Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 49,264
- 19,595

Kama wewe ni kizazi cha Adam na Hawa basi suala la ndoa linakuhusu sana na ndoa ni kitu beautiful, Kwani huleta mahusiano ya kutosheleza yanayowaunganisha watu wawili mke na mume.
Inapendeza kwamba Mungu amemuumba mtu maalumu kwa ajili yako.
10. UJUZI WA KUTATUA MATATIZO
Kama wanandoa hawana ujuzi wa kutatua matatizo inaweza kusababisha ndoa kuwa ngumu sana hasa miaka 2 ya kwanza katika ndoa.
Kuwa na ujuzi namna ya kutatua matatizo katika ndoa ni kufahamu namna ya kuzozana kwa kuelezana ukweli kwa upendo, kufahamu ni wakati gani wa kukaa kimya au kuzungumza.
9. UJUZI WA KUMWEKA MWENZI WAKO NAMBA MOJA
Kumbuka katika ndoa kuna wewe, mwenzi wako na Mungu.
Jambo la msingi ni uhusiano wako na Mungu wako (siyo kazi ya Mungu, au kwenda kanisani bali uhusiano wako na Mungu, then mwenzi wako (mume au mke) ndipo wanakuja watoto na mwisho kazi.
Kama mke wako anafuata baada ya watoto, mama yako au baba yako au ndugu zako au rafiki zako au TV au Manchester United au chochote kile basi ndoa yako haina jipya na ipo siku mwenzi wako ataona hana maana katika ndoa yenu.
8. UJUZI WA KIMAISHA
Ni muhimu sana kila mwanandoa kufanya vitu ambacho vitakuwa msingi wa maisha ya baadae (future) pia kila mwanandoa analo jukumu la kujiuliza ni namna gani anaweza kuwa mwanandoa mwema miaka 10 au 20 ijayo.
Kila mwanandoa analojukumu la kujiuliza nifanye vitu gani ili niwe mwenye mvuto hata miaka 10 ijayo.
Je, niende shule?
Je, nianzishe biashara?
Je, nifanyeje kumpa support mwenzi wangu katika kazi zake au taaluma yake?