UK yaikatia Uganda misaada kwa tuhuma za rushwa ?


Yericko Nyerere

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined
Dec 22, 2010
Messages
16,675
Points
2,000
Yericko Nyerere

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined Dec 22, 2010
16,675 2,000
Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza, Justine Greening amesema serikali ya London imesitisha misaada ya takribani dola milioni 18 kwa serikali ya Uganda kutokana na kuwepo tuhuma za ufisadi katika ofisi ya Waziri Mkuu.

Greening amesema misaada hiyo haitatolewa hadi pale Kampala itakapochunguza tuhuma hizo na kuchukua hatua zifaazo.

Waziri huyo amesema fedha hizo zinatokana na ushuru wa wananchi wa Uingereza na kwa mantiki hiyo wanataka kuona fedha zao zikitumika kuwasaidia wale wanaohitaji misaada ya dharura.

Katibu wa kudumu katika ofisi ya Waziri Mkuu nchini Uganda anatuhumiwa kufuja fedha za umma hususan zinazotokana na misaada ya kigeni lakini kiongozi huyo amekanusha tuhuma hizo sambamba na kukataa kujiuzulu.

Ikulu ya Rais mjini Kampala pia imeonekana kumkingia kifua katibu huyo kwani imesema haiwezi kumuachisha kazi iwapo hakuna ushahidi unaoonyesha ameiba mali ya umma
 
KING COBRA

KING COBRA

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2011
Messages
2,783
Points
1,225
Age
29
KING COBRA

KING COBRA

JF-Expert Member
Joined Nov 10, 2011
2,783 1,225
Rushwa katika Rada watuhumiwa Uk wamesamehewa na Chenge amaepeta hapa Tz
 
L

LIpili

Member
Joined
Apr 14, 2012
Messages
43
Points
0
L

LIpili

Member
Joined Apr 14, 2012
43 0
Mi nadhani kuna lingine, maana hapa TZ rushwa ipo hadi ofisi ya Rais, misaada ingekuwa imeshakatwa siku nyiingii
 

Forum statistics

Threads 1,296,597
Members 498,672
Posts 31,253,287
Top