UKAWA bado hawajaidhinisha Lowassa na Duni kama wagombea

UKAWA bado hawajaidhinisha Lowassa na Duni kama wagombea

Usiombe maneno haya yakamfikia Askofu Gwajima, sasa hivi utakwambia umevimbiwa marahage na unabwabwaja hovyo.

Naomba uelewe yafuatayo:-
1. Hakuna chama cha siasa kinachohitwa UKAWA
2. UKAWA haina mkutano mkuu au barazaila ni viongozi wa vyama vya CUF, CHADEMA, NCCR - Mageuzi na NLD ambao viongozi wao walikuwepo au kutuma wawakilishi.
3. Mgombea wa urais anatoka CDM na UKAWA wanaunga mkono, hivyo kutano mkuu wa CDM kisheria ndo unaendorse mgombea.
4. CUF hawakuweka mgombea hivyo wameridhia chaguo la CDM.

Hivyo CDM ndio wenye kazi ya kufuata taratibu za vikao kitu ambacho wamefanya.

usiropoke siku nyingine.



Uko sahihi mkuu. Mkutano wa UKAWA ulishakaa zamani na kukubali kuwa CDM ndicho kitakachotoa mgombea. Sasa CDM kimefanya hivyo ridhaa gani nyingine CDM iisubiri? Muda sio rafiki tena inabidi Lowasa asindikizwe kwenda kuchukua fomu kazi ianze.
 
Tatizo wewe ukiidhinisha wewe kama wewe mwanachama wa chama cchako aweza kukuburuza wewe na chama mahakamani kupinga maamuzi yako na huyo uliyemwidhinisha kuwa si mgombea halali wa kuungwa mkono na CHAMA kwa kuwa taratibu za kichama za kuidhinisha ikiwemo kuitisha mkutano mkuu hazikufuatwa!! Ikala kwako na mgombea wako uliyeidhinisha bila kibali cha kikao cha chama!!!

Vyovyote vile ndio ameshakuwa mgombea na mgombea mwenza ameshakuwa Duni. Haujaridhika tu? KAma haujaridhika, basi kubali tu uyaachie hapo.
 
Unaweza kuonyesha hiki kipengele kwenye MoU ya UKAWA? Kama huwez tuachie ukawa yetu! We are more briliant than chama cha makashfa ccm
UKAWA wana wana vyama ambavyo mikutano mikuu yao lazima iridhie kabla ya wao kutangaza chochote.Lowasa kateuliwa na CHADEMA jina lake ilibidi lipelekwe mikutano mikuu ya vyama husika kwa ajili ya kuridhia.Mikutano hiyo mikuu ndio ingewapa Ruksa hao viongozi kuwa na sauti ya kusema CUF,NLD,au NCCR imeridhia!!!! na MGOMBEA mwenza vivyo hivyo!! ilibidi jina lake likajadiliwe baraza kuu la CUF lipate baraka na kuruhusiwa na baadaye lipate baraka toka vikao halali vya vyama vinavyounda UKAWA!!!
 
Vyovyote vile ndio ameshakuwa mgombea na mgombea mwenza ameshakuwa Duni. Haujaridhika tu? KAma haujaridhika, basi kubali tu uyaachie hapo.

Madhara ni kuwa wanachama wa vyama husika waweza zua sintofahamu kupinga vyama husika kuwaunga mkono hao wagombea wawili kwa kuwa taratibu za vyama vyao hazikufuatwa na hakuna ridhaa yao kupitia vikao!!!
 
CUF gani tena imetoa mgomgea? Si mmesema babu Duni kahamia chadema na kapewa kadi? CUF hawana chao! hata kura za rais zitakazotoa wabunge wa kuteuliwa hawatakuwa wa CUF bali ni wa chadema!.elewa hivyo mkuu! CUF hawana chao.

Unaongelea uhalisia na kwakweli kura za rais zitakazotoa wabunge wa kuteuliwa CUF hawatakuwa na chao hayo ndio madhara ya wanaouita UKAWA ila faida yao ni huo umoja wa kuitoa CCM madarakani tu.

