UKAWA haina ajenda ya kukemea rushwa tena

UKAWA haina ajenda ya kukemea rushwa tena

Rushwa imekuwa kama mila na destuli ndani ya CCM,Dr Magufuli hawezi kulimaliza hili tatizo tusidanganyane hapa,rushwa hiyo hiyo ndiyo inayotumika sasa hivi kutaka kumwingiza Dr Magufuli madarakani na Dr Magufuli hajalikemea jambo hili mpaka sasa,kitendo cha kutumia kiasi kikubwa cha pesa kwa wasanii ili waandamane na Dr Magufuli ktk kampeni zake ni rushwa pia,au wenzetu sijui rushwa mnaielewaje?
 

Kutoka FB:

.."Slaa jana alinishangaza...kabla hajasafiri alisema mwenyewe kuwa kinywa chakekuwa Ilani ya CHADEMA ambayo Mh.Lowassa anainadi leo, iliandaliwa kabla Mh.Lowassa hajaingia CHADEMA na yeye Slaa alishiriki vyema kuiandaa (akitegemea kuja kupeperusha bendera ya CHADEMA).
Baada ya kurudi safari ..anasema Ilani ya CHADEMA haizungumzii ufisadi..!!! Duh huyu Daktari vipi..mbona anajikologa...!!??

Hii imenibidi niperuzi tena Ilani ya CHADEMA..na nikakutana na hichi kipengelee...
Nukuu......
" UZALENDO, UTENDAJI NA UWAJIBIKAJI
Tutajenga uzalendo ili kila Mtanzania aweze kutathmini mchango wake kwa taifa kila siku
Tutaimarisha nidhamu, utendaji na uwajibikaji katika Sekta ya Umma
Tutaimarisha mchango wa Wataalam wetu, wanawake na vijana katika kusimamia uchumi na kuwajengea mazingira stahiki ya kazi pamoja na mafao.
TUTAPIGA VITA RUSHWA/UFISADI NA UBADHIRIFU katika sekta ya Umma na binafsi
Tutadhibiti na kupunguza matumizi ya serikali ikiwa ni pamoja na kufuta safari za watumishi serikalini zisizokuwa muhimu pamoja na zile za Rais na kupiga marufuku matumizi ya mashangingi serikalini.
Tutadhibiti deni la Taifa kwa kuanza na ukaguzi wa madeni ya serikali ili kuhakiki jinsi yalivyotumika
Tutaimarisha uwazi na kuondoa usiri katika shughuli za serikali na kuweka bayana mikataba yote ya nchi ikiwa ni pamoja na ile ya mafuta, madini na gesi asilia "
.....Mwisho wa kunukuu.
Hivi ina maana Daktari mara hii kasahaua Ilani aliyoandika mwenyewe ??
KWELI UTUMWA WA PESA UNALETA OPOFU WA FIKRA.
R.I.P FIKRA ZA DAKTARI.
VIVA MABADILIKO. ""




Na MwanaJamii

02:41

Kama magufuli ni muadilifu Lowassa sio muadilifu

Kama magufuli anakemea wala rushwa lowasa hakemei wala rushwa

Unaposema bora mchafu mmoja katika kundi la wasafi kuliko msafi mmoja katika kundi la wachafu usisahau kukumbuka kuwa huyo msafi au mchafu yupo katika nafasi gani na uwezo wake na maamuzi yake na mipaka yake na matarajio yake na uwezo wake

HOJA NI KWAMBA

Mchafu mmoja anachafua kundi lote kwasababu yeye ndio kiongozi top na mfano wa kuigwa na kutokana na uchafu wake hawezi kuwanyooshea vidole wachafu wenzake NA msafi mmoja anaweza kusafisha kundi lote kwakuwa yeye Ana mamlaka na uwezo huo

Nafasi inayotafutwa ni ya Urais ambaye ndie amiri jeshi mkuu na mwenye uwezo na mamlaka ya kufagia nyumba sasa umeona wapi mchafu aanze kuwasafisha wenzake wakati yeye ni mchafu

TAFAKARI CHUKUA HATUA

MAGUFULI NI muadilifu kuliko lowasa

#TunzaKichinjioChakoSubiri25OktobaUchinjeLowasa
 
Your ignorant you dont reason and logic! twambie ni kwel kuwa kuondoka kwa lowassa mafisadi wameisha CCM? ucpotoshe jamii, ieleweshe au umetumwa na CCM kurubuni watu? Huwez nambia kuwa maovu yote yaliyotokea tz na yanayotokea tz. chanzo chake ni lowassa, epuka kuongea uongo mwogope ALLAH.
 
Tunahitaji katiba mpya yenye meno ya kupambana na rushwa na sio hayo maneno ya kipuuzi majukwaani.Sasa jiulize katika ilani ya cdm na ccm ni ipi ina ajenda\ Sera ya katiba mpya? Lowasaaaaaaa
 
Na MwanaJamii

02:41

Kama magufuli ni muadilifu Lowassa sio muadilifu

Kama magufuli anakemea wala rushwa lowasa hakemei wala rushwa

Unaposema bora mchafu mmoja katika kundi la wasafi kuliko msafi mmoja katika kundi la wachafu usisahau kukumbuka kuwa huyo msafi au mchafu yupo katika nafasi gani na uwezo wake na maamuzi yake na mipaka yake na matarajio yake na uwezo wake

HOJA NI KWAMBA

Mchafu mmoja anachafua kundi lote kwasababu yeye ndio kiongozi top na mfano wa kuigwa na kutokana na uchafu wake hawezi kuwanyooshea vidole wachafu wenzake NA msafi mmoja anaweza kusafisha kundi lote kwakuwa yeye Ana mamlaka na uwezo huo

Nafasi inayotafutwa ni ya Urais ambaye ndie amiri jeshi mkuu na mwenye uwezo na mamlaka ya kufagia nyumba sasa umeona wapi mchafu aanze kuwasafisha wenzake wakati yeye ni mchafu

TAFAKARI CHUKUA HATUA

MAGUFULI NI muadilifu kuliko lowasa

#TunzaKichinjioChakoSubiri25OktobaUchinjeLowasa

Magufuli si msafi hata kidogo ni mchafu sana tena sana.
Nyumba kahonga na amelisababishia taifa hasara ya Trillion 2+ ana usafi gani?
 
Nchi haiongozwi na fikra za rais.Nchi huongozwa na katiba ya wenye nchi.Mtoa mada hata hili hulifahamu?Katiba ya wananchi haipo Tanzania sasa.Tunataka katiba itakayokuwa na uwezo wa kuwafunga Mafisadi.Hata huyo Magufuli kwa katiba ya Fisadi Chenge hana uwezo wakumfunga Chenge.TUNATAKA UKAWA ILI TUPATE KATIBA YA WATANZANIA.Hii itamfunga hata Lowasa mwenyewe akileta jeuri.
 
watanzania tuna shida sana. uzi kama huu unaonesha
1. Tunapenda maneno matupu. maana ccm wanakemea rushwa lakini mgombea mwenza alionekana akitoa hela. ccm inanunua wapinzani kwagharama kubwa.
2.Mwarubaini wa rushwa ni katiba mpya inayozaa taasisi ya kupambana na rushwa yenye meno, polisi na vyombo vya usalama vyenye meno la sivyo ni uasanii tu na ujinga ujinga na kwa hakika watanzania mkichagua tena ccm pamoja na majanga yote waliyosababisha itakua ni ajabu la kumi la dunia.

Hawa ndiyo ccm hongo ni kitu cha kawaida
 

Attachments

  • 1444458652543.jpg
    1444458652543.jpg
    36.4 KB · Views: 45
  • 1444458726859.jpg
    1444458726859.jpg
    31.2 KB · Views: 45
  • 1444458758733.jpg
    1444458758733.jpg
    46.2 KB · Views: 44
  • 1444458967104.jpg
    1444458967104.jpg
    18.7 KB · Views: 46
Kwanza unaota
Ccm haitok na haina sabab ya kutoka madarakan

Huyo mla rushwa na mpiga dili aitwae lowasa akatafute kisiwa huko ndio atawale

Ikulu sio iču
na la sio pango la walanguz

Nidhani una akili kumbe
 

Attachments

  • 1444459752537.jpg
    1444459752537.jpg
    11.8 KB · Views: 77
Chanzo cha ufisadi ktk nchi hii ni ccm.......na ufisadi mwisho wake ni kuiondoa ccm madarakani
 
Kumbe mapambano ya Rushwa ni kusimama majukwaani na KUIKEMEA!
Kwa hiyo Andrew Chenge akisimama jukwaani na kuikemea rushwa (kama anavyofanya sasa kule Baridi) basi hapo atakuwa anapambana na rushwa na yeye atakuwa Mwadilifu!!
 
Tusichambue mada kwa ushabiki wa matumbo yetu. Kuna tofauti gani kati ya kujiuzuru kwa EL na AH Mwinyi?
 
Tusichambue mada kwa ushabiki wa matumbo yetu. Kuna tofauti gani kati ya kujiuzuru kwa EL na AH Mwinyi?
 
Hatutaki kuchagua tena chama chenye ajenda ya kukemea rushwa miaka nenda miaka rudi, bali tunataka chama kitakachoondoa rushwa kwa kuondoa mfumo ulioistawisha na kuchukua hatua moja zaidi ya kukemea.
 
Ufisadi wa EL uko wapi? hata kamati ya Bunge (mwakyembe) ilishindwa kumtia hatiani. Tuache kutumia matumbo yetu kufikiri
 
Jamani, wengi watu bado hatufahamu nini tunataka. Kukemea rushwa ni kazi bure kama Katiba tutakayoipata ndio hio iliyopendekezwa. Tunataka Katiba safi na rushwa wenyewe itaondoka!
Bila ya Katiba safi rushwa hata tukiikemea vipi itaendelea kuwepo miongoni mwetu!
Nani baina ya Magufuli na Lowassa atatupa Katiba Iliyopendekezwa ambayo hatuitaki?
Vote for Lowassa ili upate Katiba itakayokubalika!


Hakika umenena vyema; UKAWA wangejua kujengea hoja zao katika msingi wa katiba mpya njia ingekuwa nyeupe kwend Ikulu tatizo wamegeuka kuwa mabubu wanaotembeana furushi la ahadi kama father xmass
 
Rushwa inaturudisha nyuma sana watanzania , lakini pia tunaambiwa fulani atazuia rushwa kwa sheria zipi ? Kwa sababu takukuru tunao lakini na wao hawafanyi kazi , siamini kama mtu huyu unayemsema ww pia ataweza kukemea hilo .Cha muhimu ni kupata katiba nzuri na sheria nzuri ili tuweze kuwabana wala rushwa.
 
Back
Top Bottom