UKAWA acheni za kuleta, Tangazeni nia

UKAWA acheni za kuleta, Tangazeni nia

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Acheni mambo ya kututegea. Watia nia wetu wamejianika na wanachambuliwa kama karanga. Wanachambuliwa kuanzia mikutano yao; udhaifu wao; uchafu wao na uimara wao. Kila mtangaza nia anakumbana na sifa au kejeli za kwelikweli. Nyinyi vipi wenzetu? Nyinyi UKAWA mbona mko kimya?

Njooni uwanjani tuanze kuicheza mechi hii, acheni kujifichaficha!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Acheni mambo ya kututegea.Watia nia wetu wamejianika na wanachambuliwa kama karanga. Wanachambuliwa kuanzia mikutano yao;udhaifu wao;uchafu wao na uimara wao. Kila mtangaza nia anakumbana na sifa au kejeli za kwelikweli. Nyinyi vipi wenzetu? Nyinyi UKAWA mbona mko kimya?

Njooni uwanjani tuanze kuichea mechi hii, acheni kujifichaficha!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Ngoja tuone scud zenu zote then tutakuja na line up ya nguvu. UKAWA kivuli chetu endelea kutuficha tuwachore kwanza!
 
acheni mambo ya kututegea.watia nia wetu wamejianika na wanachambuliwa kama karanga. Wanachambuliwa kuanzia mikutano yao;udhaifu wao;uchafu wao na uimara wao. Kila mtangaza nia anakumbana na sifa au kejeli za kwelikweli. Nyinyi vipi wenzetu? Nyinyi ukawa mbona mko kimya?

Njooni uwanjani tuanze kuichea mechi hii, acheni kujifichaficha!

Mzee tupatupa wa lumumba, dar es salaam

unataka watangaze nia.umoja ufe..bora ufe sept..nk mapema kuruhusu bilo
 
Hatuna haraka sie ati yakhe!! BVR zenu hazifanyi kazi, Kura ya maoni mmeshindwa lakini mnakimbilia kutangaza Nia!!!! Hahahahaaa Mzee mwenzangu kwema lakini??

Kwema kaka yangu. Karibu CCM!

Mzee Tupatupa
 
Mzee Tupa Tupa, ninyi endeleeni na maonyesho wenzenu wanafanya kweli!.

Sijafahamu watia nia wenu kama wanajua kwamba wapiga kura kwa ujumla wao, kama Watanzania bial kjali itikadi wala vyama vya siasa, wanaangalia kivuli cha maneno ya watia nia.

Sielewi JK anawaonaje wanapouza majina kwa kushambulia serikali yake isiyopendwa na wananchi ili waonekane wako upande wa wananchi. Pengine muwe na sera mpya ya maigizo au kutumia ulaghai wowote hata kama ni kudhalilisha chama, ili mradi mpate kura kwenye uchaguzi.

Waulizeni watia nia zenu, mioyo yao inawaambiaje wanapotumia hoja zilizokuwa zikilalamikiwa na UKAWa kwa muda mrefu, kuuza majina wakati wao walisimama kuzipinga bila haya wala uzalendo kadamnasi bungeni. Kuanzia lini zimegeuka kuwa na mantiki kwa ccm?

Wakati gani waaminike wanasema u kweli? Wakati wanachakachua katiba kuumiza wananchi na kupinga hoja zote za maana zinazogusa maslahi ya wanyonge zilizokuwa zikisemwa na upinzani bungeni AU wakati huu wanapogeuka na kuwa wapiga debe wa hoja za UKAWA?

Ila kwa kweli mnaaibika, siyo mchezo.

Fainali October 25.
 
Nyerere wanayempigia magoti kwenye kaburi lake alisema 'ukiona mtu anakimbilia ikulu ni wa kuogopa kama ukoma'.
 
Mbona una halakaaaa
 
Ndani ya UKAWA hakuna demokrasia. Hamad Rashid alitangaza kuwania nafasi ya mwenyekiti wa CUF mpaka sasa kafukuzwa uanachama wa chama hicho. David Kafulila alitangaza kumvaa James Mbatia kuwania uongozi wa NCCR, hata hivyo aliishia kufukuzwa uanachama. Zitto Kabwe alitangaza kuwania uongozi ndani ya CHADEMA kumvaa Mbowe. Kilichomkuta kila mtu anajua. Emmanuel Makaidi wa NLD hajawahi kuitisha mkutano wa uchaguzi. Sasa hayo mambo ya kutia nia yataingiaje ilhali hawajui siasa za ushindani?
 
Acheni mambo ya kututegea.Watia nia wetu wamejianika na wanachambuliwa kama karanga. Wanachambuliwa kuanzia mikutano yao;udhaifu wao;uchafu wao na uimara wao. Kila mtangaza nia anakumbana na sifa au kejeli za kwelikweli. Nyinyi vipi wenzetu? Nyinyi UKAWA mbona mko kimya?

Njooni uwanjani tuanze kuichea mechi hii, acheni kujifichaficha!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Mzee Tupatupa sahihisho kidogo, watangaza nia wenu hawachambuliwi bali wanachambuana wenyewe kwa wenyewe na hii ni neema kwetu.
 
Acheni mambo ya kututegea.Watia nia wetu wamejianika na wanachambuliwa kama karanga. Wanachambuliwa kuanzia mikutano yao;udhaifu wao;uchafu wao na uimara wao. Kila mtangaza nia anakumbana na sifa au kejeli za kwelikweli. Nyinyi vipi wenzetu? Nyinyi UKAWA mbona mko kimya?

Njooni uwanjani tuanze kuichea mechi hii, acheni kujifichaficha!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam


UKAWA wameshajua janja ya nyani kula nyama mbichi ivyo wanamsubiri yule atakaeonekana kwa maccm kuwa ndie bora,ndio wapambane nae. Sio kwa sasa hawa watangaza nia watataka watoke kwa kuwatumia Ukawa. Kama aliyoanza Membe jana, amejisahau kuwa anadaiwa mahela na serikali ya Libya, alizokomba wakati wa marehemu Gaddafi Sio rahisi Ukawa kumtoa mgombea wao kwa sasa kwani wengi watia nia wa MCCM watamshambulia yeye,badala ya kuwaeleza wananchi watawasaidia vp. UKAWA wanaona mbali!!! Mwaka huu mnalo
 
Back
Top Bottom