UKAWA haina ajenda ya kukemea rushwa tena

UKAWA haina ajenda ya kukemea rushwa tena

JMWAKA

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2012
Posts
739
Reaction score
653
Na MwanaJamii

02:41

Kama magufuli ni muadilifu Lowassa sio muadilifu

Kama magufuli anakemea wala rushwa lowasa hakemei wala rushwa

Unaposema bora mchafu mmoja katika kundi la wasafi kuliko msafi mmoja katika kundi la wachafu usisahau kukumbuka kuwa huyo msafi au mchafu yupo katika nafasi gani na uwezo wake na maamuzi yake na mipaka yake na matarajio yake na uwezo wake

HOJA NI KWAMBA

Mchafu mmoja anachafua kundi lote kwasababu yeye ndio kiongozi top na mfano wa kuigwa na kutokana na uchafu wake hawezi kuwanyooshea vidole wachafu wenzake NA msafi mmoja anaweza kusafisha kundi lote kwakuwa yeye Ana mamlaka na uwezo huo

Nafasi inayotafutwa ni ya Urais ambaye ndie amiri jeshi mkuu na mwenye uwezo na mamlaka ya kufagia nyumba sasa umeona wapi mchafu aanze kuwasafisha wenzake wakati yeye ni mchafu

TAFAKARI CHUKUA HATUA

MAGUFULI NI muadilifu kuliko lowasa

#TunzaKichinjioChakoSubiri25OktobaUchinjeLowasa
 
Ajenda yetu UKAWA kwa sasa, ni moja tu, kuiondoa CCM madarakani!!!!!!
 
So what is your solution? Kupigia kura CCM tena? You fail to understand that tatizo ni mfumo mzima sio individual candidate. You should know better than what you wrote.
 
So what is your solution? Kupigia kura CCM tena? You fail to understand that tatizo ni mfumo mzima sio individual candidate. You should know better than what you wrote.

Kama unasema mfumo lazima ufahamu mfumo huanzia juu mpaka chini sasa juu yupo nani na nafasi yake ni nini na nguvu yake ya maamuzi ni ipi ni raisi mfumo upi ni bora katika uadilifu wa lowasa au magufuli rejelea mfumo huanzia juu ss juu Kuna mtu mchafu obvious ataafect hadi chini juzi tu utajiri wa mtoto wa lowasa unakuwa questioned uingereza unatisha tunataka muadilifu kingine nani aliezungumzia kuanzishwa kwa mahakama za mafisadi mbona lowasa hawezi kusema hayoo
 
Jamani, wengi watu bado hatufahamu nini tunataka. Kukemea rushwa ni kazi bure kama Katiba tutakayoipata ndio hio iliyopendekezwa. Tunataka Katiba safi na rushwa wenyewe itaondoka!
Bila ya Katiba safi rushwa hata tukiikemea vipi itaendelea kuwepo miongoni mwetu!
Nani baina ya Magufuli na Lowassa atatupa Katiba Iliyopendekezwa ambayo hatuitaki?
Vote for Lowassa ili upate Katiba itakayokubalika!
 
Kura zote kwa UKAWA!! Hawa CCM hawana jipya, ni porojo zilezile miaka nenda rudi!
 
Kama unasema mfumo lazima ufahamu mfumo huanzia juu mpaka chini sasa juu yupo nani na nafasi yake ni nini na nguvu yake ya maamuzi ni ipi ni raisi mfumo upi ni bora katika uadilifu wa lowasa au magufuli rejelea mfumo huanzia juu ss juu Kuna mtu mchafu obvious ataafect hadi chini juzi tu utajiri wa mtoto wa lowasa unakuwa questioned uingereza unatisha tunataka muadilifu kingine nani aliezungumzia kuanzishwa kwa mahakama za mafisadi mbona lowasa hawezi kusema hayoo

Thats just talk. Politicians will say anything to get elected. Hakuna cha mahakama ya mafisadi mkuu. Do you want to tell me atamshtaki boss wake wa sasa? Au Katibu mkuu wa Chama? Na wengineo? Lets be real.
 
watanzania tuna shida sana. uzi kama huu unaonesha
1. Tunapenda maneno matupu. maana ccm wanakemea rushwa lakini mgombea mwenza alionekana akitoa hela. ccm inanunua wapinzani kwagharama kubwa.
2.Mwarubaini wa rushwa ni katiba mpya inayozaa taasisi ya kupambana na rushwa yenye meno, polisi na vyombo vya usalama vyenye meno la sivyo ni uasanii tu na ujinga ujinga na kwa hakika watanzania mkichagua tena ccm pamoja na majanga yote waliyosababisha itakua ni ajabu la kumi la dunia.
 
