magode
JF-Expert Member
- Oct 2, 2014
- 2,204
- 3,337
Baada ya kukamatwa aliyekuwa kamishina wa kodi TRA bwana Kitilya na mkwe wa Lowassa aliyewahi kuhudumu benki ya Stanbic,nimegundua hii kamata kamata hawa wanatangulia mbele tu,kuna mtu anatafutwa.
Kwa jinsi hali ilivyo,na mkuu wa kaya alivyopata shida wakati wa kampeni,sina shaka kabisa kesi ya Richmond inaibuliwa na ikiibuliwa itakuwa na maana kubwa sana kwa serikali na CCM.
Kama itaibuliwa itakuwa na faida kubwa sana kwa watawala. Lakini faida kubwa zaidi ni pigo watakalopata upinzani kwa kukamatwa aliyetajwa kama mhusika mkuu wa sakata hilo ambae pia alikuwa mgombea Urais wa Upinzani kupitia UKAWA. Takukuru wanajaribu kutanguliza hawa ili watu wasije kuona cha ajabu kukamatwa kwa Lowassa.
Ule msisitizo wa kumuombea mkuu wa kaya ili atumbue majipu maombi hayo kwa kiasi kikubwa ni kukamatwa kwa mhusika mkuu wa Richmond. Huu siyo utabiri ni jambo linalochemka,nimeliweka mapema ili we mwanaJF uwe wa kwanza kujua. Endelea kubaki hapa hapa siku si nyingi utajua ukweli.
UKAWA jiandaeni kwa pigo hili takatifu na kwa bahati mbaya nyinyi mtakuwa sehemu ya mashahidi hasa machapisho ya nyuma ya mwanahalisi. Kati ya mkenge mlioingia CHADEMA,huu mzimu wa Lowassa ni kiboko...!!
Nawasilisha..