UKAWA hamueleweki, watanzania tunawashangaa

UKAWA hamueleweki, watanzania tunawashangaa

Joined
Nov 23, 2011
Posts
45
Reaction score
17
Wakati tume ya uchaguzi ikiendelea kutangaza matokeo ya urais kupitia mgombea wenu mlisema kura zinazotangazwa na tume siyo sahihi, kuna uchakachuaji hivyo hamtakubaliana na kinachofanywa na tume, tume iliendelea na kazi yake na mwishoni ikatangaza mshindi.

Kuanzia mshindi wa uraisi atangazwe hadi leo mmekaa kimya; tuwaeleweje ili hali mlisema mmeibiwa kura? kama mna uhakika na ushahidi wa madai yenu kwanini hamjajitokeza hadharani na kuwaambia watanzania ukweli?
UKAWA HATUWAELEWI MNATUPA MASHAKA !
 
Kwanza ungejiuliza kwa nini CCM na Polisi kupitia Kova walipiga marufuku ule mkutano wa UKAWA Jana pale jangwani? Na sababu zilikuwa eti hali haijatengemaa jiulize no hali ipi hiyo ambayo haijatengemaa? Ukipata jibu utajuwa nini kilifanyika.
 
Kati ya vitu ambavyo nilishawahi kulalamikia viongozi wa UKAWA ni Idara yao ya Habari, hawa jamaa(kama wapo) sijui wanafanya kazi gani.

Moja wanaweza kutoa taarifa kisha wasiitendee kazi au wanaweza kutotoa taarifa kabisa(pale panapohitajika).

Kujiamini kupita kiasi ni tatizo.
 
Walichonifanyia CCM ni sawa na kuniingilia...............bila hata mate.
 
alaf walitwambia tusubiri ujio wa TB Joshua, haya jamaa keisharudi kwao mnangoja nini? Ebu ingia mitaani kama hawa jamaa muone cha mtema..#HapaKaziTU

Maandamano.jpg Maandamano.jpg
 
Wakati tume ya uchaguzi ikiendelea kutangaza matokeo ya urais kupitia mgombea wenu mlisema kura zinazotangazwa na tume siyo sahihi, kuna uchakachuaji hivyo hamtakubaliana na kinachofanywa na tume, tume iliendelea na kazi yake na mwishoni ikatangaza mshindi.

Kuanzia mshindi wa uraisi atangazwe hadi leo mmekaa kimya; tuwaeleweje ili hali mlisema mmeibiwa kura? kama mna uhakika na ushahidi wa madai yenu kwanini hamjajitokeza hadharani na kuwaambia watanzania ukweli?
UKAWA HATUWAELEWI MNATUPA MASHAKA !

Wametumia busara kukaa kimya na kama unakumbuka 08.11.2015 walitaka kufanya mkutano jangwani ila polisi walikataa mkutano huo na wakasema watarejea tena.Kuwa mpole TANZANIA KWANZA
 
Kuna vyombo vingi vya kimataifa. Wanashindwa kutumia vyombo hata magazeti ya Kenya ambayo hayafungwi na sheria za Tanzania, na tv mbali mbali za kigeni zilizopo hapa wakaweka wazi matokeo sahihi na vielelezo vyao?

Ninaona kama kun atatizo hapa.
 
Siwezi kujiuliza hilo swali kwani mshindi alitangazwa tarehe 29 oktoba na baada ya kutangazwa mshindi raisi akaapishwa tarehe 05 Novemba, huo muda wote (siku 8) ukawa walikuwa wapi wasiseme kile walichokuwa wanadai?kwanini wasubiri hadi tar. 08 novemeba? Tunataka ukawa mtuambie Ukweli na mkiendelea kunyamaza tutajua mlikuwa mnasema uongo!
 
Kwani katiba inasemaje kuhusu raisi aliyetangazwa baada ya uchaguzi?
 
Sisi hatuna shida na katiba kwani walivyokuwa wanaingia kwenye uchaguzi si walikuwa wanaijua katiba na wanaijua tume ya uchaguzi? kwanini wasingepambana kipengele cha katiba kirekebishwe ili matokeo ya uraisi yahojiwe mahakamani na pia kwanini hawakupambana ipatikane tume huru ya uchaguzi kabla ya uchaguzi? Tunataka ukawa waje hadharani watuambia kama kweli kura za Mh. Lowassa ziliibiwa, na kama hazikuibiwa wafute ile kauli ya awali.
 
kwa sasa nchi inaongozwa kijeshi. taratibu zote za kiraia hazifuatwi...
 
Kwanza ungejiuliza kwa nini CCM na Polisi kupitia Kova walipiga marufuku ule mkutano wa UKAWA Jana pale jangwani? Na sababu zilikuwa eti hali haijatengemaa jiulize no hali ipi hiyo ambayo haijatengemaa? Ukipata jibu utajuwa nini kilifanyika.

kwa hiyo pale kwenye mkutano ndio mngemuapisha mamvi?!
 
Back
Top Bottom