Ukali wa wana-CCM unamaanisha nini?

Petro E. Mselewa

Verified Member
Dec 27, 2012
9,484
2,000
Inapotokea kuna hoja zimewasilishwa Bungeni na Kambi ya Upinzani zenye mashiko na zinazohitaji majibu, Mawaziri na Wabunge wa CCM Bungeni Dodoma huwa wakali sana. Badala ya kujadili hoja zilizopo za kibajeti,wachangiaji hujielekeza kwa Wapinzani kwa 'kuwashambulia' kwa maneno ya kejeli na 'mipasho' kwa muda wao wote wa kujadili.

Wewe fuatilia utaona. Kwamba, kama hoja ya Kambi ya Upinzani ina 'ukweli' fulani,wana-CCM Bungeni humo huwa wakali kama nyigu. Kiukweli,leo nimesikitishwa sana na ukali ulioonyeshwa na Prof. Anna Tibaijuka,Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi. Badala ya kujibu hoja za Wabunge wote waliochangia katika Hotuba yake ya Bajeti,yeye akajawa na ukali na kushambulia upinzani hasa Waziri Kivuli wa Wizara hiyo Halima Mdee.

Ukifuatilia kwa makini utaona kuwa ukali wa wana-CCM Bungeni una jambo. Una ujumbe wake mzito kabisa ambao sisi watanzania tunapaswa kuujua. Na ni ukali huo ambao,kwa Bunge hili la Bajeti, Mawaziri wamekuwa hawatoi majibu ya majumuisho yaliyo sawa kibajeti wakitegemea kuzivuruga hoja za Kambi ya Upinzani kwa ukali,kejeli,vijembe na dhihaka.

Ndiyo maana nachelea kuuliza: ukali huu unamaanisha nini?
 

Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,386
2,000
Ukali huo unaonyesha ni jinsi gani Mwiba unachoma kuliko!Ndiyo maana kama ningekuwa kwenye viatu vya Madame Tibaijuka na ninauhakika matendo yangu ni masafi na tuhuma si za kweli,ningesema hivi:

Mheshimiwa Spika,nazikubali hoja za upinzani ila hizi tuhuma ningeomba bunge lako lifanye uchunguzi wa kina ili kupata ukweli na kunisafisha.Then ningeendelea na kujibu hoja za wabunge.

Kwa yeye amejikosea heshima,busara,hekima na shule yake haikuonekana maana alikuwa yuko mkali na mpaka uso unaonyesha amechanganyikiwa,na hili limeleta maswali mengi zaidi kuliko majibu.
 

letlive

Senior Member
Oct 25, 2013
117
0
Binadamu anazo silaha mbili za kujipreserve.
Instinct hisia ya mnyama ya kujikinga na hatari ......na will/volition/reason/concious.
Inapokosekana uwiano/Balance katika kutumia zawadi/endowments hizi ndipo binadamu hugeuka zuzu.....,lipi lilizidi kwa prof mama T?
 

Tukundane

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
10,780
2,000
CCM wanajaribu kujinusuru na kifo kwa kupambana na roho inayotaka kuchomoka.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom