Hii ndio tunaita kutia hofu.
Haya mabadiliko kwenye idara hii ya uhamiaji ni muhimu na yanafanywa na nchi yoyote duniani ambayo inatunza takwimu zake sawasawa.
Kuna wahamiaji takriban laki nne ambao wanaishi nchini UK kinyume cha sheria.
Halafu kuna wahamiaji ambao ni wakazi wa kudumu ambao asilimia karibu 90 wanafanya kazi kihalali.
Mwisho kuna kundi hili la ambalo ndio limekuwa likifanyiwa tathmini kwamba linaleta matatizo kwenye ustawi wa jamii (welfare) ambao wanaitegemea serikali kwa kila kitu.
Sasa kwa kuwa hata polisi wa UK mshahara wake unaanzia kwenye £23,000 kwa mwaka, sioni mantiki ya wazo hili.
Wanachokisema ni kwamba mhamiaji yeyote anaetaka kuja UK kuanzia mwaka huu kwa lengo la kufanya kazi au kuishi kwa kufuata mkewe au mumewe ni lazima awe ana ajira inayotoa kipato hicho kinachopendekezwa cha £31,000
Ila wale wapiga boksi wote iwe kiwandani au ofisini ambao mna kazi za kudumu na hamtegemei pesa yoyote kutoka serikalini, hakuna haja ya kuwa na wasiwasi ili mradi una makazi ya kudumu na wala haya mambo hayatokugusa kwa namna yoyote ile.
Soma hii:
Under the proposals:
:: Anyone seeking to settle permanently in the UK must be able to earn between £31,000 and £49,000.
:: The visa system will be improved for short-term business visitors and world-class entertainers.
:: A more formal test will be introduced to establish whether marriages are the result of genuine relationships.
:: Husbands, wives or fiances who cannot speak English will be barred from settling in the country.
Kwa habari kamili nenda hapa:
Immigration Minister Damian Green To Say Only 'Brightest And Best' Migrants Allowed To Enter UK | Politics | Sky News