UK election results

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
51,745
107,899
Exit polls:

Conservatives 307 seats
labour 255 seats
lib dem 59 seats
others 29 seats

conservites 19 seats short of majority
 
wahamiaji wengi wangependa kuona LABOUR inashinda,lakini kwa dalili hii ya exit polls conservative wanaelekea kushinda.
 
Kweli wenzetu wako makini. Upigaji kura ulikwisha saa 4 usiku lakini tayari matokeo yametoka. Afrika kwetu ingechukua mawiki kadhaa kama siyo mwezi. Hivi Tume zetu za uchaguzi zimewahi kujiuliza kwa nini wenzetu wako makini halafu wao wanaacha chaguzi zinaparaganyika na kuzua ghasia na vita vya wenyewe kwa wenyewe?
 
kazi kweli kweli! But at least hawakufisadi kura! Let the system do its work...
 
Kwa matokeo hayo, ndio kumaanisha kwamba ???? Mseto Uu njiani bila shaka ama
 
Kweli wenzetu wako makini. Upigaji kura ulikwisha saa 4 usiku lakini tayari matokeo yametoka. Afrika kwetu ingechukua mawiki kadhaa kama siyo mwezi. Hivi Tume zetu za uchaguzi zimewahi kujiuliza kwa nini wenzetu wako makini halafu wao wanaacha chaguzi zinaparaganyika na kuzua ghasia na vita vya wenyewe kwa wenyewe?

Wenzetu wako mbali kwenye suala la teknologia na miundombinu.
 
Mzawa sio kwamba hatuwezi hiyo teknolojia tunawez sana lakini haitatupa uwezo wa kuiba kura. Nakumbuka nchi za Scandanavia ziliwahi kushauri uwezekano wa kutumika teknologia hiyo ya kisasa kwa uchaguzi wa Zanzibar wakati wa Ben ili kuondokana na matatizo sugu ya hesabu za kura visiwani tena kwa gharama zao akawajibu usitupangie jinsi ya kupiga kura.
 
Ingawa predictions zinaonyesha Conservatives itapata viti vingi kama 310 lakini kutokana na sheria za Waingereza haitaweza kuunda serikali, kinatakiwa chama kipate at least viti 326+, itabidi kuongea na Liberal Dem. party chama cha tatu au vyama vingine vidogo, vinginevyo Labour nayo inaweza kuongea na Liberal kama inavyosemekana inataka kuipiku Conservatives ili ipate support ya Liberal hata hivyo inavyoonekana hata Labour na Liberal wakiungana hawawezi kuvifikia viti itakavyopata Conservative, kwa hiyo ngoma bado mbichi sana lakini mwamzi mkuu ni Liberal Dem. party.
 
Wenzetu wako mbali kwenye suala la teknologia na miundombinu.

Siku zote wanafanya hivi kwa makusudi tu ili wavuruge matokeo.
Jana nilimsikia huyu jamaa anitwa Masilingi akihojiwa BBC pamoja na mzanzibari mmoja ambao wamekwenda kujifunza kwa wenzetu hao jinsi wanavyopiga kura.
Walikuwa wakishangaa kwamba Uingereza hawatumii teknohama yoyote katika mambo ya kura. Walidai hata sisi tunawazidi. Lakini mshangao ulikuwa jinsi walivyo accurate na walivyo faithful katika mambo yao.
Fikilia wenzetu wanapiga kura mpaka saa 4 usiku. Maana yake ni mpaka wapiga kura waishe. Sisi hawa NEC wanatulazimisha tufunge saa 12 jioni.
Kama kuna haja ya kuendelea mpaka apate amri toka kwa mgombea mmoja wapo.
Wenzetu within few hours wana matokeo kamili. Kwetu mpaka atangaze mkurugenzi wa maendeleo wa wilaya tena kwa figures zake tofauti na za vituoni na tena baada ya siku mbili.
Matokeo ya Urais bwana hayo ndio utachoka, kwani yanatangazwa baada ya wiki mbili kama vile yanakuwa processed kwenye sayari nyingine. Ni ajabu kweli.
NEC ni tatizo kweli kwenye chaguzi zetu. Ndio maana yule jaji atafia pale NEC hakuna replacement, hakuna pia tija.

 
BREAKING NEWS
Lib Dem leader Nick Clegg says he sticks to his view that the party with most votes and seats - the Conservatives - should seek to form a government.

Kwa taarifa hii ni wazi kuwa Conservatives na Liberal wata form government of coalition, ndiyo mwisho wa Gordon kwenye no 10. ikulu yao, watu wanasubiri MP atangaze kujiuzuru muda wowote kuanzia sasa.
hadi wakati huu matokeo ni
Conservatives viti...291
Labour viti...251
Liberal viti...52

Kuna jumla ya viti 650 bungeni mshindi majority anatakiwa awe na viti 326 hakuna chama kinachoweza kufikia.
 
Back
Top Bottom