Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,866
- 4,252
SIo kwamba haikujiandaa kwa kimakosa bali pengine haikutarajia haya yanayoendelea. Pamoja na Mbowe kusema wengi watahamia Ukawa na chadema, alisema kimhemko na kihisia kulingana na wakati ule. Lowasa aliwahi kuema wakati bado yuko CCM akiwa Dodoma kuwa mtu hawezi kuzuai mafuriko kwa mikono. Kauli hiyo nayo ilijibiwa kishabiki na Nape ambapo sas anaona wazi jinsi mafuriko hayo yalivyo na madhara. Wako viongozi wengi pamoja na wanachama wengi wa ccm watafurikia Ukawa na hasa chadema. Mbowe aliwahi kusema kuwa mwanachama wa siku moja na wa miaka 20 wote wana haki sawa. Kiuhalisia hii si kweli.
Juzi Arusha tumeshuhudia aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani akihamia chadema mbele ya mkutano wa kumtambulisha Lowassa. Masha si mtu mdogo tu. ana ushawishi kwa vijana hasa wa kanda ya ziwa. Ushawiwi wake utakua baada ya wananchi kuona kahamia ukawa. Hili la Masha kuhamia ukawa nililiona kwa sura mbili; kwanza yeye ni kundi la Friends of Lowassa. Pili hakuwania ubunge jimbo la Nyamagana (jimbo la chadema chini ya Wenje) na badala yake kawania Sengerema kwa aliyekuwa mwanaccm mwenzake, Ngeleja. Hiki ni kizazi cha uongozi na kuja kwao ukawa ina maana kuna utafutaji wa madaraka na si uanachama wa kawaida tu.
Bado tutawaona wanaccm wengi tu ambao ni kizazi cha viongozi wakihamia ukawa na chadema. Hawa watu ukawa wanawapokeaje? Watakuwa wanachama tu au watapewa uongozi kama ukawa wakishika Dola? Kama Prof Kitila alivyomnukuu Nkrumah kwamba 'utafuteni kwanza ufalme wa kisiasa na mengine yatafuata'. Baada ya Oktoba ukawa watajipangaje?
Maono yangu ni kuwa miaka mitano ya ukawa madarakani itakuwa ya mkanganyiko sana maana serikali itakuwa na mseto wa hali ya juu ambao haujawahi kutokea katika Taifa hili. Vipaumbele vitawekwa upande gani?
Kwa upande wa ccm wanaweza kukubali kushindwa na wakakaza moyo na kujikunyata pamoja wakijiuliza ni nini kimetokea. Kisha wakaanza kujianga tena taratibu na baada ya miaka mitano wakawa tishio tena kwa ukawa. Kitakachotokea sasa ni kizazi cha viongozi wa ccm 'wanaokatwa' huko kuhamia ukawa kwa shinikizo na upepo wa mabadiliko. Bado tunawasubiri kina Nchimbi, Kingunge, na tetesi kuwa kuna kina Sumaye na wengine.
Napenda tujadili hili. UKAWA imejiandaaje kwa mabadiliko na mapokezi haya?