Ukame wa matamasha Tanganyika

Ukame wa matamasha Tanganyika

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,095
Reaction score
828,911
Kweli mwaka 2025 utatuachia kumbukumbu nyingi Sana!
Kwa kawaida na kwa mazoea ya miaka yote kipindi hiki cha sherehe za Christmas na mwaka mpya ni kipindi cha shamrashamra na vibes za kila aina hasa kutoka kwa wasanii wetu
Ni kipindi ambacho radio na tv zinashindana kutangaza matamasha ya wasanii kwenye fukwe za bahari, hotel maarufu, na kumbi mbali mbali za starehe

Ni kipindi ambacho nguzo za umeme na maeneo mengine huchafuka mabandiko ya matangazo ya wasanii ku perform wali na wali huku viingilio vikiwekwa wazi

Ni kipindi ambacho sehemu mbalimbali huteuliwa na kutangazwa kaka maeneo ya kuuzia tickets za viingilio ili kuwarahisishia wapenzi na mashabiki upatikanaji

Leo ni tarehe 24 December siku iliyotarajiwa kuwa na matamasha ya ufunguzi lakini kila nilikopita mitaani na mitandaoni kuko kimya.. Nywiii.. Nywinywinywi kabisa

Watanganyika wameamua kubana bajeti au ndio haya mambo na nongwa za Gen Z?
 
Back
Top Bottom