Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,516
Inapotokea kuna hoja zimewasilishwa Bungeni na Kambi ya Upinzani zenye mashiko na zinazohitaji majibu, Mawaziri na Wabunge wa CCM Bungeni Dodoma huwa wakali sana. Badala ya kujadili hoja zilizopo za kibajeti,wachangiaji hujielekeza kwa Wapinzani kwa 'kuwashambulia' kwa maneno ya kejeli na 'mipasho' kwa muda wao wote wa kujadili.
Wewe fuatilia utaona. Kwamba, kama hoja ya Kambi ya Upinzani ina 'ukweli' fulani,wana-CCM Bungeni humo huwa wakali kama nyigu. Kiukweli,leo nimesikitishwa sana na ukali ulioonyeshwa na Prof. Anna Tibaijuka,Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi. Badala ya kujibu hoja za Wabunge wote waliochangia katika Hotuba yake ya Bajeti,yeye akajawa na ukali na kushambulia upinzani hasa Waziri Kivuli wa Wizara hiyo Halima Mdee.
Ukifuatilia kwa makini utaona kuwa ukali wa wana-CCM Bungeni una jambo. Una ujumbe wake mzito kabisa ambao sisi watanzania tunapaswa kuujua. Na ni ukali huo ambao,kwa Bunge hili la Bajeti, Mawaziri wamekuwa hawatoi majibu ya majumuisho yaliyo sawa kibajeti wakitegemea kuzivuruga hoja za Kambi ya Upinzani kwa ukali,kejeli,vijembe na dhihaka.
Ndiyo maana nachelea kuuliza: ukali huu unamaanisha nini?