Kinachoonekana kuendelea katika Bunge Maalumu la Katiba ni mashindano kati ya Umoja wa Katiba ya Wanachi (ukawa) dhiddi ya Umoja wa katiba ya CCM (ukaccm). Lakini tukizingatia kwamba katiba inayoandaliwa ni ya wananchi, utaona kwamba CCM wamepotoka na hawako na dhamira ya dhati katika kuandaa katiba ya Tanzania itakayosimamia maslahi ya wananchi wote bila ubaguzi. Wanachofanya wao (ccm) ni kupigania katiba ya CCM na mafisadi wachache wachumia tumbo na ambao kila siku wanatamani kuvuna na kutumia rasilimali za nchi kwa manufaa yao binafsi.
Endapo CCM wataendelea na msimamo wao wa kuwahonga baadhi ya wajumbe wa makundi mengine ili wakubaliane na matakwa yao, kuna hatari ya wajumbe wa upinzani na makundi mengine kujitoa wabakie CCM na wasaliti wachache wenye njaa wakaandae katiba yao kwa jinsi wanavyoona na wanavyotaka. Mungu aepushie mbali hili lisitokee kwani mpaka hapa tulipofikia mamilioni ya pesa za wananchi yameishatumika katika mchakato wa kuandaa katiba mpya tangu, kukusanya maoni ya wananchi, kugharimia mabaraza ya katiba na bunge hili linaloendelea sasa.
Mwelekeo mpya bungeni, Pinda atoa hoja kutuliza hali ya hewa - Kitaifa - mwananchi.co.tz
Swali la kujiuliza: Ikiwa CCM wanadhani kwamba kura ya siri nay a wazi zina nguvu sawa, ni kwa nini basi wanganganie kura za wazi na kusababisha mvutano usiokuwa na kichwa wala miguu? Hawaoni kwamba wanapoteza muda wa wanachi na mwisho wa siku bunge litakuchukua zaidi ya siku 70 zilizopangwa na hatimaye kuiingiza nchi katika hasara ya kutumia pesa za ziada kuandaa katiba? Ni lini CCM wataanza kuheshimu maoni ya wananchi waliotoa maoni juu ya aina ya katiba wanayoitaka lakini sasa hivi CCM wanalazimisha kutaka kuichakachua katiba nzima kwa kufuta vifungu vyote na kuchomekea vya kwao na ambavyo vinawanufaisha wao na wachumia tumbo wachache?
Ngoja tusubiri tuone mwisho wa tamthilia hii lakini nina wasiwasi kama tutapata katiba ya wananchi kwani naona CCM wamedhamiria kwa dhati kutaka kupora katiba ya wananchi na kuigeuiza kuwa katiba ya CCM.
:target: