Ukame umetamalaki, sasa nchi inaelekea kwenye baa la njaa

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Kwa utafiti mdogo niliofanya,asilimia kubwa ya nchi haijapata mvua za kutosha kwa ajili ya kilimo kuanzia mwezi October.

Ni muda muafaka kujiandaa kisaikolojia kupambana na baa la njaa.

Kwa upande wa serikali,hatutaki visingizio,yale mahindi yaliyoko kwenye maghala ya Taifa yaanze kusambazwa Mara moja ili ku-stabilize bei masokoni

Baadhi ya maeneo bei ya mahindi debe inafikia mpaka elfu 20,

Pia,in long term,mikoa inayozalisha mahindi kwa wingi ifunguliwe kwa barabara,hasa ile ya mpanda Tabora.

Mficha ugonjwa kifo humuumbua
 
Umesahau kuwa serikali haikuleta tetemeko! Hivyo hivyo kwenye njaa, ukame serikali is not responsible for those calamities!
 
Tunawaomba wakuu wa wilaya na mikoa wasiogope kutoa taarifa,kama alivyofanya yule wa bunda,unaweza usitoe pia ukawekwa mtu kati

Wale wa kagera,cosmas makongo alishatwambia kwamba kuna njaa,
 
Kujiandaa kisaikolojia siyo njia bora ya kukabiliana na baa la njaa. Baa la njaa linakabiliwa kupitia kuongeza uzalishaji wa chakula. Halafu ukame siyo excuse. Mbona misri ni jangwa ila inajitosheleza kwa chakula?
 
Kipaumbele ni ndege na kubana matumizi si kilimo cha umwagiliaji.
Tumezungukwa na mito na maziwa bado tunalia njaa, Misiri,Ethiopia wanawezaje au wao wanapata Mvua?
Mungu anatuhadhibu wa Tanzania hadi pale tutakapojielewa.
niliwahi msikia mbunge 1 akisema kuwa nchi hii si ya kutegemea kilimo cha mvua, tulime kwa kutumia kilimo cha njia mbadala kama kutumia maji ya mito na maziwa mpaka visima, waziri wa kilimo angejitahidi kuwawezesha wananchi njaa ingekaa pembeni, nakupa mfano, kisiwa cha ukerewe na visiwa voyte 30 vinavyozunguka kile kisiwa, wamezungukwa na maji ya ziwa victoria, lakini kuna shida ya maji kuliko mtu wa tabora na sindiga
 
Ni kweli, nimeenda sehemu debe la mahindi ni 20k, hii ni hatari ukizingatia kuwa mahindi ni zao kuu la chakula kwa watanzania walio wengi.

Serikali ijipange, hatutaki kusikia visingizio kama wakati wa tetemeko.
 
Geita maindi yanazidi kupaaaa juu kwa bei..sipati picha mwez wa 4 yatakuwa sh ngap za kitanzania
 
Labda yule mungu wa Dar es salaam anapimana ubavu na Mungu Mwenyezi wa mbinguni

Pamoja na kilio na sala za yule mama afisa ardhi wa kinondoni na wengine wengi zimefika kwa muumba
 
niliwahi msikia mbunge 1 akisema kuwa nchi hii si ya kutegemea kilimo cha mvua, tulime kwa kutumia kilimo cha njia mbadala kama kutumia maji ya mito na maziwa mpaka visima, waziri wa kilimo angejitahidi kuwawezesha wananchi njaa ingekaa pembeni, nakupa mfano, kisiwa cha ukerewe na visiwa voyte 30 vinavyozunguka kile kisiwa, wamezungukwa na maji ya ziwa victoria, lakini kuna shida ya maji kuliko mtu wa tabora na sindiga

Kama waziri husika hajui namna ya kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji... hiyo akili ya kuwezesha kilimo cha umwagiliaji ataitoa wapi!...
 
Simple law ya commerce ina apply hapo
Less supply,greater demand watu wanalima kipindi hiki,ikumbukwe SGR zilinunua mahindi mpaka zikakosa pa kuweka
Mnaoliombea mabaya Taifa ili Magufuli aonekane hafai ili mpate kiki ya kisiasa mungu anawaona
 
Kutokana na shuguli za binadamu koongezeka kunaleta mabadiliko tabia ya nchi kama ukataji miti ovyo,moshi wa viwanda ambao unapelekea udando wa kuzuia miale ya jua usiufikie uso wa dunia moja kwa moja ndicho chanzo cha kupelekea ongezeko na joto ambalo linauguza mazao shambani
 
Ni kweli, si rahisi kulijua hili iwapo hujasafiri kwa kutumia ndege. Yani kama mikoa ya Dodoma na Singida huko ni jangwa kabisa. Sijui hawa watu wanalima nini... Ila juzi nilisikia mkoa wa Mbeya una ziada ya tani milioni nne za mahindi...
 
Back
Top Bottom