na Freeman Mbowe
"Maandamano Nchi nzima na Mikutano ya
Hadhara kwa ajili ya kuhamasisha watu
kupinga matumizi mabaya ya Fedha za
Wananchi katika Mchakato wa Bunge Maalum
la Katiba."
Mhe; Mbatia ameendelea kusema "Baada ya
kukamilika kwa Mazungumzo yanayoendelea
na CCM wiki hii.Hata hivyo Ukawa
wamesema,kwa kadiri mazungumzo
yanavyoendelea hakutakuwa na tija hivyo
ameamua kuweka wazi azma ya kufanya
maandamano"
Professa Lipumba amerudia WITO wake wa
kuwataka VIJANA kuanza mazoezi ya VIUNGO
kwajili ya ukombozi.
Freeman Mbowe amesema NGUVU ya UMMA
sasa kutumika ili kuleta UKOMBOZI hakuna
kulala mpaka kieleweke kuanzia wiki ijayo.
Ni MAANDAMANO ni MAANDAMANO mpaka
Mkoloni mweusi atupatie KATIBA yetu.
NB Ikumbukwe JINI likitoka kwenye CHUPA
huwa halirudi ndani ya CHUPA serikali 3 ni
lazima sio ombi tena.

Protest is not allow
 
Kwa taarifa hii wazee wa feva bila shaka wameenza kusafisha mitutu yao ya mabomu ya mchozi
 
UKAWA KUFANYA MAANDAMANO NCHI
NZIMA KUANZIA WIKI IJAYO YASIYOKUWA
NA RATIBA WALA KIKOMO.
Mhe James Mbati akisoma Tamko la UKAWA
kwa niaba ya Mchumi wa Kimataifa Prof I
brahim Lipumba na Freeman Mbowe
"Maandamano Nchi nzima na Mikutano ya
Hadhara kwa ajili ya kuhamasisha watu
kupinga matumizi mabaya ya Fedha za
Wananchi katika Mchakato wa Bunge Maalum
la Katiba."
Mhe; Mbatia ameendelea kusema "Baada ya
kukamilika kwa Mazungumzo yanayoendelea
na CCM wiki hii.Hata hivyo Ukawa
wamesema,kwa kadiri mazungumzo
yanavyoendelea hakutakuwa na tija hivyo
ameamua kuweka wazi azma ya kufanya
maandamano"
Professa Lipumba amerudia WITO wake wa
kuwataka VIJANA kuanza mazoezi ya VIUNGO
kwajili ya ukombozi.
Freeman Mbowe amesema NGUVU ya UMMA
sasa kutumika ili kuleta UKOMBOZI hakuna
kulala mpaka kieleweke kuanzia wiki ijayo.
Ni MAANDAMANO ni MAANDAMANO mpaka
Mkoloni mweusi atupatie KATIBA yetu.
NB Ikumbukwe JINI likitoka kwenye CHUPA
huwa halirudi ndani ya CHUPA serikali 3 ni
lazima sio ombi tena.

Tuko pamoja sana makamanda.lazima kieleweke
 
Kusema kweli pamja na kuwaunga mkono 100% kwa kutoenda Bungeni kwa hili sioni mantiki. Wakae kimya maana kimya kingi kina mshindo mkubwa. Wakati wa kuhamasisha umma kupinga rasimu ya Sitta bado.
 
UKAWA KUFANYA MAANDAMANO NCHI
NZIMA KUANZIA WIKI IJAYO YASIYOKUWA
NA RATIBA WALA KIKOMO.
Mhe James Mbati akisoma Tamko la UKAWA
kwa niaba ya Mchumi wa Kimataifa Prof I
brahim Lipumba na Freeman Mbowe
"Maandamano Nchi nzima na Mikutano ya
Hadhara kwa ajili ya kuhamasisha watu
kupinga matumizi mabaya ya Fedha za
Wananchi katika Mchakato wa Bunge Maalum
la Katiba."
Mhe; Mbatia ameendelea kusema "Baada ya
kukamilika kwa Mazungumzo yanayoendelea
na CCM wiki hii.Hata hivyo Ukawa
wamesema,kwa kadiri mazungumzo
yanavyoendelea hakutakuwa na tija hivyo
ameamua kuweka wazi azma ya kufanya
maandamano"
Professa Lipumba amerudia WITO wake wa
kuwataka VIJANA kuanza mazoezi ya VIUNGO
kwajili ya ukombozi.
Freeman Mbowe amesema NGUVU ya UMMA
sasa kutumika ili kuleta UKOMBOZI hakuna
kulala mpaka kieleweke kuanzia wiki ijayo.
Ni MAANDAMANO ni MAANDAMANO mpaka
Mkoloni mweusi atupatie KATIBA yetu.
NB Ikumbukwe JINI likitoka kwenye CHUPA
huwa halirudi ndani ya CHUPA serikali 3 ni
lazima sio ombi tena.



aaaaggr? nawasubiri mtaani...... ngrrrrriiiii waje na viongoz?
 
Waandamane hata mpaka baharini kwenye kina kirefu kwani nani kawaambia kuwa mandamano yanaleta suruhu ya jambo kama siyo wanaongozwa na mibangi.
 
Safi sana nasubiri amri ya ukawa tu ili niandamane maana niliya miss maandamano Sio mchezo

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Safi sana nasubiri amri ya ukawa tu ili niandamane maana niliya miss maandamano Sio mchezo

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
Safari hii kwenye haya mandamano zamu yako kufa kwenye mandamano.
 
Kusema kweli pamja na kuwaunga mkono 100% kwa kutoenda Bungeni kwa hili sioni mantiki. Wakae kimya maana kimya kingi kina mshindo mkubwa. Wakati wa kuhamasisha umma kupinga rasimu ya Sitta bado.
Hawana kazi ya kufanya acha wakatembee mtaani wauze sura wataonekanaje bila kujiuza.
 
Tunawatakia kila la heri kitu cha maana ni ujumbe maalum katika mikutano si kutukana au kumwaga kashfa.Ningependa mikutano hiyo ilenge kuwajenga na kuwafunza waTanzania uchafu unaofanywa na bunge la posho huko mjini Dodoma.

Kueleza ukweli si matusi wala kashfa, nadhani Tz tuna matatizo kwenye mfumo wa elimu kama kiswahili chetu wenyewe kinatushinda
 
Mi nilisema UKAWA yenye chadema vurugu ni lazima. maandamano na vurugu ndo misingi ya cdm imewaambukiza UKAWA
 
Tatizo kule mjengoni hawakai bure....ingekua wanakaa bure kujadili katiba yao, tungewaachia warekebishe hadi nukta afu tuje kuipinga
 
Kusema kweli pamja na kuwaunga mkono 100% kwa kutoenda Bungeni kwa hili sioni mantiki. Wakae kimya maana kimya kingi kina mshindo mkubwa. Wakati wa kuhamasisha umma kupinga rasimu ya Sitta bado.

yanapingwa matumizi mabaya ya fedha za umma kutokana na kujadili mambo ambayo hatujawatuma.
 
Back
Top Bottom