Ujuzi na Platform ya Quora

martial jb

JF-Expert Member
Oct 21, 2021
864
1,456
Habari wakuu,

Nimeona nije kwenu wakubwa ili kupata mafunzo zaidi kuhusiana na mtandao wa quora ambao ni moja ya visima vya ujuzi na maarifa kwa sasa.

Platform hii ina kila aina ya mada ambayo mtumiaji utataka kuisikia au kuijua na pia ni platform nzuri sana kama itatumika kwa masuala ya kielimu.

Changamoto inakuja jinsi ua kuutumia mtandao huu ndo shida inapoanzia, kuna baadhi ya vitu vinakuwa changamoto kwelikweli mfano;

● Kupata topics zinazoendana na matumizi ya kila siku.

● Kupata majukwaa mbalimbali kama vile Elimu, burudani, michezo etc.

●Jinsi ya kujisajili na kuwa updated kwa habari mbalimbali ndo changamoto kweli kweli.

● Na mengine mengi

Hivyo basi wakuu naomba kwa mwenye ujuzi angalau kidogo juu ya haya mambo atufafanulie tupate darasa
 
Ukiwa una scroll down kuna spaces zipo pale nyingi tu unachagua unapenda movies,Technology, historia mbalimbali, sports au mambo ya psychology una follow hizo spaces alaf ukipenda aina flan ya stori unazoletewa unatakiwa u upvote, uki upvode contents za aina fulani unakuwa unaletewa nyingi zaidi kama hizo.

Mi ndo mbinu nazotumia hizo ila kila mmoja na mbinu yake ukiamua una search kitu unachotaka kukifaham.
 
Wakati unajiunga boss walikuletea options ya ku accept ni vitu gani upo interested navyo ili uwe unapata notifications,

Sasa fanya hivi...
Fungua app yao, nenda kwenye Spaces, hapo chini kuna icon inaonesha kama emoji ya watu wa 3... halafu nenda kwenye discover.
 
Quora huwa sichangii sababu sina akili ya kuchangia kule. Hata wakati najiunga JF nilikaa miezi sichangii nikijua sina akili muda huo nilitumia kusoma mada za zamani baadae nikashtuka kumbe sio wote ni great thinkers.

Uzuri wa Quora ID hazifichwi na kila mtu anataja sekta yake. Nasoma comment kuhusu jeshi la Marekani kutoka kwa member ambaye kwenye profile yake imeandikwa ni retired officer, tofauti na huku mganga wa kienyeji anaelezea banking industry. Quora huwa nasoma kupitia email na mada zangu ni zilezile.

Ubaya wa Quora ina michango mifupi, haina maswali mada nyingi sanasana ni maswali, hakuna utani wala masihara. Kupigwa ban ni rahisi sana. Na Wahindi wanaleta bias hasa ukileta mada inahusu China au Pakistan
Screenshot_20231003-220056~2.png
 
Back
Top Bottom