Mnajiandaa kukabidhi nchi lakini? Ninaona bado mnavuta shuka wakati kumekucha!.

Ccm wangelikuwa na agenda ya rushwa wasingeihalalisha na kuwa nguzo kuu ya chama na serikali.

Ni majuha wa ccm pekee wanaweza kukosa haya hata kusema eti ccm ina agenda ya rushwa wakati ndio walioikuza na kuwafikisha hapa walipo.

Wakati rushwa inastawi na kukua na nyinyi kuendelea kuikumbatia hadi kuwa ndiyo msingi wa utu kwenye chama na serikali yenu mlikuwa katika hali ya kuwanga, na sasa mmerudi katika mwili?

Ccm acheni upumbavu, mtuachie nchi yetu tuijenge upya.

Rushwa haipiganwi kwa maneno wakati mnai practice hadi hapa mtandaoni kila kinachoandikwa kinyume na ccm kinafutwa ajli ya rushwa.

Ondoeni wendawazimu wenu. Kabidhini nchi kwa amani, upumbvu wowote hatutaukubali. Eti agenda ya rushwa!. Ccm pumbavu kweli kweli.
 
Usipotoshe! Agenda kuu ya Ukawa siku zote ni suala la katiba mpya siyo ufisadi per se. Ukifumua mfumo kwa katiba muafaka tatizo la ufisadi halipo. Ok?
 
Magufuli ni mla rushwa na fisadi, angalia ripoti ya CAG kwa wizara ya ujenzi utaona. Pia amejilimbikizia mali, kule Chato ana bonge la ranchi anafuga ng`ombe na Nguruwe.

Ukija kwenye kukemea rushwa hata Kikwete huwa anakemea rushwa, ila tatizo anakemea kama joka la kibisa bila kuchukua hatua zozote na ndio maana rushwa inaongezeka. Sasa UKAWA tunasema ajenda yetu ni Maendeleo
 
Wewe unafikiri elimu bure itapatikana vipi kama kuna rushwa?
We are done kukemea, tunaenda kuziba mianya yote ya rushwa kwa vitendo ili kuokoa matrillion yanayopotea kwenye rushwa zote hadi za misamaha ya kodi.
Serikali ya CCM imekuwa ikibandika sticker kwenye kuta zote za police stations, hospitali, halmashauri ofisi zote, wakala zote lkn wote tunajua nini kinachoendelea.
 
Kwahiyo unamaanisha kikwete alikuwa ni mla rushwa mkubwa ama?maana ktk ungozi wake kila aina rushwa imefanyika,tafuta watu wakudanganya sio walio elimika kama sisi,shida ni mfumo maana kikwete alikuwa mzuri sana hata kuliko magufuli ila ameshindwa kubadilisha mfuko,mabadiliko nilazima hatuyaombi tene ila nilazima yafanyike
 
Mleta mada ni mfano wa nyumbu wanaovuka mto Mara kule Serengeti...
Wanashindwa kujua tofauti ya mamba na gogo ndani ya mto...
Yaani kila wavukapo wengi wanaliwa na mamba lakini hao hao bado wanapita njia zile zile zenye mamba wala nyumbu..!!!

Miaka nenda rudi ccm wamekuwa wakiifisadi hii nchi lakini wengine bado wanaamini ni mfumo salama... Kwamba ccm na mifumo yake dhaifu ilotufikisha hapa ndo itatuvusha...!!!

Kuna umuhimu wa watu kupata elimu bora ili wawe na fikra sahihi....!! Wajanja nchi nyingine wanabadilisha vyama mara kwa mara ili kuleta ufanisi sisi huku tunajiona tunajua zaidi alafu kwa bahati mbaya tunaishi kwa kutembeza bakuli kuomba misaada kutoka kwao...!!!

Unakalia vito vya thamani kubwa alafu kila siku unazunguka zunguka kwa wengine kuomba omba vito... So insane...!!
 
Hebu nikuulize tena miaka 10 hii imepita kikwete akiwa madaraka nini alikosa ili apambane na rushwa?ukumsikia BBC akisema anayo listi ya wauza pembe ila mfumo haumruhusu kuchukua hatua,watu wamekula tsh 350 billion ila wako home wakizitafuna pole pole hivi unafikiri magufuli ni nani wewe?akili zaki china pelekea nape mwenzako.
 
ukawa hawawezi kukemea ufisadi wala rushwa.
mtekelezaji wa hayo yote ni mtuhumiwa no moja .akifikia hatua hiyo anaishia nachukia umaskini peapooooose asanteni ilani mkasome kwenye websait
 
Back
Top Bottom