Ukame Kenya wasababisha kufungwa kwa 'Car Wash'

Satuuuu

JF-Expert Member
Dec 3, 2015
1,849
1,993
Habari zenu wadau

Katika kujilinda zaidi na balaa la ukame majirani zetu nchini Kenya wanafikiri kuzifunga sehemu zote za kuoshea magari katika jiji la Nairobi na hasa wale wanaotumia maji toka bomba kuu la serikali.
Pongezi kwenu wakuu kwa kuwa makini na kuikubali hali halisi ya kimazingira.

Source
......Radio.....
 
Hili siyo wazo la kupiga mfano. Kumbuka kuna ajira zitapotea kwa kutekeleza uamuzi kama huu. Ifike mahali tuwe tunafanya maamuzi ya kisera kwa kuhakikisha hatuathiri biashara na hasa ajira za watu.

Kabla ya kuzuia car wash, makapuni ya maji yafanye kazi kurekebisha mabomba yao yanayovuja. Pia yawekeze kwenye vianzio vipya ya maji kila wakati bila kusubiri misaada ya mataifa mengine

Na kama ni lazima kupunguza matizi ya "anasa" kama car wash basi serikali za mitaa zipitishe kodi mpya kwa makampuni ya carwash. Hii itapelekea gharama za kuosha magari kupanda na kuwalazimisha wateja kupunguza idadi uoshaji wa magari yao.
 
Mkuu hii ni kutokana na dharura ya ukame tu ili kulinda maji na kuyatunza ili siku zisonge
 
Habari zenu wadau

Katika kujilinda zaidi na balaa la ukame majirani zetu nchini Kenya wanafikiri kuzifunga sehemu zote za kuoshea magari katika jiji la Nairobi na hasa wale wanaotumia maji toka bomba kuu la serikali.
Pongezi kwenu wakuu kwa kuwa makini na kuikubali hali halisi ya kimazingira.

Source
......Radio.....
Tanzania waosha magari wanavyanzo vingi vya maji ya kuoshea magari sina sababu ya kuvitaja hapa nisiharibu biashara za watu, ila mimi binafsi kutumia maji hayo uliyoita ya bomba kuu ilikuwa mwaka 1996
 
Unapongeze lipi hasa!!
Uzuie watu wasioshe magari!!!
Wao si wanapesa
Waunge bomba kutoka Mombasa
 
Back
Top Bottom