Ukame kuipiga pigo takatifu Bajeti ya 2017/2018,hali ya mapato serikali juu/halmashauri itaporomoka

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,438
14,916
Tanzania hutegemea zaidi sekta ya kilimo izalishe na kisha mazao hayo yapelekwe nje ya nchi.Mazao hayo yakisafirishwa hulipatia taifa fedha za kigeni na pia huvuta makampuni kununua mazao husika

Pia halmashauri hutegemea tozo mbalimbali za mazao ya kilimo ili kujipatia mapato.

Kwa tathmini fupi,kutokana na ukame, asilimia kubwa ya wananchi hawajalima pamba,zao hili tegemeo kanda ya ziwa,litauacha ukanda huo ukiwa na hali ngumu kupindukia kiuchumi,jinery nyingi,karibu asilimia 95 hazitafanya kazi ya kuchambua pamba,kwa uwiano huo huo serikali itakosa mapato

Wananchi hawajalima mpunga,mahindi,karanga,dengu,kutokana na ukame,mpaka sasa bei ya sembe ni Tsh 2000,ikifika mwezi wa tano itakuwa ni kilio kikuu,sembe itauzwa kati ya 2500 na 5000

Tunataraji Bajeti ijayo utakuja na mifumo ya kukopa zaidi na kuwapigia magoti wahisani.

Tukumbuke kilimo kinaajiri asilimia 80 ya watanzania,kwa nchi,kama asilimia 80 imeshindwa kuzalisha kutokana na ukame ni hatari kubwa sana,purchasing power itashuka kwa asilimia 80!!

Ole bado inakuja .....huyo ni Bundi mmoja tu katoka,wapo wengine watatu na nusu wanasubiri
 
kama asilimia 80 imeshindwa kuzalisha - mkuu uwe unaweka source na reference au basis ya asilimia hiyo sio hisia.
 
Tanzania hutegemea zaidi sekta ya kilimo izalishe na kisha mazao hayo yapelekwe nje ya nchi.Mazao hayo yakisafirishwa hulipatia taifa fedha za kigeni na pia huvuta makampuni kununua mazao husika

Pia halmashauri hutegemea tozo mbalimbali za mazao ya kilimo ili kujipatia mapato.

Kwa tathmini fupi,kutokana na ukame, asilimia kubwa ya wananchi hawajalima pamba,zao hili tegemeo kanda ya ziwa,litauacha ukanda huo ukiwa na hali ngumu kupindukia kiuchumi,jinery nyingi,karibu asilimia 95 hazitafanya kazi ya kuchambua pamba,kwa uwiano huo huo serikali itakosa mapato

Wananchi hawajalima mpunga,mahindi,karanga,dengu,kutokana na ukame,mpaka sasa bei ya sembe ni Tsh 2000,ikifika mwezi wa tano itakuwa ni kilio kikuu,sembe itauzwa kati ya 2500 na 5000

Tunataraji Bajeti ijayo utakuja na mifumo ya kukopa zaidi na kuwapigia magoti wahisani.

Tukumbuke kilimo kinaajiri asilimia 80 ya watanzania,kwa nchi,kama asilimia 80 imeshindwa kuzalisha kutokana na ukame ni hatari kubwa sana,purchasing power itashuka kwa asilimia 80!!

Ole bado inakuja .....huyo ni Bundi mmoja tu katoka,wapo wengine watatu na nusu wanasubiri
Asilimia 80 wanangijea mvua ili wawe productive. Hii ndo maana baadhi yetu tuona ingekuwa vema kama serikali ingewekeza kwenye irrigation schemes ili kilimo kiwe na tija kwa wengi wa hao asilimia 80. Badala yake tukaweka bombadia na dream liners na vita dhidi ya upinzani juu kabisa kwenye orodha ya vipaumbele!
 
Kweli kabisa mkuu
 
Dah... Majamaa haya ya UKAWA yanajifariji kweli!

Naona hela za ruzuku za chama zinafanya kazi sawasawa.
 
Sijui kuna watu wameroga waone kama jamaa kweli hatonunua chakula maana si mchezo hii hali, jamaa alilopoka sasa hawa jamaa wamefanya kweli.
Mtulegezee jamani tutakufa.
 
Itakuwa sababu ya kutotwkelezeka kwa budget ya 2016/2017. Utasikia fedha nyingi zilielekezwa kununua chakula badala ya miradi ya maendeleo.
 
Back
Top Bottom