Ukatil wa kupindukia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukatil wa kupindukia

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Jul 17, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Richard Bukos na Haruni Sanchawa
  Mkazi wa Bunda mkoani Mara, Elisha Makumbati anadaiwa kumfanyia ukatili wa kupindukia mkewe, Nasra Mohammed (38) kwa kumburuza na gari uvunguni, umbali wa mita 150 baada ya kutokea kutoelewana kufuatia wivu wa kimapenzi.
  Akizungumza na gazeti hili dada wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Mwanne Daudi, ambaye alishuhudia tukio hilo alisema:
  “Mdogo wangu alifanyiwa ukatili wa kutisha na mumewe kwani Februari 2, mwaka huu mimi na Nasra tulikuwa tunatoka kwenye saluni moja iliyopo mtaa wa Posta, maeneo ya Bunda.
  “Tukiwa njiani ghafla tulimuona Elisha ambaye ni mumewe akiwa kwenye gari aina ya Nissan Patrol lenye namba za usajili T 400 BBC na kulisimamisha mbele yetu kisha akamuita mdogo wangu kwa hasira.
  “Nasra alivyoenda akamuuliza mumewe, kwa nini alitaka kuwagonga, wakaanza kulumbana na kushutumiana kwa wivu wa kimapenzi,” alisema Mwanne.
  Dada huyo wa marehemu aliendelea kusema huku akitokwa na machozi: “Baada ya kumaliza malumbano yao mimi na Nasra tulianza kuondoka, ghafla tukashtukia mumewe akiondoa gari kwa kasi na kumgonga mkewe na kumburuza kwa umbali wa mita 150 kwa mujibu wa kipimo cha jeshi la polisi lililopima ajali hiyo.
  “Wakati akimburuza mdogo wangu mimi na umati uliokuwa ukishuhudia tulipiga mayowe ya kumtaka Elisha asimamishe gari lakini aliendelea kuongeza mwendo huku damu zikitapakaa barabarani mpaka alipokwenda kukutana na tuta ndipo mwili ukachomoka uvunguni mwa gari.
  “Mdogo wangu Nasra wakati akisagika kwenye lami mimi nilikuwa nikilikimbiza gari hilo kwa nyuma. Nilipofika eneo alilochomoka nilimkuta askari wa usalama barabarani ameshafika na tayari alianza kupima ajali hiyo na muda si mrefu lilifika gari la polisi ‘Difenda’ na kumpakia Nasra na kumpeleka Hospitali ya Bunda, maarufu kama DDH.
  “Alipopimwa aligundulika amevunjika mbavu saba zilizosababisha kutoboa mapafu, mguu wa kushoto na kupata majeraha makubwa mgongoni na sikio la kushoto lilikuwa limenyofoka, kutokana na hali hiyo alihamishiwa Hospitali ya Rufaa Bugando mkoani Mwanza na kufikishiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
  Dada huyo wa marehemu alizidi kusema: “Hali ya mdogo wangu iliendelea kuwa mbaya ambapo Juni 16, mwaka huu, Hospitali ya Bugando ilimpa uhamisho wa kwenda Hospitali ya Taifa ya Rufaa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam ambapo alifikishiwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU)
  “Akiwa Muhimbili madaktari walimtoa nyama za sehemu mbalimbali na kumrudishia mgongoni baada ya kuona nyama yote ya mgongoni zilitoka na kujikusanya sehemu ya makalioni.
  “Marehemu mdogo wangu aliendelea kuugulia maumivu ambapo Jumanne iliyopita, saa saba za usiku aliaga dunia na tumemzika kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar,” alisema Mwanne huku akifuta machozi na akadai mtuhumiwa mpaka sasa yupo huru mitaani.
  Juhudi za gazeti hili kuzungumza na mtuhumiwa huyo ziligonga mwamba baada ya simu zake za mkononi kutopatikana hewani.
  Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa), Ananilea Nkya amelaani kitendo hicho na kulitaka jeshi la polisi nchini kumkamata mtuhumiwa huyo.

  Global Publishers
   
 2. mhalisi

  mhalisi JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,181
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  inasikitisha sana.
   
