Mdokezi2
Member
- Apr 4, 2014
- 70
- 5
UKAWA NA HATMA YA BUNGE MAALUM LA KATIBA.
UKAWA (Umoja wa Katiba ya Wananchi) wakiwa ni washiriki halali wa Bunge Maalum lililoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliamua kususia vikao vya bunge hilo ikiwa ni njia ya kushinikiza madai yao.
Baadhi tu ya madai waliyotoa ni pamoja na: kile walichodai kuwa ni kupuuzwa kwa maoni ya wananchi km yalivyokusanywa na tume ya mabadiliko ya katiba.
Pili kutupiwa maneno machafu na baadhi ya wajumbe wa bunge hilo. Kutokana na hayo pamoja na mengine kwa kauli moja waliamua kususia bunge.
Usahihi na makosa ya mbinu waliyochagua:
Kiujumla mbinu hii SIO SAHIHI kutokana na sababu zifuatazo:
>>Haukuzingatia utaratibu sahihi wa kuwasilisha madai yao kwa uongozi wa bunge. Utaratibu ni kupeleka madai ktk kamati inayohusika na masuala wanayodai ndani ya bunge. Hakukuwa na mantiki yoyote ya kutoka bungeni.
>>Hauoneshi ukomavu wao kisiasa na uelewa wao wa kusuluhisha matatizo na migogoro ndani ya ofisi na kwingineko pia.
Hili ni jambo la kushangaza kwa watu wenye nyadhfa kubwa na uzoefu ktk siasa kufanya kitendo kama kile. Tulitegemea wao ndio wawe mwanga ktk kutuonesha uwezo wao wa kusuluhisha migongano baina ya viongozi na jumuia yoyote ile kwa ujumla. Wanatupa mashaka juu ya uwezo wao wa kusuluhisha migogoro ndani ya ofisi na vyama vyao!!
>>Pia hakukuwa na hali mbaya au iliyokuwa inatishia kuvurugika kwa vikao hivyo endapo wangeendelea kuwepo bungeni.
Hali ilikuwa shwari kiasi cha kuruhusu wao kufuata taratibu za kusikilizwa madai yao.
Kwa kumalizia tu niwasihi wajumbe wa UKAWA kurejea ktk kitabu cha kanuni za Bunge Maalum la Katiba na wapate utaratibu sahihi wa kuwasilisha madai yao.