tikatika
JF-Expert Member
- May 6, 2011
- 2,330
- 4,115
Majirani zetu Rwanda hwataki kusikia mtu akijiita mimi ni mhutu au mtusi bali wanajiita wanyarwanda. Hii imetokea baada ya mauji ya wao kwa wao yaliotokea hapo 1994. Tunawashaangaa sana kwann waliuwana kwasababu ya ukabila huku kwetu sisi hatuulizani wewe kabila gani. Tunaoana na yeyote na kufanya kaz na mtu yeyote yule. Lakn kuna balaa kubwa tunalipalilia na kiukweli limeiva kabisa.
Balaa hilo ni ubaguzi wa kisiasa. Warwanda waliuwana kwasababu zinazofanana na sisi . Kabila moja lilijiona ni bora kuliko kabila lingine. Liliona kabila lingine halipaswi kupewa madaraka. Halipaswi kupata elimu. Halipaswi kuwa juu kuliko wao. Waliodharauliwa walipojitutumua matokeo yake yakaja kuwa ni mauaji tunayoyaita ya kimbari.
Katika siasa za Tanzania chama kinachotawala yaan ccm na viongozi wao wanaona vyama vingine hawapaswi kupewa nchi, bali wanaostahili kutawala ni ccm tu. Hilo limejitokeza zanzibar na hata hapa bara. Vyama vya upinzani wanaonekana hawastahili kuongea chochote na wala kupewa madaraka. Sawa hamtaki kuwapa madaraka, lakn hata kuongea hawastahili. Ukiongea chochote katika nchi hii unaitwa mchochezi. Utapewa majina ya kila aina . Tena majina hayo yanatoka kwa viongoz wa ngaz za juu kabisa. Jaman hata sisi ni Watanzania.
Ubaguzi huo umeanza kuzaa matunda kwa baadhi ya maeneo, hususani zanzibar. Watu wameanza kutengana hadi misikitini. Hutengana hata kupeana huduma za jamii yakiwemo maduka kubagua wa kumuuzia bidhaa. Kubwa zaid had kuzikana. Badala ya kuangalia namna ya kurekebisha hali hiyo ndio kwanza viongoz wa kitaifa huzid kuongeza dharau kwa vyama vya upinzani na kuwaona wao si lolote si chochote. Nawashukuru sana viongoz wa upinzani kwa uvumilivu wao. Bila wao nchi hii tungekua tumeleteana noma.
Kuna watu wanawabeza wanachama wa upinzani kwamba waoga. Lakn ni uvumilivu uliowajaa ndio tunaona huu utulivu. Lakn huu uvumilivu una mwisho . Wakija kusema ina tosha hakuna wa kuwazuia. Si majeshi wala hawa polisi . Sijaona popote majeshi yalipowashinda raia wake waliochoka dhuruma na dhihaka dhidi yao. Hawa viongoz wa upinzani siku wakiachia wanachama wajichukulie sheria mkonon hapatakalika.
Wosio wangu kwa wana ccm na viongoz wa kitaifa tenden haki . Muda si mrefu chuki mnayopandikiza italipuka. Hamtakua salama na familia zenu. Maana tunaishi nao mtaan. Wananchi wataanza na wao maana ndio wanaowamudu wakati nyie mnalindwa na majeshi. Mkifikiri ni mbali sana kutengana kisiasa mimi nawaambia tushaanza kutengana ila hatujafungulia kabisa.
Endeleen kutudharau, subilieni matokeo yake. Sisi hatuna cha kupoteza. huku nyie mna mali na vyeo!!