 3. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkazi wa Bunda mkoani Mara, Elisha Makumbati anadaiwa kumfanyia ukatili wa kupindukia mkewe, Nasra Mohammed (38) kwa kumburuza na gari uvunguni, umbali wa mita 150 baada ya kutokea kutoelewana kufuatia wivu wa kimapenzi.
  Akizungumza na gazeti hili dada wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Mwanne Daudi, ambaye alishuhudia tukio hilo alisema:
  “Mdogo wangu alifanyiwa ukatili wa kutisha na mumewe kwani Februari 2, mwaka huu mimi na Nasra tulikuwa tunatoka kwenye saluni moja iliyopo mtaa wa Posta, maeneo ya Bunda.
  “Tukiwa njiani ghafla tulimuona Elisha ambaye ni mumewe akiwa kwenye gari aina ya Nissan Patrol lenye namba za usajili T 400 BBC na kulisimamisha mbele yetu kisha akamuita mdogo wangu kwa hasira.
  “Nasra alivyoenda akamuuliza mumewe, kwa nini alitaka kuwagonga, wakaanza kulumbana na kushutumiana kwa wivu wa kimapenzi,” alisema Mwanne.
  Dada huyo wa marehemu aliendelea kusema huku akitokwa na machozi: “Baada ya kumaliza malumbano yao mimi na Nasra tulianza kuondoka, ghafla tukashtukia mumewe akiondoa gari kwa kasi na kumgonga mkewe na kumburuza kwa umbali wa mita 150 kwa mujibu wa kipimo cha jeshi la polisi lililopima ajali hiyo.
  “Wakati akimburuza mdogo wangu mimi na umati uliokuwa ukishuhudia tulipiga mayowe ya kumtaka Elisha asimamishe gari lakini aliendelea kuongeza mwendo huku damu zikitapakaa barabarani mpaka alipokwenda kukutana na tuta ndipo mwili ukachomoka uvunguni mwa gari.
  “Mdogo wangu Nasra wakati akisagika kwenye lami mimi nilikuwa nikilikimbiza gari hilo kwa nyuma. Nilipofika eneo alilochomoka nilimkuta askari wa usalama barabarani ameshafika na tayari alianza kupima ajali hiyo na muda si mrefu lilifika gari la polisi ‘Difenda’ na kumpakia Nasra na kumpeleka Hospitali ya Bunda, maarufu kama DDH.
  “Alipopimwa aligundulika amevunjika mbavu saba zilizosababisha kutoboa mapafu, mguu wa kushoto na kupata majeraha makubwa mgongoni na sikio la kushoto lilikuwa limenyofoka, kutokana na hali hiyo alihamishiwa Hospitali ya Rufaa Bugando mkoani Mwanza na kufikishiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
  Dada huyo wa marehemu alizidi kusema: “Hali ya mdogo wangu iliendelea kuwa mbaya ambapo Juni 16, mwaka huu, Hospitali ya Bugando ilimpa uhamisho wa kwenda Hospitali ya Taifa ya Rufaa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam ambapo alifikishiwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU)
  “Akiwa Muhimbili madaktari walimtoa nyama za sehemu mbalimbali na kumrudishia mgongoni baada ya kuona nyama yote ya mgongoni zilitoka na kujikusanya sehemu ya makalioni.

  KWA HABARI KAMILI BOFYA HAPA GUMZO LA JIJI: JAMANI, UKATILI WA KUPINDUKIA
   
 4. kinyoba

  kinyoba JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 1,238
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Mh.. Hii inasikitisha sana na ni vigumu kuamini imefanywa na binaadam mwenzio achilia mbali mpenzi. Natamani ningekuwa hakimu au jaji wa hiyo kesi niitolee hukumu. Baba Kama huyo ndio wale wenye uwezo wa kuua familia nzima kwa ajili ya hasira na mwishowe akajiua mwenyewe. Hafai kuishi kwenye jamii kabisa.
   
 5. Dr.kapama

  Dr.kapama Senior Member

  #5
  Jul 18, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 184
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hayo sio mapenzi,huyo jamaa mshenzi tu...
   
 6. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,878
  Likes Received: 2,829
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli huu ni ushenzi! Hapo utakuta kesi bado inapigwa danadana tu. Hivi huyu si alikuwa wa kuhukumu ndani ya masaa mawili?

  Hivi kweli hata ni wivu wa mapenzi utamfanyiaje mke wako hivyo aisee? Si bora umwache nawe utafute mwingine? Mbona wamejaa tele!!

  Shenzi kabisa hili jamaa halifai kukaa kwenye jamii. Ilitakiwa wananchi wenye hasira walipige mawe hadi life!
   
 7. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #7
  Jul 18, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kituo cha sheria na haki za binadamu,TAMWA, TGNP vipi mbona mko kimya katika hili?
   
 8. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #8
  Jul 18, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hivi yule Mama wa Harakati aliyelishikia bango suala la Ulimboka hahusiki na hili kweli?
   
 9. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #9
  Jul 18, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Si mpaka huyo Baba mwenyewe apatikane,nilikuwa naangalia kipindi cha Wanawake Live cha EATV jana walikuwepo ndugu wa Marehemu pamoja na watoto zake,wanasema Jamaa amekimbia hapatikani inasemekana anapiga misele kati ya Arusha na Dar,sasa sijui hapatikani kweli au ndo Polisi hukatiwa chao kila wanapomuona na wao kutuendelezea wimbo wa hapatikani tunaendelea kumtafuta,inatia uchungu sana, binafsi natamani adhabu ya mtu kama huyu iwe kumchukua na kumuweka mathalani pale kwenye viwanja vya Mnazi mmoja na kutuacha Raia tumhukumu kila mtu kwa anachojisikia,angeipatapata fresh.
   
Loading...