Kilichofanyika mi maridhiano tu ya kutimiza nia yao. tangu lini tukaona mtu kuhama chama anahama kwa kukubaliana na chama anachohama tena anakabidhiwa kadi mpya mbele ya katibu wake!!!

Ndio maana nasema CUF wametoa Makamu ila kwakuwa sheria hairuhusu mgombea na mwenza kutoka vyama tofauti ndio maana wakafanya hicho kiini macho. mimi ni miongoni mwa wasioamini maisha (Mafanikio) ya Ukawa na wakivuka hapa kazi najua itakuwa kwa wabunge. pale ambapo M-Chadema aliyeshinda kura za maoni akiambiwa amwachie CUF,NLD au NCCR.

Ngoja tusubiri.
 
Kikao pekee kilichompitisha mgombea uraisi ni Mkutano mkuu wa CHADEMA ulikofanyika Mlimani CITY.Baada ya kumpitisha mkutano mkuu hatua ya pili ilitakiwa Jina la Lowassa lipelekwe kwenye kikao cha UKAWA .

Baada ya kikao cha viongozi wa UKAWA kukaana kujadili na kumptisha Lowasa kuwa ndie mgombea wa UKAWA ndipo UKAWA wangempa kibali Lowassa kupendekeza jina la mgombea mwenza kutoka vyama vinavyounda UKAWA.

Hapo angepeleka maombi kwa chama husika kimruhusu mtu anayempendekeza agombee kama mgombea mwenza.

Chama anakoomba kingeitisha kikao halali cha kujadili ombi hilo na kutoa ruksa kama huyo aliyeombwa abadili chama kwa ruksa ya kikao halali cha chama.

Baada ya hapo Chama husika kingetoa ruksa ya kuhama na kuwajulisha washirika wa UKAWA kwamba kimeridhia kama chama.

Hapo CHADEMA wangetoa kadi kwa mhusika na kuitisha tena mkutano mkuu wa kuridhia uteuzi wa huyo mtu ndani ya CHADEMA

Lakini ule mkutano mkuu wa CHADEMA ukafanya yote,Ukajifanya mkutano mkuu wa CHADEMA na mkutano mkuu wa UKAWA na tawi la kugawa kadi kwa wanachama wapya na kuwatangaza wagombea wenza!

Seif sharif Hamad akakubali kitu kisichokuwepo kiutaratibu ndani ya CUF na kusema anashukuru lowasa kama raisi mgombea na mgombea mwenza kuwa duni haji akageuza mkutano mkuu wa CHADEMA kuwa mkutano mkuu wa UKAWA na Mkutano wa baraza kuu la CUF!!!!!! bila agenda wala chochote.

Kiutaratibu Lowassa bado hajaidhinishwa na mkutano wa Viongozi wa UKAWA kile kilichofanyika mlimani CIty ULIKUWA mkutano mkuu wa CHADEMA sio MKUTANO mkuu wa UKAWA.

Hivyo UKAWA bado hawajapata mgombea Urais na mgombea mwenza hadi pale kikao cha UKAWA. kitakapofanyika.

Usiongee kama upo kona bar,
UKAWA wana mkutano mkuu?
 
kazi najua itakuwa kwa wabunge. pale ambapo M-Chadema aliyeshinda kura za maoni akiambiwa amwachie CUF,NLD au NCCR.

Ngoja tusubiri.

Ni kweli mkuu hapo kazi pevu itakuwepo ingawaje kuna mtu kaniambia watawatupa nje kwa vipengele vifuatavyo

1.Kama mtu hana mchango wa hali na mali kwa chama ajiandae kutolewa
2.Kama haelewani na viongozi wa CHADEMA
3.Kama yeye ni team SLAA
4.Kama yeye haelewani na LOWASA yaani hata kama alikuwa CCM akatimukia CHADEMA na alikuwa haelewani na Lowasa

Lengo kuu la kuwatoa baadhi ya wagombea ni kuwapa nafasi watu wa Team LOWASA ambao hawana majimbo wapate majimbo ya kugombea
 
Mimi napita tu, ils nikiiangalia sura ya chadema naiona mgombea uraisi ccm, mgombea mwenza cuf, sisi wengine nib endera tunafuata upepo tu, mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom