Ukaccm vs ukawa

Ukaccm vs ukawa

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
25,897
Reaction score
25,236
Kinachoonekana kuendelea katika Bunge Maalumu la Katiba ni mashindano kati ya Umoja wa Katiba ya Wanachi (ukawa) dhiddi ya Umoja wa katiba ya CCM (ukaccm). Lakini tukizingatia kwamba katiba inayoandaliwa ni ya wananchi, utaona kwamba CCM wamepotoka na hawako na dhamira ya dhati katika kuandaa katiba ya Tanzania itakayosimamia maslahi ya wananchi wote bila ubaguzi. Wanachofanya wao (ccm) ni kupigania katiba ya CCM na mafisadi wachache wachumia tumbo na ambao kila siku wanatamani kuvuna na kutumia rasilimali za nchi kwa manufaa yao binafsi.

Endapo CCM wataendelea na msimamo wao wa kuwahonga baadhi ya wajumbe wa makundi mengine ili wakubaliane na matakwa yao, kuna hatari ya wajumbe wa upinzani na makundi mengine kujitoa wabakie CCM na wasaliti wachache wenye njaa wakaandae katiba yao kwa jinsi wanavyoona na wanavyotaka. Mungu aepushie mbali hili lisitokee kwani mpaka hapa tulipofikia mamilioni ya pesa za wananchi yameishatumika katika mchakato wa kuandaa katiba mpya tangu, kukusanya maoni ya wananchi, kugharimia mabaraza ya katiba na bunge hili linaloendelea sasa.

Mwelekeo mpya bungeni, Pinda atoa hoja kutuliza hali ya hewa - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Swali la kujiuliza: Ikiwa CCM wanadhani kwamba kura ya siri nay a wazi zina nguvu sawa, ni kwa nini basi wang’ang’anie kura za wazi na kusababisha mvutano usiokuwa na kichwa wala miguu? Hawaoni kwamba wanapoteza muda wa wanachi na mwisho wa siku bunge litakuchukua zaidi ya siku 70 zilizopangwa na hatimaye kuiingiza nchi katika hasara ya kutumia pesa za ziada kuandaa katiba? Ni lini CCM wataanza kuheshimu maoni ya wananchi waliotoa maoni juu ya aina ya katiba wanayoitaka lakini sasa hivi CCM wanalazimisha kutaka kuichakachua katiba nzima kwa kufuta vifungu vyote na kuchomekea vya kwao na ambavyo vinawanufaisha wao na wachumia tumbo wachache?

Ngoja tusubiri tuone mwisho wa tamthilia hii lakini nina wasiwasi kama tutapata katiba ya wananchi kwani naona CCM wamedhamiria kwa dhati kutaka kupora katiba ya wananchi na kuigeuiza kuwa katiba ya CCM.
:target:
 
wanajua CDM ni mabingwa wa kuchukua kura za wanaCCM ktk siri...

sasa iko wazi kwamba CCM wanataka kuvuruga mchakato kufuatia msimamo wa CCM uliotolewa na Rais Kikwete kipindi anazindua bunge la katiba siku ya tarehe 21-03.2014. maCCM hawana nia ya kuandaa katiba mpya. Nia waliyo nayo ni kutaka kuona kwamba mchakato wa utunzi wa katiba unakwama ili waendelee kutumia katiba mbovu iliyopo kwa ajili ya kujichotea na kutafuna mali za umma bila kunawa. cursed be CCM and their supporters!
 
JK kajiuza sana,kwani mashirika ya kimataifa yapo..
 
Mbona mnaongea kama vile CCM sio sehemu ya wananchi na vilevile hawawakilishi wananchi? Kumbukeni kuwa zaidi ya 80% ya wananchi hawakuzungumzia Muungano wakati wa kukusanya maoni kwa kuwa hawakuona tatizo na Muundo wa Muungano! Sasa ya nini ku-create tatizo huku mkijua kuwa halipo kwa kiasi hicho?
 
Tatizo hapa ni baadhi ya watu kutokufahama mantiki ya hoja zao. Kuna baadhi wanadhani hoja zao ndiyo za wananchi bila kufahamu kuwa CCM ni sehemu ya wananchi.
 
Mbona hueleweki na wewe , CCM wanahonga wajumbe wa Bunge la Katiba , wakati hui huo watajitoa?
 
Tatizo hapa ni baadhi ya watu kutokufahama mantiki ya hoja zao. Kuna baadhi wanadhani hoja zao ndiyo za wananchi bila kufahamu kuwa CCM ni sehemu ya wananchi.

