UKAWA bado kazi nzito, kwa mara nyingine tena ni CCM

TEMBO WANGU

JF-Expert Member
Feb 21, 2014
929
1,277
Wakuu, kama endapo ccm watampitisha john pombe magufuri, basi UKAWA, itakuwa na kazi nzito sana kushinda huu uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, maana magufuri anakubalika ile mbaya, ndani ya ccm na hata nje ya ccm. Pia kumbuka katiba tunayoingia nayo kwenye uchaguzi, ndio ile katiba ambayo inasema matokeo ya urais hayapingwi mahakamani. Kilichobaki ukawa ni kupambana kupata wabunge, pia hata hapo pia itakuwa ngumu sana, maana john pombe, atawanadi kiurahisi sana. Ccm kwa mara nyingine wamecheza karata zao vizuri.
 
CCM watajiuza kwa wananchi kutokana na matokeo waliyoyatoa katika vile waliahidi,kwa miaka 10 ya raisi wa nchi hii tumeona wizi (Ufisadi)umeongezeka na umezoeleka mfano mzuri ni mawaziri walioombwa kujiuzulu na waajiri wao /baraza la mawaziri limevunja rekodi kwa kuvunjwa kutokana na wizi ndani ya Serikali na cha ajabu kabisa hakuna kati yao aliekamatwa/kufunguliwa mashitaka au kufilisiwa..Endelea kuota ndoto mkuu
 
Wakijipanga vizuri wanaweza pati vinginevyo wajipange kuchukua majimbo mengi ili wakamatilie mhimili mkuu wa maamuzi (binge)
 
Kama ni uchaguzi huru na wa haki, fisadi Magufuli hawezi kuwa Rais kwa sababu ni mwizi, fisadi, hajui kupanga hoja/kuzungumza. Hastahili huyu la kabisa.
 
haa haa magufuli ni mgombea mweupe sana kama ukawa watajipanga vizuri.muuzaji wa nyumba za serikali. nakumbuka ule msemo wake wa kivuko...
 
Kati ya tatu bora, AMINA ndiye atakayeoongoza kwa kura nyingi za chuki, wajumbe wameamua kumsimamisha mgombea dhaifu kuipa kazi ngumu ccm kipindi cha kampeni.
 
CCM haina mpango wa kuiacha nchi kwa mpinzani, Tume ya uchaguzi haiwezi kamwe kumtangaza mpinzani kuwa mshindi, haina uwezo huo.

Vv
 
Magufuli anatosha sana tunahitaji MTU mwenye maamuzi thabiti kwa baki ya nchi yetu ilipo fika.
 
Lowassa tu ndio alikuwa anaumiza Kichwa ukawa Ila hao wengine hakuna Kitu ni sawa na kumsukuma mlevi au kusukumiza gari kwenye mtelemko.
 
Wakuu, kama endapo ccm watampitisha john pombe magufuri, basi UKAWA, itakuwa na kazi nzito sana kushinda huu uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, maana magufuri anakubalika ile mbaya, ndani ya ccm na hata nje ya ccm. Pia kumbuka katiba tunayoingia nayo kwenye uchaguzi, ndio ile katiba ambayo inasema matokeo ya urais hayapingwi mahakamani. Kilichobaki ukawa ni kupambana kupata wabunge, pia hata hapo pia itakuwa ngumu sana, maana john pombe, atawanadi kiurahisi sana. Ccm kwa mara nyingine wamecheza karata zao vizuri.

Ccm hawana mvuto tena kwa wananchi hata magufuli ni walewale na anatuhuma pia ukawa wakizitoa kwisha habar yke... Mkomboz wa taifa letu hawez kutoka ccm
 
Back
Top Bottom