Kweli kabisa , huezi kutenganisha wananchi na CCM.
 
Mbona mnaongea kama vile CCM sio sehemu ya wananchi na vilevile hawawakilishi wananchi? Kumbukeni kuwa zaidi ya 80% ya wananchi hawakuzungumzia Muungano wakati wa kukusanya maoni kwa kuwa hawakuona tatizo na Muundo wa Muungano! Sasa ya nini ku-create tatizo huku mkijua kuwa halipo kwa kiasi hicho?

Mimi bado naamini CCM ndiyo itakatupa Katiba zuri, wana nia ya dhati na Muugano wetu.
 
sasa iko wazi kwamba CCM wanataka kuvuruga mchakato kufuatia msimamo wa CCM uliotolewa na Rais Kikwete kipindi anazindua bunge la katiba siku ya tarehe 21-03.2014. maCCM hawana nia ya kuandaa katiba mpya. Nia waliyo nayo ni kutaka kuona kwamba mchakato wa utunzi wa katiba unakwama ili waendelee kutumia katiba mbovu iliyopo kwa ajili ya kujichotea na kutafuna mali za umma bila kunawa. cursed be CCM and their supporters!

Serikali mbili au tatu ni kipengele tu ndani ya Katiba Mpya, hakiwezi kuvuruga Mchakato, labda kama Wapinzani wao wanafikri Katiba mpya ni mjadala juu ya aina ya serikali.
 
Hv hawa wanaojiita ukawa wana hoja gani inayowaondolea ccm kuwa sehemu ya wananchi wa Jamhuli ya Muungano wa Tanzania? Kwanza hilo ni kosa na ni ubaguzi mkubwa sana, bunge la katiba lilihitaji zaidi ya wajumbe 600 na kupitia mchakato halali tulipendekeza uwakilishi kupitia vyama vya siasa , makundi maalum na Taasisi mbalimbali, Sasa iweje leo wazo la kundi fulani au msimamo uwe dhambi? na kwa utaratibu katika michakato hii ya kuandika katiba kuna kupiga kura kuunga mkono hoja fulani sasa hofu inatoka wapi? Ni uhuni tuu na nia mbaya kwa baadhi ya makundi fulani kutaka kuvuruga mchakato huu wa kupata katiba.
 
Wito wangu kwa UKAWA: " Komaeni na msimamo wenu hadi mwisho. Watanzania sasa wanawatazamia kutetea upatikanaji wa Katiba yao dhidi ya ile ya CCM"
 
issue kubwa ni serikali 3

lakini pia mambo ya msingi ni
1. Tume huru ya uchaguzi
2. Idadi ya mawaziri isizidi 15 3. Mawaziri wasiwe wabunge (hili rais alilipinga lakini likae kama lilivyo kwenye rasmu)
4. Madaraka ya rais yapunguzwe
5. Kuwe na mamlaka za kuwathibitisha wanaoteuliwa eg bunge, baraza la mdiwani etc
 
Mbona mnaongea kama vile CCM sio sehemu ya wananchi na vilevile hawawakilishi wananchi? Kumbukeni kuwa zaidi ya 80% ya wananchi hawakuzungumzia Muungano wakati wa kukusanya maoni kwa kuwa hawakuona tatizo na Muundo wa Muungano! Sasa ya nini ku-create tatizo huku mkijua kuwa halipo kwa kiasi hicho?

basi tuambie tatizo la muungano lipo kwa kiasi gani na utushawishi kwa hoja mpaka tukuelewe. na hiyo 80% uliyoipachika kwenye maelezo yako ni kitu gani na umeipataje? usikariri kila jambo kama kasuku.
 
Tatizo hapa ni baadhi ya watu kutokufahama mantiki ya hoja zao. Kuna baadhi wanadhani hoja zao ndiyo za wananchi bila kufahamu kuwa CCM ni sehemu ya wananchi.

'wananchi' wa CCM nchi nzima hawapindukii milioni 2. sasa hiki kikundi kidogo ndiyo kiwasemee watanzania wote milion 45? ebo!
 
Mimi bado naamini CCM ndiyo itakatupa Katiba zuri, wana nia ya dhati na Muugano wetu.

katiba ya CCM itakumaje katiba ya wananchi? ndugu yangu wewe sio mzima. kwa hiyo tuache maoni ya wananchi tufuate maoni ya CCM? are u maniac?
 
Back
Top Bottom